Jinsi jirani alivyoniweka njia panda. Ungefanyaje?

Jinsi jirani alivyoniweka njia panda. Ungefanyaje?

Fohadi

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2020
Posts
772
Reaction score
2,421
Utangulizi:
Huyu dada ni mke wa mtu na ni jirani yangu pale nyumbani ninapoishi. Ni zaidi ya miezi 9 sasa toka nimehamia mtaa ule, ila kwa kipindi chote hiki sijawahi kuwa na mazoea na huyu mwanamke. Huwa ni mwendo wa salamu tu halafu kila mtu anachukua 50 zake. Sina uhakika kama ananijua jina. Sababu kubwa ya kutozoeana sana nadhani ni nature ya maisha yangu.

Mimi nikitoka asubuhi, narudi jioni/usiku na mda mwingi nakuwa ndani tu nafanya mambo yangu. Kiufupi mi sio mtu wa mazoea kabisa hasa kwa wanafunzi na wake za watu. Huyu dada ni mke wa mtu na mmewe ni wale jamaa ambao huwa hawakai sana nyumbani. Siku tatu atakuwepo nyumbani, siku mbili hayupo na huwa tunaonana mara chache sana. Wanaishi nyumba ya jirani na ninapokaa mimi.

Twende kwenye mada:
Jana nimerudi home nikiwa stressed kiasi, sababu ya yule mdogo wetu wa mwisho ambae nishawahi hata kuandika humu kuwa nampenda sana kuliko ndugu zangu wote. Dogo alimaliza form four sasa selection zimetoka amepangiwa shule moja hivi ambayo ndo inaanza sasa kwa matokeo yake na kwa combination aliyokuwa anaitaka/aliyochaguliwa alitegemea kupangiwa hizi shule kubwa kubwa bahati mbaya amepelekwa shule ambayo ndo inaanza kabisaa kwa A level.

Sasa as a brother, jana nimekesha mtandaoni natafuta shule nzuri hasa hizi za serikali halafu nacheki wadau wangu kama wana connection nione namna gani naweza msaidia akapata nafasi kwenye hizo shule.

Nimeendelea kuhangaika hadi usiku mrefu mida ya saa 6 hivi usiku mara nikaanza kusikia kelel nje huko kama watu wanagombana. Nilitaka nipuuzie ila badae ikabidi niwe makini na hizo kelele ukizingatia ni usiku ambao sio wetu. Katika kufatilia nikagundua kuwa ni mke na mme (wale jirani zangu hapo kwenye utangulizi) wanagombana. Baada ya kugundua sio uhalifu, ikabidi niendelee na ratiba zangu tu za usiku. Mambo ya mme na mke chumbani kwao tena usiku sio ya kuingilia kabisaaa.

Nikawaza pengine hata hawapigani huenda jamaa (yule mme) ana ugwadu umejaa kama wa bwana INTEGRITY halafu anapeleka moto kama bwana CARLOS kwa kutumia mikunjo ya bwana EXTROVERT. Nikaendelea kuwaza isije ikawa yule jirani (mke) amenogewa kutokana na kuwa na upwiru uliojaa kama wa bibi NEW GAL basi sauti lazima azitoe kwa juu kama honi la treni inayoweka nanga pale tazara...Nikasema mimi ni nani niingilie mambo yao? hapa ndipo nikamkumbuka bwana SMART911 kuwa mambo yao waachie wenyewe.

Fikra zangu hazikuwa sahihi kabisaa, kumbe ulikuwa ugomvi wa kweli wa kimwili na sio kihisia. Nusu saa baadae nasikia mlango wangu unagongwa na mtu analia sana kwa maumivu makali huku akiniita 'jirani'.

Nilivyochungulia nikamuona ni yule jirani yangu..Ikabidi nimuulize shida nini, akasema kuwa amepigwa na mmewe na amefukuzwa ndani na hana pa kwenda usiku huo. Shida yake kubwa alitaka apate hifadhi angalau alale mpaka asubuhi maana mda ule ulikuwa umeenda sana, ilikuwa inakaribia saa nane usiku. Muda huo anasema mumewe amefunga milango na hataki kumuona.

Huruma ikaniingia sana ila naanzaje kumruhusu mke wa mtu alale kwangu?. Nikamwambia basi mtafute mjumbe angalau akupe msaada, bahati mbaya kwa mjumbe ni mbali kidogo ndio maana hawezi kwenda mda ule. Nikawaza nitoke nikajaribu kuongea na mme wake muda ule?..Nikaona haijakaa poa..Je nitoke usiku ule nimsindikize mke wa mtu hadi kwa mjumbe muda ule...Nikafikilia pia nikaona nitakuwa najiingiza matatizoni...mmewe atanichukuliaje na atawaza kwanini mkewe alikuja kwangu direct usiku ule...Hapana, siwezi nunua ugomvi nikakataa.

Nikamwambia jirani siwezi kukufungulia uingie na wala siwezi kukusindikiza popote..Nikaona ananilaumu sana kuwa jirani yake (mimi) sina huruma na je itakuwaje kama akikutana na madhira usiku ule hata kubakwa..Hakutegemea kama nina roho mbaya kiasi kile.. Alinilaumu sana kwa maneno mabaya ila sikujali, msaada pekee niliompa muda ule ni sh. 10k niliyokuwa nayo nikamwambia akiweza aende hata lodge za jirani akachukue room alale..sikutaka kusikiliza sana lawama zake nikafunika pazia nikazima taa nikalala. Hata mood ya kubaki online ikakata..Sijui aliamua nini baada ya pale.

Leo nimetoka nimekuta pale kwao pamefungwa..Sijui kiliendelea nini baada ya pale, sijui alienda wapi yule mwanamke..Kama wakiyamaliza salama najua atakuwa ananichukulia kama nina roho mbaya sana..sasa ningefanyaje?..Niliamua kuchagua roho mbaya dhidi ya huruma.

Ni kweli, Roho mbaya haijengi ila kuna mda kama jana Roho nzuri inaharibu zaidi...Hizi ndoa zimejaa matatizo mengi sana.

 
Utangulizi:
Huyu dada ni mke wa mtu na ni jirani yangu pale nyumbani ninapoishi. Ni zaidi ya miezi 9 sasa toka nimehamia mtaa ule, ila kwa kipindi chote hiki sijawahi kuwa na mazoea na huyu mwanamke. Huwa ni mwendo wa salamu tu halafu kila mtu anachukua 50 zake. Sina uhakika kama ananijua jina. Sababu kubwa ya kutozoeana sana nadhani ni nature ya maisha yangu. Mimi nikitoka asubuhi, narudi jioni/usiku na mda mwingi nakuwa ndani tu na

Nina mashaka na umri wako. Ishu ndogo kama hiyo inashindwa solve eti jamaa atakuchukuliaje wakati kafukuza mkewe usiku?
 
Nina mashaka na umri wako. Ishu ndogo kama hiyo inashindwa solve eti jamaa atakuchukuliaje wakati kafukuza mkewe usiku?
Wewe ndo umri wako ni wa kutiliwa shaka kabisaaa angekuwa mwanamke mwenzie sawa, Ila kwa mwanaume msaada aloutoa wa kumpa support atafute pa kulala ni sawa kabisa! Ukute wamechokana anatafuta sababu na mwanaume ni mshenzi angejaribu tu kuingiwa huruma hakuna rangi angeacha kuona
 
Ulitakiwa utoke na kumsaidia kwa kumgongea jirani mwenye mke, ili hao majirani wampe hifadhi na ikiwezekana kwenda kwa mjumbe mkiwa team. Lakini kumuacha nje kwa kuhisi mume wake atakuchukuliaje sio sawa.

Ingekuwa ni tabia yao kugombana kila siku, hiyo ungeuchuna.

Do the right thing, not to be seen! But because it is the right thing to do.
 
Ulitakiwa utoke na kumsaidia kwa kumgongea jirani mwenye mke, ili hao majirani wampe hifadhi na ikiwezekana kwenda kwa mjumbe mkiwa team. Lakini kumuacha nje kwa kuhisi mume wake atakuchukuliaje sio sawa.

Ingekuwa ni tabia yao kugombana kila siku, hiyo ungeuchuna.

Do the right thing, not to be seen! But because it is the right thing to do.
Nice comment mkuu...Ndio maana pale juu nimeandika ningafanyaje?...asante sana na nimejifunza next time nitafanya hivi ulivoshauri..asante sana.
 
Back
Top Bottom