Mkalimani wa taifa
JF-Expert Member
- Aug 8, 2020
- 753
- 1,290
mambo yao waachie wenyewe
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe ni mwanaume na nusu+yaani unafikiri kabla ya kutenda yaani nimekuheshimu unaakili sana
Hahahahahha Mr. Ugwadu, hii ilikuwa chance yako ya kuongeza story kule kwenye uzi wa rikiboy...unfortunately nguruwe kaingia kwa shehe hahahha...Mniwie radhi wakuu.Ndugu yangu ulishindwa hata kulala nae kibingwa umpelekee moto umpunguze machungu? umetuaibisha saanaaanaaa, unahitaji hukumu kuu
uliamua vizuri tena kwa busara kuzidi umri wako ila sina uhakika kama utaweza kukabiliana na mitego ya jirani kama kulipwa fadhira kwa huruma uliyonayo na jinsi ulivyojaliToa solution mkuu...age is just a number.
The best advice everUlitakiwa utoke na kumsaidia kwa kumgongea jirani mwenye mke, ili hao majirani wampe hifadhi na ikiwezekana kwenda kwa mjumbe mkiwa team. Lakini kumuacha nje kwa kuhisi mume wake atakuchukuliaje sio sawa.
Ingekuwa ni tabia yao kugombana kila siku, hiyo ungeuchuna.
Do the right thing, not to be seen! But because it is the right thing to do.
Kweli mkuu wanajuana wenyewe huko na wala hata usijichoshe mi nimependa staili yako ya maisha yaani ni maisha flani simple hiviAsante mkuu...tunaambiwa fikiri kabla ya kutenda....angekuwa ni mtoto sawa unaweza amka ukawagongea wazazi wake then akapata msamaha akarudi kulala..ila mke wa mtu amefukuzwa na mumewe...unaamka unaenda kumgongea mwanaume mwenzio tena ambaye sio mshikaji wako/hamna mazoea hata kidogo..Ni ngumu sana.
sometimes heri lawama kuliko hasara...Jamaa atajiuliza kwanini mkewe kaja kwako ikiwa pale labda kuna majirani kibao tu wenye wake...Haiingii akilini...Halafu ile ni usiku, how sure was I kama kweli mmewe amejifungia humo ndani?..je kama huyu mwanamke hata kamuua na anatafuta refuge..kesho jirani unakuwa shahidi..
Ilikuwa ngumu sana kumfanyia fairness yule mwanamke...otherwise angenikuta na akili za usiku...
Sometimes, huruma ya nusu saa inaweza kukupa lawama/majuto ya milele
Shikilia hapo ndugu yangu ushauri wa humu mwingi ni wa kupotosha,tena nasema hivi usije kurogwa kuanza kumuuliza sijui ilikuwaje mara nini kilisababisha mgombane yaani mute tu kama hakijatokea kituKwamba ningemkalibisha home alale kwa amani....aiseeee bora niwe fala maana hata akiniona shujaa haisaidii chochote
Umefanya sahihi. Mume wake ndie mwenye roho nzuri! Watu wengine ni wanga kwa matendo yao.Utangulizi:
Huyu dada ni mke wa mtu na ni jirani yangu pale nyumbani ninapoishi. Ni zaidi ya miezi 9 sasa toka nimehamia mtaa ule, ila kwa kipindi chote hiki sijawahi kuwa na mazoea na huyu mwanamke. Huwa ni mwendo wa salamu tu halafu kila mtu anachukua 50 zake. Sina uhakika kama ananijua jina. Sababu kubwa ya kutozoeana sana nadhani ni nature ya maisha yangu.
Mimi nikitoka asubuhi, narudi jioni/usiku na mda mwingi nakuwa ndani tu nafanya mambo yangu. Kiufupi mi sio mtu wa mazoea kabisa hasa kwa wanafunzi na wake za watu. Huyu dada ni mke wa mtu na mmewe ni wale jamaa ambao huwa hawakai sana nyumbani. Siku tatu atakuwepo nyumbani, siku mbili hayupo na huwa tunaonana mara chache sana. Wanaishi nyumba ya jirani na ninapokaa mimi.
Twende kwenye mada:
Jana nimerudi home nikiwa stressed kiasi, sababu ya yule mdogo wetu wa mwisho ambae nishawahi hata kuandika humu kuwa nampenda sana kuliko ndugu zangu wote. Dogo alimaliza form four sasa selection zimetoka amepangiwa shule moja hivi ambayo ndo inaanza sasa kwa matokeo yake na kwa combination aliyokuwa anaitaka/aliyochaguliwa alitegemea kupangiwa hizi shule kubwa kubwa bahati mbaya amepelekwa shule ambayo ndo inaanza kabisaa kwa A level.
Sasa as a brother, jana nimekesha mtandaoni natafuta shule nzuri hasa hizi za serikali halafu nacheki wadau wangu kama wana connection nione namna gani naweza msaidia akapata nafasi kwenye hizo shule.
Nimeendelea kuhangaika hadi usiku mrefu mida ya saa 6 hivi usiku mara nikaanza kusikia kelel nje huko kama watu wanagombana. Nilitaka nipuuzie ila badae ikabidi niwe makini na hizo kelele ukizingatia ni usiku ambao sio wetu. Katika kufatilia nikagundua kuwa ni mke na mme (wale jirani zangu hapo kwenye utangulizi) wanagombana. Baada ya kugundua sio uhalifu, ikabidi niendelee na ratiba zangu tu za usiku. Mambo ya mme na mke chumbani kwao tena usiku sio ya kuingilia kabisaaa.
Nikawaza pengine hata hawapigani huenda jamaa (yule mme) ana ugwadu umejaa kama wa bwana INTEGRITY halafu anapeleka moto kama bwana CARLOS kwa kutumia mikunjo ya bwana EXTROVERT. Nikaendelea kuwaza isije ikawa yule jirani (mke) amenogewa kutokana na kuwa na upwiru uliojaa kama wa bibi NEW GAL basi sauti lazima azitoe kwa juu kama honi la treni inayoweka nanga pale tazara...Nikasema mimi ni nani niingilie mambo yao? hapa ndipo nikamkumbuka bwana SMART911 kuwa mambo yao waachie wenyewe.
Fikra zangu hazikuwa sahihi kabisaa, kumbe ulikuwa ugomvi wa kweli wa kimwili na sio kihisia. Nusu saa baadae nasikia mlango wangu unagongwa na mtu analia sana kwa maumivu makali huku akiniita 'jirani'.
Nilivyochungulia nikamuona ni yule jirani yangu..Ikabidi nimuulize shida nini, akasema kuwa amepigwa na mmewe na amefukuzwa ndani na hana pa kwenda usiku huo. Shida yake kubwa alitaka apate hifadhi angalau alale mpaka asubuhi maana mda ule ulikuwa umeenda sana, ilikuwa inakaribia saa nane usiku. Muda huo anasema mumewe amefunga milango na hataki kumuona.
Huruma ikaniingia sana ila naanzaje kumruhusu mke wa mtu alale kwangu?. Nikamwambia basi mtafute mjumbe angalau akupe msaada, bahati mbaya kwa mjumbe ni mbali kidogo ndio maana hawezi kwenda mda ule. Nikawaza nitoke nikajaribu kuongea na mme wake muda ule?..Nikaona haijakaa poa..Je nitoke usiku ule nimsindikize mke wa mtu hadi kwa mjumbe muda ule...Nikafikilia pia nikaona nitakuwa najiingiza matatizoni...mmewe atanichukuliaje na atawaza kwanini mkewe alikuja kwangu direct usiku ule...Hapana, siwezi nunua ugomvi nikakataa.
Nikamwambia jirani siwezi kukufungulia uingie na wala siwezi kukusindikiza popote..Nikaona ananilaumu sana kuwa jirani yake (mimi) sina huruma na je itakuwaje kama akikutana na madhira usiku ule hata kubakwa..Hakutegemea kama nina roho mbaya kiasi kile.. Alinilaumu sana kwa maneno mabaya ila sikujali, msaada pekee niliompa muda ule ni sh. 10k niliyokuwa nayo nikamwambia akiweza aende hata lodge za jirani akachukue room alale..sikutaka kusikiliza sana lawama zake nikafunika pazia nikazima taa nikalala. Hata mood ya kubaki online ikakata..Sijui aliamua nini baada ya pale.
Leo nimetoka nimekuta pale kwao pamefungwa..Sijui kiliendelea nini baada ya pale, sijui alienda wapi yule mwanamke..Kama wakiyamaliza salama najua atakuwa ananichukulia kama nina roho mbaya sana..sasa ningefanyaje?..Niliamua kuchagua roho mbaya dhidi ya huruma.
Ni kweli, Roho mbaya haijengi ila kuna mda kama jana Roho nzuri inaharibu zaidi...Hizi ndoa zimejaa matatizo mengi sana.
Alitakiwa akae nje ya chumba chao. Mumewe alitegemea mkewe aende wapi hadi mtu baki ndio ateseke?Ulitakiwa utoke na kumsaidia kwa kumgongea jirani mwenye mke, ili hao majirani wampe hifadhi na ikiwezekana kwenda kwa mjumbe mkiwa team. Lakini kumuacha nje kwa kuhisi mume wake atakuchukuliaje sio sawa.
Ingekuwa ni tabia yao kugombana kila siku, hiyo ungeuchuna.
Do the right thing, not to be seen! But because it is the right thing to do.