Jinsi kuku walivyonizuia kuhudhuria msiba wa kaka yangu

Jinsi kuku walivyonizuia kuhudhuria msiba wa kaka yangu

KISIWAGA

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2015
Posts
8,022
Reaction score
16,563
Ilikuwa mwaka 2011 nilipata kazi ya mkataba wa miaka 2 kijiji kimoja cha huko kwa wahaya

Kutokana na kukuta huko bei ya kuku iko chini nilianza kuwanunua kidogo kidogo ili wakiwa wengi niwe naenda kuwapush Town

baada ya miezi mitatu nilikuwa na kuku zaidi ya 40 ambao nilikuwa ninawahifadhi kwenye chumba kimojawapo cha nyumba niliyokuwa nimepewa kuishi bure

Ikatokea siku nikapigiwa simu nyumbani kuwa kuna msiba wa kaka yangu hivyo nijitahidi nifike mapema kwaajili ya maziko

Baada ya kupokea hizi taarifa niliwasiliana na boss wangu akanipatia ruhusa ili niwahi msibani.Fasta nikaandaa nguo kwenye kibegi,nikaoga na kufanya mawasiliano na sekido aje kunichukua

Sekido hakukawia ndani ya ½ saa alikuwa tayari ameshafika,nikaanza kufunga funga vyumba ili nisepe mida hiyo ni saa 11 jioni lakini ghafla nikawakumbuka kuku wangu

Du nitamuachia nani hawa kuku,je niwafungie chumbani niwawekee msosi & maji vya kutosha halafu nisepe au nifanyeje ?

Pumba zenyewe zilikuwepo kidogo sana,maji nayo yamo kidogo, mfukoni pesa haitoshi,kuku wenyewe bado wengine hawajarejea. dah mambo gani haya sasa yaani mimi Kisiwaga ndio wa kuumizwa kichwa na kuku

Namuachia nani sasa hawa kuku au niwauze,namuuzia nani sasa saa 12 hii

Yule boda wangu nae tayari keshaanza kulalamika kuwa namchelewesha,sasa niwafanyeje hawa kuku.dah saa 1 jioni ikanikuta bado sijuhi nawaachaje hawa kuku wangu vipenzi.

Nikapata wazo kwanini nisihairishe kwenda huko msibani ili nibaki nikiwalea kuku wangu vipenzi(wazo zuri) nikamlipa sekido pesa ya usumbufu nikarudi ndani kupumzika

Kaka yangu kipenzi akawa amezikwa bila mimi kuwepo msibani, iliniuma sana ila sikuwa na cha kufanya
 
KISIWAGA sekido? Umtwekele ? Inchikumi dah long time there, God bless you ila ulifeli why ukumtafuta mtu awepo kwa huo muda? Au ulikuwa tayari ushapita lwabizi? Linas? Oxygeen? Au kill time ndugu yetu.
 
KISIWAGA sekido?umtwekele ? Inchikumi dah long time there , God bless you ila ulifeli why ukumtafuta mtu awepo kwa huo muda ? Au ulikuwa tayari ushapita lwabizi? Linas ? Oxygeen? Au kill time ndugu yetu
Acha kabisa waitu wale kuku walitaka kunifanya kama sina magezi kabisa
 
Huu uzi unabidi uandikwe wahaya tuuu maana sasa dahh wahaya mshaufanya wa makutano 🤣🤣
Naomba toeni comments kwa kiswahili jamani ili Uzi usionekane umekaa kinshomile nshomile
 
Back
Top Bottom