Jinsi lugha ya Kilatini ilivyokufa

Jinsi lugha ya Kilatini ilivyokufa

Mimi nimerudia za kwetu...hizo za wayaudi na warumi zimenishinda....zile mbaya sizifwati...ila nzuri
Tatizo kubwa la hizi za kwetu inaonekana wataalam wa kuwamudu zile roho waliisha wakabaki makanjanja. hatari yake ni unaenda na tatzo dogo unarudi umeibuliwa tatzo kubwa sana jipya. ndo hapo unapoteza mwelekeo kwa hofu ya kufa au kuharibikiwa mambo. ikibidi unafilisiwa. hata hawa wahubiri wapigaji wanaiga staili hii ya waganga ya kuanza na kukutisha na hofu ili wakutaftie suluhu. Mimi nimebaki na amri moja tu USICHOTAKA KUFANYIWA USIMFANYIE MTU. Matatizo mengi anajiundia mtu mwenyewe kwa namna anavyotafsiri mambo au anavyoingiziwa mambo akilini(content). kifupi dunia ilishasetiwa tangu uumbaji kuwa nguvu ya kuwa utakavyo i mikonon mwako. majibu mengi unayo mwenyewe. garbage in garbage out!
 
La lingua cresce man mano che può anche morire.

Nyegezi Seminari ....enzi hizo
 
Leo ndo nimejua Spanish na Latin ni tofauti kabisa.
 
Duh nilijua kiebrania ndio kinaelekea shimo la tewa... kumbe na kilatino nacho![emoji848][emoji848]
Habari za Kiebrania uliskia wapi? Ni lugha rasmi nchini Israeli na lugha ya mamilioni.
Kilatini kinaendelea tu. Si tena lugha inayojadiliwa kama lugha ya mama lakini hasa katika nchi za Ulaya kuna wanafunzi milioni wanaoichagua kama lugha moja shuleni; Italia na Ujerumani ni takriban asilimia 30 za wanafunzi wa shule za sekondari za juu, katika nchi mbalimbali mtihani wa Kilatini ni sharti ya kuingia katika masomo mbalimbali kwenye Chuo Kikuu.
 
upadre ni matokeo ya ufanisi kimasomo seminarin na nidhamu binafs. vyote vikiwa chini ya mwavuli wa NIA YA KUWA KASISI. km hivi ndo wito ..sawa. kinachopunguza wengi ni udhaifu wa standard zao kimasomo, ukosefu wa umakini kwa kila tambo za kinidham, na sera ya siri ya jimbo husika. kuna jimbo linapambana kupunguza finalists kwa sabab mbali mbali ikiwemo uwezo wa kuwatunza. hali hii ufanya jimbo husika kutovumilia error yoyote ya kibinadam. TUSISAHAU HII DUNIA ALITUPWA HUMU SHETAN KAMA MILIKI YAKE BAADA YA VITA KUU MBINGUN KAT YAKE NA MUNGU, KIAS KWAMBA VITU VINGI VITAM DUNIAN VIKO KINYUME NA SHERIA ZA MUNGU WA HUKO MBINGUNI. KANUNI ZA SHETAN ZINAISHIKA KULIKO ZA MUNGU. HATA KAMA NI CHLOROQUIN ILIYOPAKWA SUKARI.
Mkuu nakufatilia 😁🤣🙏 ila inaonekana ulihujumiwa Sana seminarini mpaka kukoseshwa wito. Ila sahivi Kama huna Imani kabisa.
 
Utawala wa Roma haukuanguka. Baada ya kuona mambo magumu wakateka ukristo na kuunda taasis ya ukatoliki. Still ni utawala wa kirumi world wine.
 
.. karne ya 6 baada ya utawala wa warumi kuanguka ndipo lugha hii ilianza kupata kashikashi. Lahaja mbalimbali ziliibuka na kuchota lugha ya kilatini, lahaja hizo za warumi zilikua ni Kifaransa, kireno, kiitaliano, kispanish (kihispaniola) na kiromania.
Hivyo watu waliacha kabisa kuandika na kutumia kilatini na kuanza kucheza na lugha hizo tano.
Picha yako juu ya Kilatini ina hitilafu kidogo. Maana si kweli kwamba Kilatini kilipotea baada ya kuanza kwa lugha za Kiitalia na kadhalika.
Kilatini kiliendelea kote Ulaya kama lugha rasmi kwa shughuli za kiutawala na elimu. Kila msomi alipaswa kujua Kilatini na kutunga tasnia yake kwa Kilatini hadi karne ya 19, wakati mwingine hadi mnamo 1900.
-Martin Luther (mnamo 1517) alifundisha chuoni kwa Kilatini akatunga sehemu ya vitabu vyake kwa kilatini
-Koperniko (mnamo 1450) alieleza mafundisho yake mapya eti Dunia si tena kitovu cha ulimwengu kwa Kilatini
-Kolumbus aliatunga taarifa yake kuhusu kugunduliwa kwa Dunia mpya kwa Kilatini
- Isaac Newton (mnao 1700, aliyetambua kanuni ya graviti) alitunga kitabu chake kikuu Philosophiae Naturalis Principia Mathematica kwa Kilatini

Hii ni mifano michache tu.
Hadi leo majina mengi ya kisayansi yanatungwa kwa kutumia Kilatini; katika nchi kadhaa wanafunzi wa tiba wanapaswa kusoma angalau kozi fupi ya kilatini ili waelewe istilahi za fani yao. Maana majina ya kisayansi si Kiingereza jinsi wengi wanavyoamini, ni Kilatini (kinachotumiwa na Kiingereza maana hawana maneno wenyewe, wanaazima tu)
 
Mnaokoment kwa kilatini mtupatie na maana zake basi tusijedhani mnatutukana....Roma locuta....malizieni bas
 
Back
Top Bottom