Jinsi mapenzi ya mtoto wa Kizulu Durban South Africa yalivyotaka kunitoa roho

Jinsi mapenzi ya mtoto wa Kizulu Durban South Africa yalivyotaka kunitoa roho

Habari wakuu? Nimepitia comments za wadau na kuona karibia kila mtu anataka nisikiruke kipengele cha 071. Halafu nimeona hii thread imepata view nyingi sana. Kulingana na watu wengi kuonyesha kutaka kipengele tajwa nikiweke, nimeona haina budi nikiweke. Ila ningeomba moderators waufute huu let's say baada ya wiki hivi. Maandishi yanadumu, vizazi na vizazi vitakuja kusoma huu uzi na nisingependa uzi huu uwe sehemu ya kuhamasisha hicho kitendo ingawa kitendo chenyewe hakikufanyika. Sasa sina uhakika kama moderators watakuja kuufuta huu uzi au ndio watauacha uendelee kuwepo daima.
Hahaaaa... about 2025.
 
Mwaka 2008 niliingia Durban baada ya kuitwa na jamaa zangu waliokuwa huko. Hawa jamaa zangu tuna undugu pia. Kaka yao kaoa shangazi yetu, na pia kaka yetu kaoa dada yao, ni kama tumeoleana, wao wameoa kwetu na sisi tumeoa kwao. Pia hawa jamaa tumesoma shule moja ya msingi japo madarasa tofauti.

Historia fupi kabla sijaingia Durban. Nilifika South Africa toka 2003. Nilifikia Johannesburg. Joburg nilienda kama volunteer kwenye taasisi moja ya kidini ambayo nisingependa kuitaja. Nikiwa naendelea kufanya kazi kwenye hiyo taasisi niliwaomba wanisaidie kumalizia elimu nyangu ya sekondari. Walinikubalia na process zikaanza kufanyika. Ilibidi nirudi Tanzania kwa ajili ya kwenda shule niliyokuwa nasoma ili kupata nyaraka za kuonyesha nimesoma mpaka level gani maana nilitoka bongo nikiwa hata sijamaliza form three. Mambo yalienda vizuri na niliweza kuanza masomo kwenye shule moja inaitwa Mosupatsela High School iliyopo kwenye kitongoji kinaitwa Kagiso. Kagiso ipo karibu na suburb moja inaitwa Krugersdorp. Nilimaliza high school 2007, na 2009 nikafanikiwa kuingia chuo. Mwaka 2008 ndio nikapata mawasiliano na hao ndugu zangu waliopo Durban, Kwa Zulu Natal.

Huko Joburg sio kwamba sikuwa na mahusiano, mahusiano nilikuwa nayo ila nimeamua kuongelea mahusiano ya Durban maana vurugu za Durban naweza kusema kama ni jembe basi mpini ulivunjikia Durban. Kuna mambo kila nikiyakumbuka yanafurahisha na kuhuzunisha. Durban kuna mambo mengi nimeyafanya, mengine siko proud nayo kabisa. Mojawapo ni hili la mshikaji kumleta demu gheto na tukamla wote wawili, demu mwenyewe alilidhia. Hili wala sitaliongelea.

Mwaka 2008 nikawa nimeingia Durban. Nilipanda basi sehemu moja inaitwa Park station mida ya saa tatu usiku. Saa tisa alfajiri nikawa nimetia timu stand ya mabasi Durban. Nikawacheki wenyeji wangu kwenye simu, wakasema nisubiri kupambazuke watanifuata. Asubuhi jamaa zangu wakaja na kipira kunichukua. Break ya kwanza nikapelekwa sehemu moja inaitwa “the workshop”. The workshop ipo downtown Durban, ipo karibu tu na kituo cha mabasi. Kipindi hicho masela wangu walikuwa na goli la viatu vya kike. Tulipofika hapo workshop jamaa wakawa wanafunga tent ili wapange viatu tayari kwa biashara. Baada ya kumaliza kupanga viatu na movements za watu kwenda kazini zishaanza kuwa nyingi jamaa akaniambia sasa ni muda wa kunipeleka magetoni nikapumzike kwanza. Tukaingia kwenye ndinga na safari ya kwenda magetoni ikaanza. Tukiwa tunaelekea magetoni jamaa akapitia KFC ili nipate kitu cha kwenye mabox kwa ajili ya msosi. Jamaa walikuwa wamepanga sehemu moja inaitwa Rossburg. Walikuwa wamechukua flat nzima yaani floor nzima. Kwenye hiyo flat walikuwa wanashare watu watatu. Flat ilikuwa na vyumba vitatu, sebule moja kubwa, jiko na bafu. Pia kulikuwa na kichumba kimoja kwa ajili ya store. Sasa kwenye hicho kichumba nilikuwa nalala mimi na mshikaji mmoja ambaye pia ni homeboy. Nyumba nzima tulikuwa watu watano, yaani Jamaa zangu wawili walioniita (ni mtu na mdogo wake), Mburundi mmoja, jamaa mmoja Mbongo alikuwa akiitwa baba Isa, na mimi sasa. Hawa jamaa wote walikuwa na mademu zao wa kizulu. So siku ya kwanza ikaisha kwa kupumzika.

Siku ya pili jamaa wakaniambia nikiamka nifanye mpango wa chai kisha nipande taxi kwenda workshop wanakofanyia biashara. Kule daladala zinaitwa taxi. Kule taxi zinaitwa “meter taxi”. Ukisema taxi unamaanisha daladala. Nilipoamka, nikafanya utastaarabu wa chai kisha nikapanda taxi kuelekea workshop. Jamaa enzi hizo walikuwa wanaamuka saa 11 alfajiri kwa ajili ya kujiandaa kwenda kufungua goli. Saa 12 asubuhi yatari wapo kazini. (Sasa hivi jamaa hawauzi tena viatu, wanafanya biashara za magari, ni madon wakubwa. Sembe inalipa).

Maisha rasmi ya Durban yakaanza. Nikawa kila siku naamka alfajiri tunaenda kufungua goli la viatu. Biashara ilikuwa nzuri sana hasa siku za Jumamosi na Jumapili. Workshop siku za Jumamosi na Jumapili ilikuwa inajaa watu sana. Of course hata siku zingine watu walikuwa wanajaa lakini siku za weekends ilikuwa funga kazi. Watu wa Durban na vitongoji vyake siku za weekends ndio siku za kwenda kutembea town. Na ndio siku wabongo huzitumia kwenda kupiga mchomoko maana watu huondoka familia nzima na kwenda town kufurahia maisha. Pia shamrashamra za weekend huko huanza Ijumaa. (Mchomoko ni wizi wa kwenda kuvunja majumba na kuingia ndani na kuiba). Kule ukitaka kumjua kama demu ni wako na anakupenda muombe muonane siku za weekends. Demu wa South Africa, hasa Durban huwezi kumpata siku za weekends. Siku zingine zote utampata lakini weekends never ever. Akija siku ya weekend huyo ni wako na anakupenda.

Safari yangu ya mahusiano nikiwa Durban.

Kuna mademu watano ambao nilijihusisha nao kwa ukamilifu. Achana na wale wakuokota na kupiga na kusepa. Ila nitamuongelea huyu mmoja ambaye aliuteka moyo wangu, nikawa kama zezeta. Na hii ndio sababu imenifanya nianzishe huu uzi baada ya kumkumbuka huyu mtoto wa kizulu na drama zake zilizotaka kunitoa uhai.

Picha linaanza kama ifuatavyo:

Kama nilivosema saa 12 asubuhi tayari tupo workshop tunafunga tent kwa ajili ya kupanga viatu. Kazi ya kufunga tent na kupanga viatu ilikuwa inachukua kama masaa mawili hivi au saa moja na nusu hivi. Kwa hiyo kwenye saa mbili hivi tunakuwa tushamaliza kupanga viatu, na kuanza kutafuta chai. Kulikuwa na mbongo (jamaa) mmoja alikuwa anatupitishia chai na chapati. So, mida ya saa mbili hivi atatuletea chai na chapati. Jina lake alikuwa anaitwa Chaduma. Nadhani masela wa Durban kama wamo humu JF watakuwa wamemnyaka huyu mwamba na huenda wakanijua, ila nitajitahidi kuficha codes zote muhimu ili nisitambulike. Sometimes chapati za Chaduma zilikuwa zinakifu hivyo mtu unaamua kwenda kufungua kinywa sehemu nyingine. Dah! Chaduma alikuwa na maneno ya shombo hatari. Usipokula chapati zake atakusema kwa wabongo balaa. Kwa hiyo sometimes unaamua kula chapati za Chaduma kwa kuogopa kwenda kusemwa kwa wabongo kwamba unaringa.

Siku moja nilichoka kula chapati za Chaduma nikaamua kwenda kutafuta chakula sehemu nyingine. Hiyo siku ndio siku niliyokutana na kipenzi changu Khumbu Mkhize.

Nilipomaliza kufunga tent na kupanga viatu, kabla Chaduma hajafika nikaamua kwenda kufuata chai na vitafunio sehemu moja hivi. Hiyo sehemu ni ng’ambo ya pili kutoka workshop, yaani unatoka nje ya workshop, unavuka barabara ndio unaifikia hiyo sehemu. So, wakati nataka kuvuka barabara nikamuona msichana amekaa kwenye kingo ya barabara kajiinamia kama mtu yupo kwenye lindi la mawazo hivi. Basi nikamsogelea, nikamsemesha. Nikamsalimia, kisha nikamwuliza, vipi? Kulikoni asubuhi hii upo hapa? Akaniambia ana njaa. Nikimcheki ni binti mdogo tu, alikuwa na miaka 18 (nilikuja kujua umri wake baadae tulipokuja kuwa wapenzi). Basi nikampa rand 20 akale, nikamwelekeza goli langu (ninapofanyia kazi) ili akimaliza kula aje tufahamiane zaidi.

Nimechoka kuandika nipumzike kidogo, itaendelea.

Kusoma muendelezo bofya

SEHEMU YA PILI

SEHEMU YA TATU

SEHEMU YA NNE

SEHEMU YA TANO

SEHEMU YA SITA

SEHEMU YA SABA

SEHEMU YA NANE

SEHEMU YA TISA

SEHEMU YA KUMI

SEHEMU YA KUMI NA MOJA

SEHEMU YA KUMI NA MBILI

SEHEMU YA KUMI NA TATU

SEHEMU YA KUMI NA NNE

SEHEMU YA KUMI NA TANO

SEHEMU YA KUMI NA SITA

SEHEMU YA KUMI NA SABA

SEHEMU YA KUMI NA NANE

SEHEMU YA KUMI NA TISA

SEHEMU YA ISHIRINI

SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA

SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI

SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU

SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE

SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO

SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA

SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA

SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE

SEHEMU YA ISHIRINI NA TISA

SEHEMU YA THELATHINI

SEHEMU YA THELATHINI NA MOJA

SEHEMU YA THELATHINI NA MBILI

SEHEMU YA THELATHINI NA TATU

SEHEMU YA THELATHINI NA NNE
Naomba link ya ile stori ya amina
 
Maisha yanaend fasta sana nakumbuka nilikuwa nasoma hii strory live lol years are time scamer
 
Back
Top Bottom