konda msafi
JF-Expert Member
- Sep 5, 2018
- 1,696
- 8,763
- Thread starter
-
- #601
Inaendelea...
Nikawa naumiza kichwa ni namna gani naweza kumtafuta na kuonana na Khumbu bila Sandile kujua. Pia nikawa najiuliza kumtafuta ni swala jingine na kukubali kuonana na mimi nalo ni swala jingine. Kumbuka mara ya mwisho kuwasiliana naye ni kipindi nilipomtolea matusi mpaka akanitishia kunipeleka mahakamani, na mara ya mwisho kuonana ni pale tulipokutana workshop akiwa kabambiwa na msela. Nikawa hata sielewi cha kufanya.
Kwenye yale maeneo ya kuonyeshea mpira kwa ajili ya public pia kulikuwa na maonyesho ya bidhaa mbalimbali kama vile inavyokuwa maonyesho ya sabasaba pale Kilwa road. Kulikuwa na shughuli nyingi tu zinaendelea na watu walikuwa wanajaa hasa. Kabla ya mpira kuanza kulikuwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali locally and internationally wanatumbuiza kwa zamu.
Sandile alikuwa anatoka na kwenda kutafuta matukio kwa ajili ya kuripoti kwenye gazeti hivyo muda mwingi alikuwa akitoka toka na kuniacha peke yangu kwenye tent la VIP, haimaanishi kabisa kuwa nilikuwa nabaki peke yangu, si mnajua burudani ya world cup, lazima upate company nyingi tu humo mnaoshabikia timu moja. Nakumbuka ile siku mchezaji wa Ghana alipokosa penalty kwenye robo finali, tent zima tulijikuta tumekuwa kitu kimoja tunaomboleza. Ilikuwa ni majonzi, ninachotaka kusema hapa company ilikuwa ya kutosha hata pale Sandile alipokuwa ameenda kutafuta matukio.
Kuna muda Sandile alitoka kwenda kutafuta matukio nikaona huu ndio muda wa kumtafuta Khumbu. Nikapiga simu akapokea, nikamwambia nipo hapa kwenye hii sehemu wanapoonyesha mpira kwa ajili ya public kama hatojali tuonane. Akasema yeye yupo nyumbani anachekia mpira nyumbani.
Nikamwomba aje huku tuonane. Akasema anakuja ila akasema tukutane huku kwenye shopping mall hivi iliyokuwa pembeni mwa hiyo sehemu tuliyokuwepo. Basi mimi fasta nikachomoka kwenda kwenye hiyo mall. Akanipigia simu kunielekeza upande tutakaokutania. Basi nikawa nimefika sehemu ya tukio nikawa namsubiria. Haijapita muda nikamuona kwa mbali akija akiwa na rafiki yake. Walivyofika Khumbu akanitambulisha kwa rafiki yake kama mimi ni mtu wake.
Khumbu alikuwa amevaa kikaputula cha jean na jezi ya timu ya taifa ya South africa. Alikuwa amependeza hatari. Kile kikaputula kilikuwa kimemkaa vizuri hatari. Tako lilikuwa linaning'inia kama mzinga wa nyuki. Haraka haraka nilinotice Khumbu amebadirika sana kimuonekano, hakuwa Khumbu yule niliyekutana naye kwa mara ya kwanza.
Alikuwa na muonekano mmoja wa matawi wa juu. Unajua mwanamke anayejijua status yake, anayejijua thamani yake kuna namna flani ana behave kuonyesha ni quality. Halafu nikimcheki tu hata ngozi yake unaona kabisa huyu kwa sasa life lake lipo njema. Kichwani alikuwa amebana nywele zake hivyo kumfanya kuonekana ana sura ndefu nyembamba amazing. Basi baada ya utambulisho akapendekeza tuingia ndani ya mall tutafute sehemu tukae tuongee.
Tukaingia ndani, akamwomba rafiki yake atupe privacy ili tuongee mambo yetu. Tuliongea mengi ila kubwa akaniambia kwa sasa kama ninamtaka nifanye mpango wa kumuoa. Akasema haitaji tena mahusiano ya kutiana tu. Akaniambia nitafute pesa, au nisubiri nimalize chuo nipate kazi. Nakumbuka alisema haya maneno. "Babe South african girls need money". Akaniambia akipata nafasi atanitembelea ila nizingatie alichoniambia. Tukaagana, nikarudi zangu kuendelea kuangalia mpira.