Jinsi mazingira uliyokulia yanachelewesha mafanikio yako

Jinsi mazingira uliyokulia yanachelewesha mafanikio yako

Wakusolve

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2020
Posts
561
Reaction score
997
Jinsi Mazingira uliyozaliwa yanaweza kukuchelewesha kufanikiwa.

Mazingira yanamchango mkubwa wa mtu kufanikiwa, ukiwa kwenye Mazingira sahihi ni rahisi kupiga hatua.Mazingira uliyozaliwa au home town yanaweza kuwa kikwazo cha mtu kutopiga hatua kivipi.

1. Marafiki uliokuwa nao, unapokuwa kwenye mazingira uliokulia au kuzaliwa unakuwa na marafiki wale wale ambapo ukibadilika kutaka kutimiza ndoto zako wanaweza kukukatisha tamaa, kukupinga na kukurudisha nyuma, ili uweze kufika kwenye kutimiza ndoto zako unaitaji watu wenye maono kama yako.

2. Kukosa msaada au kutengwa, unapokuwa kwenye jamii ambayo umekulia na wewe una ndoto kubwa tofauti na watu waliokuzunguka utapata upinzani mkubwa sababu watu hawata tamani uwapite kimafanikio hivyo itakulazimu utumia nguvu kubwa sana.

3. Kukuchukulia wa kawaida na kutumia makosa yako ya nyuma kukurudisha nyuma, unapokuwa kwenye jamii uliyozaliwa na wewe unapambania ndoto zako watu watakukejeli na kusambaza makosa yako kwa watu ambao unashirikiana nao kwenye kutimiza ndoto zako hivyo ni muhimu kuelewa hivi.

4. Mtazamo wako na fursa, unapokuwa kwenye mji ulio zaliwa akili yako inakuwa aijafunguka sababu ni jamii umeishi nayo muda mrefu, unapo badilisha mazingira, unapata fursa ya kujifunza kwa watu wapya, utamaduni, tabia, akili inakuwa hivyo unakuwa na uwezo wa kufanikiwa kimaisha katika angle nyingi.

Vitu gani ufanye ili utimize ndoto zako

Lazima utambue ni muhimu kuondoka sehemu uliyozaliwa ili uweze kutimiza malengo yako, utakuwa huru na pia utapata msaada.

Mungu alipotaka amubariki ibrahimu alimwambia aondoke sehemu aliyozaliwa na ibrahimu akafanya hivyo akapata baraka na utajiri.

Yesu alianza huduma yake kwenye mji wa galilaya na mji wake aliozaliwa nazareth watu wake walimkataa na kutomuamini hii inatufundisha umuhimu wa kuondoka sehemu tulizo zaliwa na kupambana na ndoto zetu miji mingine ambapo utapata msaada na kuungwa mkono na watu wengine.
 
Hiyo hoja yako ni sawa na kuamini uganga ,ni vyema kama unaamini ufuate ila kwangu BIG NO.

Ninachoamini mimi riziki yangu iko pale nilipozaliwa ,ni kutafuta sababu na juhudu ili kupata hiyo riziki...I love Tanga ,I love home.

Hizo hoja zako zimesababisha miji mingi kufa na kukosa wazalisha ; watu wanekimbilia mjini.
 
Back
Top Bottom