Jinsi mazoezi yanavyoweza kumfanya mtu kuonekana younger

Traxtion

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2021
Posts
8,000
Reaction score
16,414
Watu wengi wakiona picha za “before and after” za watu walioanza kufanya mazoezi, mara nyingi hushangazwa na jambo moja, mtu anaonekana mdogo kuliko zamani. Wengine huonekana kama wamerudisha miaka yao nyuma kabisa. Swali ni, hii hutokeaje?
Ukweli ni kwamba mazoezi yana mchango mkubwa sana katika muonekano wa mwili, ngozi, uso, nguvu na hata namna mtu anavyoonekana mbele za watu. Hapa chini ni baadhi ya sababu zinazofanya watu wanaofanya mazoezi waonekane younger kuliko umri wao halisi.

1. Mazoezi Huboresha Mzunguko wa Damu
Unapofanya mazoezi, moyo unasukuma damu kwa ufanisi zaidi kwenda sehemu mbalimbali za mwili. So inasaidia ngozi kupata oxygen na virutubisho vya kutosha. Matokeo yake unakuwa na ngozi yenye afya, inayong’aa na kuonekana fresh muda wote.
traits-healthy-woman-own-glow-make-time-move.jpg

2. Mazoezi yanapunguza mafuta Yasiyo ya Lazima
Mafuta mengi mwilini, hasa usoni na shingoni, yanaweza kufanya mtu aonekane mkubwa au mchovu. Mazoezi husaidia kupunguza mafuta hayo na kufanya shape ya uso na mwili ionekane vizuri zaidi. Jawline huonekana vizuri, uso huonekana lighter na wenye muonekano wa ujana.
Mfano angalia picha ya mwanaume, before na after kufanya mazoezi
Face fat loss didn_t come from shortcuts or magic workouts. It came from showing up on days I...jpeg

.
Kwa wanawake pia, mazoezi yana mchango mkubwa kwenye kupunguza mafuta ya usoni, shingoni nk na kufanya mtu aonekane younger na mrembo pia

3. Hupunguza Stress
Stress ni moja ya vitu vinavyozeesha watu haraka. Msongo wa mawazo unaweza kuathiri usingizi, ngozi, nguvu na hata facial expressions za mtu. Mazoezi husaidia mwili kutoa hormones kama endorphins ambazo hupunguza stress na kufanya mtu ajisikie vizuri zaidi.
overview_image_160130728_10590786.png

4. Huboresha Usingizi
Watu wanaofanya mazoezi mara nyingi hulala vizuri zaidi. Usingizi mzuri ni muhimu sana kwa afya ya ngozi, macho na mwili kwa ujumla. Mtu anayelala vizuri huwa anaonekana mwenye nguvu na mwenye afya zaidi.
shot-of-a-young-man-sleeping-peacefully-in-bed-at-home.jpg

5. Mazoezi huboresha Posture na Muonekano wa Mwili
Mazoezi huimarisha misuli ya mgongo, mabega na kiuno. Kwa hiyo inasaidia kumfanya mtu asimame vizuri zaidi badala ya kukaa au kutembea akiwa ameinama. Posture nzuri humfanya mtu aonekane confident, smart na younger.

6. Huongeza Confidence
Mtu anapoona mwili wake umebadilika na afya yake kuwa bora, confidence huongezeka. Confidence nayo huathiri namna mtu anavyoonekana mbele za watu. Mara nyingi watu wenye confidence huonekana vijana zaidi kuliko wale waliokata tamaa au wenye stress nyingi.
healthy-young-black-man-running-outdoors-beach-45302307.jpg

7. Mazoezi Huboresha Afya ya Mwili kwa Ujumla
Mazoezi husaidia moyo, mapafu, mifupa na misuli kufanya kazi vizuri zaidi. Mwili wenye afya huonyesha dalili zake nje pia. Ndiyo maana watu wengi wanaofanya mazoezi kwa muda mrefu huonekana energetic hata wanapokuwa na umri mkubwa.

Mazoezi siyo tu kwa ajili ya kupunguza uzito au kujenga misuli. Pia yana uwezo mkubwa wa kuboresha muonekano wa mtu na kumfanya aonekane younger kuliko umri wake halisi. Ukiunganisha mazoezi, lishe bora na usingizi mzuri, mwili na ngozi hubadilika kwa kiwango kikubwa sana.
Ndiyo maana mara nyingi ukiona picha za before and after za watu waliodumu kwenye mazoezi, unaweza kudhani ni watu wawili tofauti.
 
Watu wengi wakiona picha za “before and after” za watu walioanza kufanya mazoezi, mara nyingi hushangazwa na jambo moja, mtu anaonekana mdogo kuliko zamani. Wengine huonekana kama wamerudisha miaka yao nyuma kabisa. Swali ni, hii hutokeaje?
Ukweli ni kwamba mazoezi yana mchango mkubwa sana katika muonekano wa mwili, ngozi, uso, nguvu na hata namna mtu anavyoonekana mbele za watu. Hapa chini ni baadhi ya sababu zinazofanya watu wanaofanya mazoezi waonekane younger kuliko umri wao halisi.

1. Mazoezi Huboresha Mzunguko wa Damu
Unapofanya mazoezi, moyo unasukuma damu kwa ufanisi zaidi kwenda sehemu mbalimbali za mwili. So inasaidia ngozi kupata oxygen na virutubisho vya kutosha. Matokeo yake unakuwa na ngozi yenye afya, inayong’aa na kuonekana fresh muda wote.
View attachment 3587559
2. Mazoezi yanapunguza mafuta Yasiyo ya Lazima
Mafuta mengi mwilini, hasa usoni na shingoni, yanaweza kufanya mtu aonekane mkubwa au mchovu. Mazoezi husaidia kupunguza mafuta hayo na kufanya shape ya uso na mwili ionekane vizuri zaidi. Jawline huonekana vizuri, uso huonekana lighter na wenye muonekano wa ujana.
Mfano angalia picha ya mwanaume, before na after kufanya mazoezi
View attachment 3587553View attachment 3587554
.
Kwa wanawake pia, mazoezi yana mchango mkubwa kwenye kupunguza mafuta ya usoni, shingoni nk na kufanya mtu aonekane younger na mrembo pia
View attachment 3587557

3. Hupunguza Stress
Stress ni moja ya vitu vinavyozeesha watu haraka. Msongo wa mawazo unaweza kuathiri usingizi, ngozi, nguvu na hata facial expressions za mtu. Mazoezi husaidia mwili kutoa hormones kama endorphins ambazo hupunguza stress na kufanya mtu ajisikie vizuri zaidi.
View attachment 3587560

4. Huboresha Usingizi
Watu wanaofanya mazoezi mara nyingi hulala vizuri zaidi. Usingizi mzuri ni muhimu sana kwa afya ya ngozi, macho na mwili kwa ujumla. Mtu anayelala vizuri huwa anaonekana mwenye nguvu na mwenye afya zaidi.
View attachment 3587562

5. Mazoezi huboresha Posture na Muonekano wa Mwili
Mazoezi huimarisha misuli ya mgongo, mabega na kiuno. Kwa hiyo inasaidia kumfanya mtu asimame vizuri zaidi badala ya kukaa au kutembea akiwa ameinama. Posture nzuri humfanya mtu aonekane confident, smart na younger.

6. Huongeza Confidence
Mtu anapoona mwili wake umebadilika na afya yake kuwa bora, confidence huongezeka. Confidence nayo huathiri namna mtu anavyoonekana mbele za watu. Mara nyingi watu wenye confidence huonekana vijana zaidi kuliko wale waliokata tamaa au wenye stress nyingi.
View attachment 3587558

7. Mazoezi Huboresha Afya ya Mwili kwa Ujumla
Mazoezi husaidia moyo, mapafu, mifupa na misuli kufanya kazi vizuri zaidi. Mwili wenye afya huonyesha dalili zake nje pia. Ndiyo maana watu wengi wanaofanya mazoezi kwa muda mrefu huonekana energetic hata wanapokuwa na umri mkubwa.

Mazoezi siyo tu kwa ajili ya kupunguza uzito au kujenga misuli. Pia yana uwezo mkubwa wa kuboresha muonekano wa mtu na kumfanya aonekane younger kuliko umri wake halisi. Ukiunganisha mazoezi, lishe bora na usingizi mzuri, mwili na ngozi hubadilika kwa kiwango kikubwa sana.
Ndiyo maana mara nyingi ukiona picha za before and after za watu waliodumu kwenye mazoezi, unaweza kudhani ni watu wawili tofauti.
for sure mazoezi ni tiba mujarabu sana, naweza kusema katika kila changamoto ya kiafya ambayo mwanadamu anaweza kua nayo,

well done gentleman kwa bandiko mujarabu sana kuhusu mazoezi na faida zake:KasugaYeah:
 
Mazoezi yanasindikizwa na
Lishe bora
Maji ya kutosha
Matumizi haba ya vilevi
Mapunziko ya kutosha
Stress kiduchu..kutoweka vitu moyoni
Hapo kwenye maji ya kutosha, ni wachache sana wanaojitahidi kufuata
 
Back
Top Bottom