Jinsi mbunge Ramadhan Kihiyo alivyojiuzulu baada ya kashfa ya kufoji vyeti

Jinsi mbunge Ramadhan Kihiyo alivyojiuzulu baada ya kashfa ya kufoji vyeti

Mwezi September mwaka 1996 kulitokea tukio la kihistoria ambapo mbunge wa Temeke bwana Ramadhan Kihiyo alijiuzulu ubunge kwa sababu za kiafya baada ya kushindwa kesi ya uchaguzi.

Vyama za NCCR mageuzi na Chadema walifungua shauri mahakamani kudai ushindi wa jimbo la Ubunge kwa kuwa Ramadhan Kihiyo alitumia vyeti vya kughushi wakti akiwania nafasi hiyo katika uchaguzi wa wabunge wa mwaka 1995.

Pia ilidaiwa kuwa bwana Kihiyo wakati wa kampeni alikuwa akigawa takrima ya pesa, fulana na katika mzunguko wa pili wa uchaguzi alikuwa akigawa bure maji ya kunywa kwa wapiga kura walokuwa wakimsikiliza katika mikutano yake ya kampeni.

Ikumbukwe kuwa tume ya uchaguzi ilifuta matokeo ya kwanza ya uchaguzi huo na katika mzunguko huu wa pili namba ya wapiga kura ilishuka kwa asilimia 39 katika watu 143.749 na hii ilikuwa ni baada ya bwana Kihiyo kuwatishia wapiga kura ambao ni wafanyabiashara za uchuuzi kwamba wasingepata leseni zao za biashara.

Baada ya kutangazwa matokeo ya mzunguko wa pili, bwana Kihiyo alipata kura 37,303 kati ya kura 57,152 zilizopigwa na ilidaiwa kuwa baadhi ya vituo vya kupigia kura vilikuwa vikitozwa ada kubwa ya pango na vingine kubadilishwa kiasi cha kuwachanganya wapiga kura na kuwakatisha tamaa.

Hivyo NCCR Mageuzi pamoja na Chadema wakaamua kuingia mahakamani kudai kiti hicho cha ubunge ambacho iliaminiwa kilipatikana kwa hila za bwana Ramadhan Kihiyo.

Kesi hiyo ilifunguliwa katika mahakama kuu ya Tanzania na ilikuwa ikisikilizwa kwa makini na watanzania khasa baada ya kuwepo madai ya kwamba bwana Ramadhani Kihiyo hakuwa na vyeti stahiki kuitwa Dakta Kihiyo "Title" ambayo alikuwa akiitumia.

Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano baina ya wakili wa upande wa NCCR Mageuzi na Chadema Dk Masumbuko Lamwai na Ramadhan Kihiyo, sehemu ambayo ilimmaliza kabisa kisiasa mwanasiasa huyo feki.

Dakta Lamwai: Ulisema ulimaliza chuo cha ufundi cha Dar-es-Salaam mwaka 1986. Hiyo ni sawa?

Kihiyo: Ndiyo , bila shaka.

Lamwai: Unamfahamu mtu yule? ( akimwonyesha mwenyekiti wa baraza la wanafunzi wa Dar tech)?

Kihiyo: Hapana, simfahamu.

Lamwai: Karakana ni nini?

Kihiyo: Sifahamu (kicheko kutoka kwa watu walio sehemu ya wasikilizaji).

Lamwai: Kuna vitengo vingapi ndani ya karakana ya ufundi kwenye chuo cha ufundi?

Kihiyo: Kuna chumba cha injini, chumba cha pump na cha kufanya kufanyia matengenezo (Kicheko).

Lamwai: Unayo karatasi yoyote inayoonyesha alama ulizopata?

Kihiyo: Nafikiri ninayo iko mahali.

Lamwai: Unamtambua mkuu wa chuo wakti ukiwa chuoni?

Kihiyo: Hapana Simfahamu.

Lamwai: Nani alikuwa ni msajili wa wanafunzi?

Kihiyo: Mr Kuhanga.

Lamwai: Hapana. Mr Kuhanga wakti huo alikuwa ni makamu mkuu wa chuo kikuu cha Dar-es-Salaam.

Lamwai: Lini ulianza masomo pale chuoni?

Kihiyo: Sikumbuki.

Dr. Lamwai aliiambia mahakama kwamba Kihiyo alitumia cheo cha uhandisi wakti wa kampeni kuhusiana na uwezo wake wa kutatua matatizo ya maji katika jimbo la Temeke.

Jaji alimuamuru Kihiyo aleta cheti chake mahakamani siku ilofuata..

Kihiyo: (Siku ilofuata). Mheshimiwa jaji naomba siku mbili zaidi , ili niweze kutafuta cheti changu.

Lamwai: Bado unasisitiza kwamba ulimaiza chuoni hapo?

Kihiyo: Ndiyo.

Dr. Lamwai aliendelea kumhoji bwana Kihiyo kwa kumuuliza kuhusu muda alokuwa pale chuoni, madai kwamba alikuwa ni mkuu wa idara pale Dar Tech ni nani alimtunuku cheti siku ya mahafali na ni masharti gani ya kujiunga na chuo yalikuwepo.

Kihiyo hakuwa na jibu na wakai mwingi alitoa majibu yasiyo sahihi.

Lamwai: VTC inasimama kuwakilisha nini?

Kihiyo: National Committee Centre (kicheko).

Lamwai: Sasa nakutaka uachie kiti cha ubunge wa Temeke.

Baada ya kisanga hiki cha kupigwa chini na Dakta Lamwai, Ramadhan Kihoyo aliandika barua ya kujiuzulu kwa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akitoa sababu za kiafya na ikakubaliwa mara moja.

Mbunge wa Kwela wakti huo Christiant Mzindakaya alisimama bungeni mwezi huhuo na kusema kwamba badala ya Dakta Lamwai hakuwa comrade mzuri yaani badala ya kuwasaidia wabunge kwa kutumia ujuzi wake wa sheria yeye alikuwa akisaidia kuwaondoa bungeni.

Kweli CCM imetoka mbali.

Tuunge mkono juhudi zinazofanywa za kuiimarisha CCM,kuibadili na kuweka katika mstari ulonyooka na kuwa chama chenye kupokea mabadiliko.
 
..sasa hebu tueleze nini kilimkuta Dr.Lamwai mpaka akaamua kurudi CCM.

..majuzi nimesoma habari gazetini Dr.Lamwai anapambana na mwanafunzi wake Tundu Lissu mahakamani.

..Tundu Lissu angeshinda ubunge mara ya kwanza alipogombea angeingia bungeni pamoja na Dr.Lamwai, Mabere Marando, James Mbatia, Ndimara Tegambwage, ..
 
..sasa hebu tueleze nini kilimkuta Dr.Lamwai mpaka akaamua kurudi CCM.

..majuzi nimesoma habari gazetini Dr.Lamwai anapambana na mwanafunzi wake Tundu Lissu mahakamani.

..Tundu Lissu angeshinda ubunge mara ya kwanza alipogombea angeingia bungeni pamoja na Dr.Lamwai, Mabere Marando, James Mbatia, Ndimara Tegambwage, ..

Mwaka 2004 Lamwai alipatikana na hatia ya professional Misconduct na akapigwa ban ya mwaka mmoja.

Na baadae pia nafikiri ni mwaka huohuo wa 2004 alikuwa na kesi nyingine inayohusiana na "dereliction" au kukimbia majukumu ambapo alimtelekeza mteja wake.

Mwisho hao wote ulowataja ni wamoja na wanabadilishana tu uzoefu wa kutumia vifungu vya sheria lakini kwa kuwa TL ni mbishi tangia akiwa shule aking'ang'ania kitu basi ndiyo twashuhudia hizi drama.

Mfano ni kesi ya uchaguzi ya mwaka 2016 kati ya Dr Kiruswa na Onesmo Nangole ambapo Dr Lamwai "successfully" aliwezesha kupatikana ushindi kwa Dr Kiruswa na Onesmo Nangole kushindwa kesi na baada akuvuliwa ubunge.

Lakini Tundu Lissu aingia kumsaidia Nangole kukata rufaa na pia kila Dr Lamwai aliposhiriki kutetea mteja yoyote yule TL huingia na ukiangalia hata kesi ya Bulaya ni hivyohivyo.

Hivy utaona ushindani wa aina fulani baina ya wanasheria hawa na vita yao haitakwisha soon.
 
Kwa habari ya KIHIYO ilikuwa ni NCCR ,ila umejitahidi kuingiza na Chadema. Chadema haikuhusika.
Usiipe sifa ambayo Haikuwa nayo
 
Mwaka 2004 Lamwai alipatikana na hatia ya professional Misconduct na akapigwa ban ya mwaka mmoja.

Na baadae pia nafikiri ni mwaka huohuo wa 2004 alikuwa na kesi nyingine inayohusiana na "dereliction" au kukimbia majukumu ambapo alimtelekeza mteja wake.

Mwisho hao wote ulowataja ni wamoja na wanabadilishana tu uzoefu wa kutumia vifungu vya sheria lakini kwa kuwa TL ni mbishi tangia akiwa shule aking'ang'ania kitu basi ndiyo twashuhudia hizi drama.

Mfano ni kesi ya uchaguzi ya mwaka 2016 kati ya Dr Kiruswa na Onesmo Nangole ambapo Dr Lamwai "successfully" aliwezesha kupatikana ushindi kwa Dr Kiruswa na Onesmo Nangole kushindwa kesi na baada akuvuliwa ubunge.

Lakini Tundu Lissu aingia kumsaidia Nangole kukata rufaa na pia kila Dr Lamwai aliposhiriki kutetea mteja yoyote yule TL huingia na ukiangalia hata kesi ya Bulaya ni hivyohivyo.

Hivy utaona ushindani wa aina fulani baina ya wanasheria hawa na vita yao haitakwisha soon.
Alaa kumbe!
 
Ramadhan Ali Kihiyo alikubunge wa Temeke alishinda uchaguzi wa Temeke....

aadae NCR Mageuzi ilienda Mahakamani kupinga kwakua Mtuhumiwa alitumia vyeti visivyo vyake.

Yafuatayo ni Mahojiano Ya Dr.Lamwai na Mtuhumiwa Kihiyo.

Lamwai: You say you graduated from the Dar es Salaam Technical College in 1986. Is that right?.

Kihiyo: Yes, of course.

Lamwai: Do you know that man? (pointing to former Technical College Students Council Chairman)?

Kihiyo: No, I don’t know him.

Lamwai: What is a foundry?

Kihiyo: I don’t know (laughter from the packed public gallery).

Lamwai: How many sub-departments are there in the Mechanical Department of the College?

Kihiyo: An engine room, an injection pump and repair (laughter).

Lamwai: Do you have any paper indicating what marks you got?

Kihiyo: I think I have it somewhere.

Lamwai: Do you know who the Principal of the College was when you were there?

Kihiyo: I don’t know.

Lamwai: Who was the Registrar?

Kihiyo: Mr Kuhanga.

Lamwai: No. Mr Kuhanga was my Vice-Chancellor at the University of Dar es Salaam at that time.

Lamwai: When did you start your studies there?
Kihiyo: I don’t remember.

Dr. Lamwai told the court that Kihiyo had used the title engineer during the campaign in relation to his ability to solve water problems affecting the constituency. The Judge asked Kihiyo to bring his certificate to court.

Kihiyo: (Next day). Your Honour, can you please give me two more days to look for the document.
Lamwai: Do you still maintain that you graduated from the College?

Kihiyo: Yes.

Dr. Lamwai then asked about the stream he had been in, his Head of Department’s name, who had presented the certificate to him, what were the entrance requirements but in every case Kihiyo either did not know or gave the wrong answer.

Lamwai: What does VTC stand for?

Kihiyo: It is National Committee Centre (laughter).

Lamwai: I ask you to step down as MP for Temeke

On May 29, following a month in the High Court, Mr Kihiyo announced through his counsel that he had written to the House of Assembly Speaker resigning as MP for Temeke on medical grounds.
Asee
 
I think the title "kihiyo" representing someone with empy head started from that time.
 
Rip Masumbuko Lamwai Umetangulia sijui shida nini au upumuaji ulisumbua?
 
Back
Top Bottom