Jinsi Meli ya Titanic inavyo zidi kuoza tazama picha

James Cameroon alisema sio kila kitu kwenye ile movie ni cha kweli
Kuna matukio mengine ni ya kusadikika tuu
 
Ni ndoto yangu siku moja kwenda chini ya bahari kutalii niione natafuta pesa siku moja nikawaone Oceangate wanipe utaratibu
KWel tuko tofauti Mungu alituumba, mimi natafuta ila zaidi ya kula kunywa na kuwa na afya na kutunza familia yangu, na kusubiri kurudi kwa Mungu, sina cha ziada nilicho na hamu nacho hapa dunian, hizo habar za kusafir na adventures and the likes, are never found on my to do list when am on earth
 
AI generated images.
 
Kinacho nishangaza ni huo mwaka, 1912 hao jamaa walikuwa na maarifa ya kujenga meli kubwa kihasi hicho. Sasa najiuliza ivi sisi wabongo tunashidwa nini leo hii 2024 kufanya vitu vikubwa zaidi.
Mkuu linapokuja suala la tech mzungu kitu kingine, kuna meli ya MV LIEMBA kanda ya ziwa huko, nayo ina takriban miaka 100.

Tutafute pesa tununua vitu vya ulaya, Mchina tunatumia vitu vyake sababu ya umaskini wetu tu.
 
Sisi huku kijijini kwetu wazee wakishirikiana na babu yangu wamefanikiwa kutengeneza ndege isiyotumia mafuta wala umeme!
Kinacho nishangaza ni huo mwaka, 1912 hao jamaa walikuwa na maarifa ya kujenga meli kubwa kihasi hicho. Sasa najiuliza ivi sisi wabongo tunashidwa nini leo hii 2024 kufanya vitu vikubwa zaidi
 
Naomba kujibu swali la vipande viwili vya meli hizo kuwa kama vimetofautiana.

Meli ilipogonga mwamba ule wa barafu (eneo la kati la meli), ilianza kukatika eneo la kati, sehemu ya nyuma ikaelemewa na uzito, meli ikaanza kukatika hapo, kipande cha nyuma kikatangulia kwenda chini.

Baada ya kipande cha kwanza cha nyuma kwenda chini, baada ya muda ndo kipande cha mbele kikaanza kwenda chini pia.

Hivi vipande viwili vipo umbali wa tofauti tofauti, havipo sehemu moja, ni kama zaidi ya mita mia kutoka kipande kimoja hadi kipande cha pili kilipo.
 
James Cameroon alisema sio kila kitu kwenye ile movie ni cha kweli
Kuna matukio mengine ni ya kusadikika tuu
Mojawapo ni la First officer Mr. Murdoch kuua watu wawili na yeye pia kujipiga risasi
lakini pia kwamba mahaba ya jack na rose pale yalipelekea lookouts Frederick Fleet na Reginald Lee kuchelewa kuona barafu mbele, na mengine mengi sana. Japo jamaa alijitahidi mno ku base katika matukio mengi halisi.
 
Sisi nasi technology yetu ya kutiana mazagaza tumboni nayo ikaangaliwe.
Au mtu anaruka na ungo, faamchezo nini!! Uwezo tunao ila in a negative way
Hata tungekuwa na uwezo wa tech kama wazungu bado kuna vijitabia vinamrudisha nyuma mwafrika uswahili, wizi, kuchawiana, roho mbaya, tamaa, uroho wa madaraka n.k...

Tuna safari ndefu sana, japo jamii nyingine duniani sikatai wana tabia hizo lakini kwetu ni too much, too much is harmful...
 
Photoshop. Ile meli likatika katikati na sehemu kubwa ya mbao zake ziliondoka na watu. Hiyo nzima kabisa. Halafu mbona mara imelala mara imesimama, au ndo ichunguzi unaendelea?
hehehe kweli ilikatika katikati, na wewe source yako ni ile movie?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…