Mr Chapchap
New Member
- Aug 15, 2022
- 1
- 0
Utangulizi:
Nchini Tanzania, Mtoto ni binadamu mwenye umri chini ya miaka 18, Ni tafsiri kutoka sheria ya watoto ya mwaka 2009, iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019, sehemu ya pili, kifungu cha nne, kifungu kidogo cha kwanza
Rejea: TLS – Online Legal Aid Repository
Kila mzazi/mlezi huwa nania njema kwa mtoto wake, hakuna mzazi mwenye kusudi la kukwamisha ndoto hai kwa mtoto wake, hupigana kufakupona ili mtoto afanikiwe.
Juhudi ambazo wazazi wamekuwa wakizichukua kwa lengo la kuwa kwamua watoto, zimekuwa na matokeo yasiyo tarajika kwa sababu uwasilishwaji wake huleta tofauti katika tafsiri.
Siri nyingi za mafanikio zina changamoto ya kutokugusa mzizi wenyewe, zinagusa vitu vya juu juu tu kama weka juhudi, jiamini na mengine.
Mzizi mkuu wa mafanikio ni mtazamo ambao mtu anakuwa nao kwenye uwezo wake
Kama mtazamo hautabadilika, haijalishi ni mambo gani ya nje anafanya, hataweza kufikia mafanikio
Watu wengi wamekuwa wanachanganya mtazamo wa ukuaji(growth mindset) na mtazamo chanya(positive mindset), hivi ni vitu viwili tofauti, mtazamo chanya ni jinsi unavyochukulia mambo na mtazamo wa ukuaji ni jinsi unavyochukulia uwezo wako na hatua(juhudi) unazochukua kutokana na vile unavyoamini
Mtazamo wa ukuaji ni kupiga hatua kutoka chini na kwenda juu zaidi na kushindwa ni hatua ya kufanikiwa, ni sehemu ya kujifunza na kufanya vizuri zaidi ili upate unachokitaka
Ndio maana mtazamo unanguvu ya kumjenga mtu au kumbomoa kwenye mafanikio
Mtoto anaweza kufikia mafanikio makubwa akijua nguvu yake ilipo, ambayo ni kwenye akili yake
Angalia mfano ufuatao;
Watoto waligawanywa kwenye makundi mawili,
Kundi la kwanza wakasifiwa kwa juhudi walizoweka na kundi la pili wakasifiwa kwa uwezo wao
Kisha wakapewa zoezi ambalo ni rahisi
Kundi la kwanza wakasifiwa kwamba wameweka juhudi kubwa na zimewasaidia kukamilisha zoezi hilo
Kundi la pili walisifiwa wana uwezo mkubwa ndiyo maana wameweza kukamilisha zoezi hilo
Baada ya hapo walipewa zoezi lingine ambalo ni gumu zaidi ya lile la kwanza na hapo matokeo yalikuwa tofauti
Wale waliosifiwa kwa juhudi waliona juhudi zao ndizo zinawapa matokeo hivyo walikuwa tayari kuendelea kuweka juhudi, huu ndiyo mtazamo wa ukuaji
Wale waliosifiwa kwa uwezo, waliona uwezo wao ndio umewapa matokeo hivyo kwenye zoezi gumu hawakujisumbua kwa sababu waliona hawana uwezo huo, huu ndiyo mtazamo mgando
Mtoto anaweza kufanya vizuri zaidi, kama mzazi ataondoa ukomo kwenye uwezo wake, hapo unakuwa umefungulia mlango wa mafanikio
Mfano huu unatupa funzo kwamba ufanikishaji huwa una athiriwa na mtazamo ambao mtu anao kwenye uwezo na juhudi
Hii inaelezea kwamba kwanini watoto wengi wanaoonekana wana uwezo mkubwa utotoni huwa hawafanikiwi wakati wale ambao wanaonekana hawana uwezo mkubwa wanafanikiwa
Tofauti kati ya mtazamo na fikra
Binadamu huwa tunazaliwa na akili amabazo ni tupu kabisa yaani hakuna chochote tunachokijua,
Kadhalika kwenye imani tunazokuwa nazo, hatukuzaliwa nazo, bali tumejifunza hapa duniani.
Kipindi cha utoto ndiyo kipindi ambacho huwa tunajenga imani tunazokuwa nazo, huwa tunawaamini wale waliotuzidi na kuona wapo sahihi hivyo yale wanayoamini na sisi pia ndiyo tunayoamini hata kama hayapo sahihi
Kwahiyo Imani huwa zinaleta fikra
Fikra na imani zinajengwa na mtazamo
Mtazamo ambao mtu anakuwa nao, unakubali imani na fikra hizi ndiyo uhalisia wa mtu, mtu anakubali na kujiona ndivyo alivyo kwa matokeo anayoyapata.
Mfano:
Inapotokea mtu ameshindwa, fikra zina mwambia kuna kitu hakipo sawa ila mtazamo unamwambia kuwa wewe ndio haupo sawa
Inapotokea mtu amefanikiwa fikra zinamwambia amefanya vizuri huku mtazamo ukimwambia yeye ni bora kuliko wengine
Mtazamo ambao mtu anakuwa nao uwe ni mgando au wa ukuaji unatokana na imani ambazo mtu umekuwa nazo kwa maisha yake tangu akiwa mdogo kulingana na ushahidi, taswira na mazingira yanayomzunguka
Njia ya kubadili mtazamo inayofanya kazi
Njia ya uhakika ya kubadilika ni kuweka mpango uliokamilika
Badala ya kusema kwamba kesho nitafanya sema utafanya nini na kwa wakati gani
Mfano:
Unapanga kuandika makala kwenye jukwaa la “stories of change” lakini una hairisha kila siku, weka mpango wa kuandika kwenye kijitabu
“Jumamosi asubuhi, baada ya kuamka nitakaa mahali kompyuta ilipo kwa saa moja na kuandika makala”
Kwa mabadiliko yoyote unayotaka kuyafanya weka mpango thabiti unaojibu maswali matano muhimu:
1. Nini unakwenda kufanya?
2. Wakati gani utafanya?
3. Wapi utafanyia kitu hicho?
4. Nani utafanya nae?
5. Kwa muda gani utafanya kitu hicho?
Tambua kwamba kubadili mtazamo hakutatui kila tatizo ulilonalo lakini itakupa uwezo wa kukabiliana na kila tatizo utakalo kutana nalo vile-vile kunakupa nafasi ya kuwa wewe halisi
Jinsi ya Kubadili mtazamo wa watoto
Picha kwa hisani ya mtandao:familia yenye furaha
Njia sahihi ya kufanya hivyo ni kuweka msisitizo kwenye kujifunza na kuongeza juhudi ili kupata matokeo bora
Mtoto wako anapokuja kwako kukueleza sifa zake jinsi alivyowazidi wengine,
Badala ya kumsifia kwa hilo muulize amejifunza nini katika hilo?
Anapoeleza jinsi ilivyorahisi kwake kufanya baadhi ya vitu, mtake ajaribu vitu vya juu zaidi ili ajifuze na kuongeza juhudi zaidi
Anapowasifia watu kwa uwezo wao, mwoneshe jinsi watu hao wanavyoweka juhudi na kujifunza
Mpe mtoto mazoezi yanayoongezeka ugumu kadiri anavyokwenda kisha angalia anachukuliaje anapokutana na ugumu
Je anakata tamaa au anakuwa tayari kuendelea?
Msaidie ajifunze kuweka juhudi kadri mazoezi yanavyokuwa magumu
Atakapoweza kuvuka magumu hayo atakuwa amejijengea mtazamo wa ukuaji kwamba anaweza kufanya zaidi ya alivyozoea
Unapowasifia watoto kwa uwezo wao, inaua kabisa hamasa na kuathiri ufanisi wao
Mtoto anapokuwa na mtazamo wa ukuaji anaondokana na kiburi na kuwa mnyenyekevu
Maoni
Mtazamo wa mtu upo kwenye fikra na hauonekani wazi kwa watoto na pia watoto wanajifunza zaidi kupitia matendo ya watu wazima na sio maneno yao.
Mzazi jifunze kumpa mtoto uhuru kuwa kile anachotaka kuwa, unachopaswa ni kimuunga mkono kwa vitendo na siyo kumlazimisha awe kama unavyotaka wewe
Makosa ambayo wazazi wengi hufanya:
Kila neno au hatua ambayo mzazi anaichukua, huwa inapeleka ujumbe kwa mtoto
Wazazi wengi wamekuwa wanahakikisha kila mtoto anasifiwa kwa uwezo/vipaji na sio juhudi hata pale anapopata matokeo ambayo sio sahihi, Hali hii imekuwa inawazuia watoto wasishindwe.
Kama mzazi hakikisha humkingii kifua mtoto afanyapo makosa
Muoneshe mtoto, kushindwa kwake sio kwa sababu ya uwezo wake bali juhudi alizoweka hazijatosha anapaswa kuongeza juhudi.
Hitimisho
Kwa mzazi/mlezi, zawadi unayoweza kuwapa watoto na ikawasaidia maishani mwao ni kuwajengea mtazamo wa ukuaji kwa kuwafanya wazipende changamoto badala ya kuzikimbia ili wawe tayari kujifunza, kwa kuweka juhudi na kupata matokeo mazuri.

Attachments
Upvote
0