Jinsi Mungu anavyopangua mawazo finyu ya wanadamu dhidi ya mpango wake kwa Chadema na Lissu

Jinsi Mungu anavyopangua mawazo finyu ya wanadamu dhidi ya mpango wake kwa Chadema na Lissu

Mpango mkuu wa wanadamu dhidi ya Chadema na Lissu, ni kuhakikisha chama anachokiongoza kinakuwa kwenye mgogoro mkali wa wao kwa wao ndani ya Chadema ili tu, mwenyekiti wake na timu yake yenye msimamo mathubuti na wasioiogopa haki, wasifanikiwe kwa chochote katika kuisaka haki ya wanyonge katika nchi hii ya wapenda amani

Lupia ya wapanga mipango hiyo ikapitishwa kwa wapenda mkate ili waanzishe genge (kundi) ndani ya chama litakalo kwenda kinyume na makubaliano yoyote ya chama na kuhakikisha kwamba, chama kina kuwa kwenye mgogoro usiotibika

Wapanga mipango hiyo, wanamjua fika mh Tundu Lissu, misimamo yake na kwamba, akishaamua jambo, harudi nyuma hata kama mbele yake kuna simba mla watu

Mungu alivyo fundi, Uchaguzi wa Chadema alihakikisha kwamba, timu inayoongoza mapambano, yote, mfano wake ni kama Danieli, Abedinego na meshack wa Biblia, watu hawa hawatishiki, hawaogopi na hawatishwi, wapo tayari kuifia haki bila wogàa, hayo ndiyo maajabu ya Mungu

Kinachodhihirisha hiki nikisemacho kwa wapanga mipango kwamba mkono wa Mungu upo juu ya Chadema, ni pale waliposahau kwamba, kuna kipengele cha kujaza fomu za maadili ya uchaguzi kwa kila chama

Laiti Chadema wangejaza hizi fomu, leo kungekuwa na mgogoro mkubwa wa ndani, kuna wale ambao wangeendelea na msimamo wa kutokufanyika uchaguzi, lakini lile kundi la waliopewa lupia, wao wangeendelea na mipango ya uchaguzi kama kawaida

Kana kwamba hiyo haitoshi, Mungu aliwanyima hata hayo macho ya kuona mbali, maana iliwapasa wakae kimya tu kwanza, wakati wa majira kufika ya uchaguzi, ilikuwa ndio wakati sahihi wa hawa wasaliti kuanzisha mgogoro

Mungu anamaajabu yake, hasa wakati na majira yake yanapowadia, ndio hujionyesha kwamba, yeye ndiyo yeye na hapana mwingine

Waliopewa lupia, walichanganyikiwa na wameendelea kuchaganyikiwa na wataendelea kuchanganyikiwa licha kwamba wamejiondoa Chadema

Kitendo cha kutokusaini Maadili ya uchaguzi, Kilitosha kabisa kuchiria kusudi la Mungu kwa uongozi wa Tumdu Lissu na Chadema kwa ujumla

Ni dhahili ukombozi umewadia, Tanzania huru ni sasa

Yeyote aliyeko Chadema, amekusudiwa kuwa sehemu ya ukombozi kwa watanzania wanyonge

Na ole wa mwadamu ashupazaye shingo juu ya hili, shoka la Bwana wa majeshi lipo kwenye shina tayari kufyeka na kuangamiza

Mh Lissu, mahali ulipo, unatimiza tu kusudi la Mungu katika nchi hii, mikono yako ni misafi na kila mtu anajua hivyo, ila tu kiburi cha uzima cha wapenda madaraka

Mungu uirehemu Tanzania na uwalinde wote wenye haki wako katika nchi yetu

Mungu ibariki Tanzania na uibariki Chadema
Lissu ni mpakwa mafuta wa Mungu. Hakuna hila mbaya dhidi yake itakayofanikiwa.
 
Back
Top Bottom