Jinsi navyoteseka moyoni. Nahitaji faraja yenu ndugu zanguni

Bill Lugano

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
1,189
Reaction score
6,450
Nipo tu hapa nasikiliza Music wa Taratibu huku nikicheck News mwenye Screen yangu ya inch 72. Nmekuwa Mnyonge maana weekend hii jumamosi nlipaswa niwe na family Dubai.imekuwa kinyume. Mzee na mama wapo Canada nami nmekwama hapa TZ.

Mzee alinipigia simu juzi akisikitika sana kuwa this birthday yake hatutakuwa kama family.tulizoea wote tunakusanyika kama ni UK,Sweden,Canada,USA au South Africa kusheherekea siku ya kuzaliwa ya mzee au mama.

Nimeamua tu niwaalike ndugu zangu humu JF.Mwaka huu theme ya mavazi ni Suit ya kijivu,shari jeupe,kiatu cha brown na mkanda kitambaa cha mkononi cheupe na soksi nyeusi kwa wanaume.

Wanawake kasoro soksi na mkanda but hivyo hivyo. Nimeshaweka order pale woolworths. Nahitaji members wa kiume 6 na wakike then nafasi nyingine nawaachia jamaa zangu.

Hizo nguo ndo card yenyewe.so usijali kuhusu mwaliko ila pia uje na nguo za kuogelea.tutaanza jumamosi mpaka jumapili jioni kama mtu atakuwa ready.

Nahitaji kuunda kamati ndogo kwa ajili ya siku hiyo. Tunahitaji mbuzi wawili.nmeambiwa mbuzi mmoja ni tsh 250,000 jumla nmetenga tsh 500,000 na usafiri tsh 100,000 kuleta Oysterbay.so awepo mtu wa kushughulikia hili.mimi sijui pa kuwapata.

Wachomaji mbuzi wawe wa 4 kila mmoja ntamlipa tsh 250,000. Chakula nimewaambia watu flani wa catering wataleta na wahudumu pia.

Ntafurahi maana mtaweza kuiona familia yangu kupitia SKYPE hasa yule mdogo wangu mtukutu mbaye alilia sana siku ya kwanza kuja TZ.

Juzi ananiuliza huko Tanzania na hii Corona si mtakuwa mmebaki wachache sana.nlicheka mpaka machozi yalitoka.yeye anaamini huku watu watakuwa wanadondoka tu mitaani kama kuku wa mdondo sababu ya Corona.

Nmemwambia huku corona si issue sababu watu wa huku washaumwa sana corona wakiwa hawajui na wakapona wenyewe.

Wadau mkija msisahau pia masweta maana ndani kwangu kuna baridi sana.napenda baridi na ndo maana nina high capacity AC zile za kwenye dari.

Atakuwepo daktari kupima kwanza wagonjwa kabla hawajaaingia ndani ili tusiambukizane Corona.mi ntakuwa wa kwanza kupimwa.

Karibuni wadau msisahau nguo za kuogelea maana nina swimming pool hapo home linaweza accomodate watu 70.

Kama utakuwa tayari nifuate inbox nikuelekeze hilo duka la nguo pale posta na pia suala la usafiri usipate shida kama huna gari kuna dereva atakuwa anawachukua watu makwao kuwaleta na kuwarudisha.

Njooni pia ili familia yangu waone nina marafiki wengi TZ maana wao huwa wanaamini mimi si mwepesi kupata marafiki kama last born wetu yeye ulaya nzima na marekani ana marafiki mpaka utashangaa.

Ntafurahi mkiifahamu familia yangu na muone maisha wanayoishi.siyo mimi naishi huku kwa shida.naomba unapokuja zingatia kuja na boyfriend au girlfriend wako.huku hakuna kudandia wa mtu.pia uhakikishe nguo inakukaa vizuri.maana usije ukatokea kama sanamu imevalishwa nguo.

Wadada muwe warembo please.na usisahau the main communication language will be english.so you should be fluent in english.if you dont have fluency in english please dont bother coming.

Hata hao wachomaji mbuzi nmehangaika sana kuwapata maana nlikuwa nawa interview in english kwanza.naamini kwa kampani yenu ntafarijika na kujisikia kma nipo home na family.

Pamoja na Corona maisha yanaendelea tu.
 
Utakula mkuu siyo issue kubwa sana. Chakula kitakuwepo cha kutosha. Hii catering nliyowakodi ndo huwa wanaandaa dhifa za kimataifa pale Ikulu.wapo fresh sana.mimi wamenifanyia plate moja tsh 130,000 sababu jamaa anayeimiliki nliwai msaidia one time alikuja USA akapungukiwa pesa za matumizi so nlimpa kiasi flani.amekuwa kama ndugu though amenizidi sana umri.alitaka anifanyie bure nlimwambia hapana kama hela ninazo nitumie tu why nifanye ubahili?

hahahaha..kidukulilo njaaa kali
 
Boss wangu kidukulilo nipe mimi tenda ya kutafuta hao mbuzi ila hata hivyo mbona bajeti ya mbuzi ni kidogo sana yaani laki 5 tu kwa jinsi ninavyo kufahamu wewe boss wangu ungefanya hata MILIONI 2 bajeti ya kwenye mbuzi....ila usinisahau kwenye tenda ya kutafuta mbuzi.
 
Juzi ananiuliza huko Tanzania na hii Corona si mtakuwa mmebaki wachache sana.nlicheka mpaka machozi yalitoka.yeye anaamini huku watu watakuwa wanadondoka tu mitaani kama kuku wa mdondo sababu ya Corona.

Nmemwambia huku corona si issue sababu watu wa huku washaumwa sana corona wakiwa hawajui na wakapona wenyewe.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata tenda ya kutafuta mbuzi, You should be fluent in English mzee [emoji16][emoji23][emoji23][emoji16][emoji16]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…