Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hujalazimishwa kusoma, kuna nyuzi nyingi tu hapa jf.We jamaa ni hopeless sana.
Umeandika kidogo tu unasema umechoka sa si bora usingeweka uzi wako huu
mtu chake zitto junior JokaKuu Moronight walker wa kupuliza pitieni hapa tafadhali...Naitafsiri kidogo Ile posting ya JF ya Jager Master ya Sec, 2011.
Hii makala ya 2001, imeandikwa na kachero Wayne Madsen. Anasema Marekani Wana kambi Cyangugu, Rwanda karibu na mpaka wa Congo.
Wizara ya Ulinzi ya Marekani mara nyingi inaàjiri PMC (private military contractors) ambao zamani walikuwa wanaitwa 'mamluki'. Haya mambo yameandikwa 2001.
Hawa Marais waliopo madarakani sasa hivi Uganda, Rwanda, Ethiopia, Angola, Eritrea na DRC wanaongoza nchi nchi zenye vurugu kubwa za kikabila na kisiasa ambazo zinawezesha kampuni za madini za kimataifa kupeana mali za Afrika.
Hizi kampuni nyingine zinashirikiana na PMC zilizotajwa hapo juu. Kwa mfano, American Mineral Fields Inc,ambayo ilishiriki sana katika kumuweka hayati Laurent- Desire Kabila madarakani. Kampuni hiyo inamilikiwa kwa kiasi kikubwa na washirika wa Bill Clinton.
Pia, lengo moja kubwa la RCD, Warwanda wanaopigana Congo dhidi ya Kasbila ni kuwasaidia Barrick Gold kupata madini.
Sasa hivi,Barrick na makumi ya makampuni ya madini yanachochea mgogoro wa Congo.
Vurugu za sasa, Afrika ya Kati zinasababishwa kwa kiasi kikubwa na tukio la Aprili 6,1994, liliporushwa kombora kwa ndege iliyokuwa imembeba Rais wa Rwanda, Mhutu,Juvenal Habyarimana,na mwenzake, Rais wa Burundi, Cyprien Ntaryamira.
Oh, I am dead tired. Nitaendelea kesho. Inatoa ushahidi mwingi, kuliko unaohitajika kuonyesha Kagame kaitungua ile ndege. Pia unasema hawa watu ndio waliomuua Director wa TISS.. Labda, hakuna haha ya kuendelea(kesho). Yaliyoandikwa yanatosha.
hahahahaha.atapatikana tu muhusika mkuu.iko siku.nasubiri muendelezo wa hii madamtu chake zitto junior JokaKuu Moronight walker wa kupuliza pitieni hapa tafadhali...
Mzimu wa mwaka 1994 huko Rwanda bado unasumbua tu maziwa makuu mpaka kesho na umegoma kutoweka.
Punguza shobo utajazwa mimba.Hujalazimishwa kusoma, kuna nyuzi nyingi tu hapa jf.
Hao waliouawa huko Zaire hawakufika hiyo idadi ?Kwa hiyo wakaona ni bora wamshirikishe,the man from Edinburgh,no doubt kwa sababu walikuwa wanataka kuzuia watu wengine 800,000 wasiuawe.
Ndege imetunguliwa 1994,taarifa kuelezea tukio ya mwaka 1988Uuuwiiiiiiiii kambaaaaaa!!!
Wakati wa utawala wa le marchel kuku ndbegu wa zabanga ilikua shwareee hata ukimwambia mtu naenda Zaire unajisikia rahaaaCongo lini ilikuwa na amani? Tangu ile nchi ipate uhuru ina vurugu.
Kagame na congo ugomvi wao upo hapa na wacongo wamesha mchokaNaitafsiri kidogo Ile posting ya JF ya Jager Master ya Dec, 2011.
Hii makala ya 2001, imeandikwa na kachero Wayne Madsen. Anasema Marekani Wana kambi Cyangugu, Rwanda karibu na mpaka wa Congo.
Wizara ya Ulinzi ya Marekani mara nyingi inaàjiri PMC (private military contractors) ambao zamani walikuwa wanaitwa 'mamluki'. Haya mambo yameandikwa 2001.
Hawa Marais waliopo madarakani sasa hivi Uganda, Rwanda, Ethiopia, Angola, Eritrea na DRC wanaongoza nchi nchi zenye vurugu kubwa za kikabila na kisiasa ambazo zinawezesha kampuni za madini za kimataifa kupeana mali za Afrika.
Hizi kampuni nyingine zinashirikiana na PMC zilizotajwa hapo juu. Kwa mfano, American Mineral Fields Inc,ambayo ilishiriki sana katika kumuweka hayati Laurent- Desire Kabila madarakani. Kampuni hiyo inamilikiwa kwa kiasi kikubwa na washirika wa Bill Clinton.
Pia, lengo moja kubwa la RCD, Warwanda wanaopigana Congo dhidi ya Kasbila ni kuwasaidia Barrick Gold kupata madini.
Sasa hivi,Barrick na makumi ya makampuni ya madini yanachochea mgogoro wa Congo.
Vurugu za sasa, Afrika ya Kati zinasababishwa kwa kiasi kikubwa na tukio la Aprili 6,1994, liliporushwa kombora kwa ndege iliyokuwa imembeba Rais wa Rwanda, Mhutu,Juvenal Habyarimana,na mwenzake, Rais wa Burundi, Cyprien Ntaryamira.
Oh, I am dead tired. Nitaendelea kesho. Inatoa ushahidi mwingi, kuliko unaohitajika kuonyesha Kagame kaitungua ile ndege. Pia unasema hawa watu ndio waliomuua Director wa TISS.. Labda, hakuna haha ya kuendelea(kesho). Yaliyoandikwa yanatosha.
Huyu jamaa hata motoni hato kaaBaada ya hii ndege kutunguliwa, Serikali ya Rwanda ikaanzisha yale mauaji ya halaiki ambapo watu 800,000 waliuawa. Baadaye RPF wakalipiza kisasi kwa kuua Wahutu 500,000,wengi wao wakiwa wakimbizi waliokuwa Zaire.
Watu walioutungungua Ile ndege mpaka leo hawajulikani ni kina nani,na hawajafikishwa mahakamani.
Umoja wa Mataifa ukifanya uchunguzi ukashindwa kuwapata. OAU ilifanya uchunguzi ikashindwa kuwabaini.
Mwaka 1988,Jaji wa zamani wa Ufaransa ,Jean-Louis Bruguire,alichunguza kushambuliwa kwa Ile ndege. Baada ya kuzungumza na mashahidi Switzerland,Rwanda, Tanzania,na Russia,Bruguire inaelekea ana ushahidi wa kutosha kuamuru hati ya kimataifa itolewe kumkamata Kagame.
Jaji mwingine mstaafu wa Ufaransa, Thiery Jean-Piere,ambaye sàsa ni Mbunge wa Bunge la Ulaya,katika uchunguzi mwingine kabisa wa kibinafsi alifikia uamuzi kwamba Kagame alikuwa nyuma ya shambulizi Hilo.
Wakati shambulizi hilo lilipotokea,RPF ilikuwa inasaidiwa na Marekani na Uganda.
Kabla ya shambulizi, miezi mitatu kabla ya shambulizi Jenerali Kagame alikuwa Fort Leavenworth, Kansas, kwenye General Staff College akipata mafunzo ya kijeshi,pamoja na mafunzo ya SAM( Surface to Air Missiles),katika kambi ya Air Force ya Barry Goldwater, Arizona.
Duh!Katika kutoa ushahidi mbele ya Kamati ya uchunguzi ya Ufaransa ( kumbuka Ile ndege ilikuwa inaendeshwa na rubani Wafaransa), Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Ufaransa,Bernard Debre alisisitiza kwamba makombora maeili ya SAM-16 yaliyotumika katika hilo shambulizi yalikuwa yametokea katika Jeshi la Uganda, ambayo probably walipewa na Marekani kutoka katika Vita ya Ghuba.
Aliungwa mkono na wakuu wawili wastaafu wa idara ya ujasusi ya Ufaransa (DFSE) Jacques Dewatre na Claude Silberzahn.
Waziri wa Ulinzi wa Habyarimana, James Gasana, aliyekuwa Waziri wa Ulinzi kuanzia April 1992 mpaka July 1993 alisema hawakuona sababu ya kupoteza fedha kununua SAM,kwa sababu RPF walikuwa hawana ndege. Kwa hiyo siyo sahihi kusema Wahutu waliitungua Ile ndege.
Haya maelezo ya hawa officials wa serikali ya Ufaransa DFSE yanaungwa mkono na majasusi wa zamani wa RPF ambao walitoa ushuhuda kwa U. N.
Hawa wanasema ndege ilitunguliwa na kikosi cha watu kumi cha RPF. Hizi ripoti alipewa Mkuu wa ule uchunguzi, Jaji Louise Arbor wa Canada ambaye hakuufanyia kazi,hasa alipoona Rwanda wanashutumiwa.
M7 naye mshenzi ndio maana wanatunishiana vifua tu na kutumiana EBOLAMichael Hourigan,mwanasheria wa Australia anasema,"Sisi tulikuwa UNO tunashughulika na hili swala, lakini wakubwa wetu kule walikuwa wanatukwamisha.
Baada ya hao majasusi watatu wa RPF kutoa hizo habari,waliungwa mkono na jasusi mwingine wa zamani wa RPF, Jean-Piere Mugabe. Mugabe alisema mauaji na lile kombora yaliongozwa na Kagame na 2i/c wake James Kabarebe.
Jasusi mwingine wa RPF,Christophe Hakizebara,aliwaambia UNO kwamba "taifa la kigeni" lililoisaidia RPF lilikuwa Uganda. Hakizabera alisema mkutano wa kwanza na wa pili wa kufanya mipango ilifanyika Uganda katika miji ya Kabale na Mbarara,wa tatu ulifanyika Machi 2994,Bobo-Dioulassi,Burkina Faso,ambapo Kagame alihudhuria.
Kama kawaida yake,UNI ilipuuzia ushahidi huu uliotolewa.
Uchunguzi wangu,ambao nimefanya kwa miaka minne,unaonyesha haya makombora yalitekwa na Marekani katika Vita ya Desert Storm na yakaletwa na CIA kupitia Cairo,Misri. Uganda ikaweka baadhi, mengine ikawapa SPLA na RPF.