The patriotic
Member
- Aug 7, 2021
- 25
- 22
Habari wanajamiiforum, Namshukuru Mungu na natanguliza shukrani za dhati kwenu nyote maisha yangu yanaweza kuwa funzo kwenu vijana mliokosa ajira baada ya kumaliza Chuo.
Mimi ni kijana niliomaliza shahada ya ualimu mwaka 2019 ambapo baada ya kumaliza Chuo na kusubiri ajira takribani mwaka mmoja nikaona mbinu pekee inayoweza kunisaidia ni kujiajiri kutokana na changamoto ya ajira Tanzania ambapo miaka inavyozidi kwenda wasomi wanakuwa wengi na shida kubwa ya ajira nayo inazidi kuota mizizi
Hata ajira zinazotolewa bado hazikizi mahijati ya wahitimu wa elimu ya vyuo nchini Tanzania kwa sasa kwa hiyo
Nikafanya tathmini nikagundua kwamba mtu yeyote duniani ili afanikiwe kimaisha lazima awe kwenye vipengele vifuatavyo;
.Kuajiriwa
. Kilimo
.Biashara
. Vyote kwa pamoja au viwili nakadharika
NIKAANZA KUJIAJIRI KATIKA KILIMO
Binafsi natokea nyanda za juu kusini mwa Tanzania ambapo nakafanya tathmini nilime mazao ya mda mfupi na ya mda mrefu na ya mda mfupi
Kwa Kanda ya kusini nililima viazi mviringo ambavyo hela niliyopata mwaka 2020 baada ya kuvuna maisha nashukuru Mungu yalianza kubadilika na nikatoka kuwa tegemezi na kuanza kujitegemea katika mazingira ninayoishi hela niliyopata nikafanikiwa kununua mche ya parachichi na kuanzisha shamba la parachichi ambapo Hadi Sasa nashukuru Mungu Miche inaendelea vizuri
Sasa maisha yangu kwa kiasi kikubwa sio tegemezi kwa maana kadri siku zinavyozidi kwenda naanza kuona ahueni na maisha yanazidi kubadilika
Mwaka huu tayari nimeshaanza maandalizi ya shambani langu ambapo nategemea mwakani Mungu akipenda nipande Miche ya Macadamia, parachichi na pia mazao ya mda mfupi Kama viazi mviringo na mahindi ya kumwagilia
Mfano parachichi uhitaji wake ni mkubwa katika soko lá África hususa ni nchi za Morocco,South Africa
Ulaya pia nchi za Hispânia ,ufaransa,Uingereza na Italy
Na nchi za mashariki ya kati
Pia Macadâmia (karanga pori ) no mazao ambayo uhitaji wake kwa Sasa sokoni ni mkubwa ambapo unga wake ni dawa kwa magonjwa mengi kwa hiyo vijana ili tujikomboe katika uchumi lazima tujihusishe katika kilimo hususu mazao yanayoweza kutoa malighafi za viwandani ambapo tutakuwa tumepiga hatua kwenye maendeleo ya kiuchumi na kutokuwa tegemezi kwa serikali
BAADHI YA FURSA ZA KILIMO TANZANIA ZINAZOWEZA KUWAKOMBOA VIJANA NA KUJIAJIRI
Kilimo chá misitu, vijana tukijiwekeza kwenye misitu ni lahisi kuweza Kujiajiri kwa maana naamini vijana wengi wasomi tunatoka vijijini ambapo ardhi ya Babu zetu haitumiki na haina matumizi yeyote kwa hiyo vijana nashauri tuache kukaa mijini na kusubiri ajira kwa sababu njia pekee inayoweza kututoa katika umaskini ni kijiajiri katika kilimo chá misitu hususa kwa ajiri ya mbao na mikoa ambayo misitu inakubali Tanzania ni mingi mno
Kilimo chá nyuki (ufugaji) ufugaji wa nyuki hauhitaji gharama kubwa zaidi ya kununua mizinga na kuweka porini na asali ni zao ambalo haliwezi kuharibika kwa mda mfupi na thamani yake no kubwa pia tunaweza kuongeza thamani kwa kutengeneza bidhaa mbalimbali zitokanazo na asali
Kilimo Cha matunda ,matunda ya mda mrefu Kama vile passion na parachichi yanaweza kutatua tatizo la ajira nchini kwa sababu uhitaji wake katika soko la dunia ni mkubwa na unatalajia kuongezeka kutokana na Covid 19
N.B ni moja tá zao ninalojihusisha nalo n
Kilimo chá viungo,Kuna viungo vingi ambavyo katika soko la dunia vinafanya vizuri hususa ulaya na nchi za mashariki ya Kati mfano karanga pori(macadamia,)
Serikali ifanye yafuatayo ili kuwezesha vijana Kujiajiri hususa ni katika kilimo
Serikali iweke punguzo ,ruzuku au iweke malipo kwa asilimia fulani kwenye pembejeo, serikali iweke bei punguzo kwenye pembejeo hususa ni viwatilifu,mboleo na vifaa vya umwagiliaji kwa vijana kufanya hivyo kutarahisisha vijana wengi kupenda kilimo
Ianzishe benki ya maendeleo kwa vijana,serikali ianzishe benki ya maendeleo itakayohusisha vijana ambapo itoe mikopo ya riba ndogo na ihamasishe vijana Kujiajiri katika kilimo chá mazao ya biashara kwa sababu kilimo kikikua vijana wengi wataingia katika mnyororo wa thamani mfano wajasiriamali wadogo kupitia viwanda vidogo vidogo
Serikali ianzishe televisheni itakayohusisha kilimo na maendeleo,nchi Kama Kenya zimeendelea kiuchumi kwa sababu Wana runinga ya taifa mahususi katika kutoa elimu juu ya mazao yanayolimwa Kenya ndio maana hata wanunuzi wengi wa mazao yanayolimwa Tanzania ni kenya
Serikali itafute masoko pamoja na kuangalia vigezo vya kuuza bidhaa,serikali itafute masoko ya mazao yanayolimwa hususa ni ya biashara mfano iwe na wataalamu wa masoko watakaozunguka nchi mbalimbali kutafuta masoko pamoja na kujua vigezo vya masoko(Global gap standard world wide)
Serikali ianzishe shirika la ubora wa mbegu na mazao na iweke vituo Kila mkoa,ubora wa mazao ndo unafanya mazao yakubalike sokoni au la mfono Kenya Wana(KEPHIS) pia Wana Avocado society of Kenya inayoshughulikia suala la viwango hususa ni kwa mazao ya parachichi
Mtaala wa elimu ufundishe vijana Kujiajiri kilingana na mazingira yaliyopo, mfano vijana wafundishwe namna ya kuzitambua fursa hususa ni za kilimo kulingana na mikoa wanayoishi mfano Dar es salaam kijana anaweza akawa anaagiza na kusafirisha nafaka kutoka mikoani na kuzipeleka mjini namaanisha mtu wa Kati
Jinsi shindano la JamiiForums linavyoweza kubadilisha maisha yangu kupitia vijana
Binafsi Kuna maeneo Kama ekari 100 ya familia yanayonizunguka ambayo ambayo yanaweza kutumika kwa shughuli ya kilimo hususa ni matunda na viungo mbalimbali ambayo yapo kwenye mkakati ambapo yakitumika vizuri na kuleta mafanikio vijana watanufaika kupitia mnyororo wa thamani ufuatao;
Wazalishaji, hawa ni watu ambao kazi kubwa itakuwa ni kuhakikisha mazao yanatunzwa vizuri mashamba ambapo kupitia sekta hiii tatizo lá ajira litakuwa limepunguzwa kwa kiasi kikubwa
Watu wa Kati(middlemen) Hawa ni vijana ambao kazi yao kubwa ni kutoa mazao shambani na kupeleka kwenye soko kwa ajili ya mauzo kwa hiyo kupitia mnyororo huo vijana tatizo la ajira itakuwa imepungua kwa kiasi kikubwa katika jamii inayotuzunguka
Wauzaji,hapa ni wajasiriamali wadogo ambao kazi kubwa ni kuuza matunda na bidhaa zitokanazo na matunda kwa kufanya hivyo suala lá Ukosefu wa ajira linaweza kuwa história kwa Tanzânia hususa ni kwa vijana
Ushauri kwa vijana waliokosa ajira na wapo mtaaani;
Tumuombe Mungu katika kazi za mikono yetu
Tuondoe aibu tujichanganye mtaani, vijana wengi mtaani ambao hawajasoma Wana vitu vingi na fursa nyingi kwa hiyo tukiambatana não ni rahisi kuzijua fursa zinazopatikana katika maeneo tuliyopo
Tutumie vizuri ardhi vijijini,baada ya kukesha kwenye kumbi za starehe na kukaa vijiweni tutumie vizuri ardhi kwa ajiri ya kilimo hususa ni mazao ya kibiashara
Tufanye utafiti juu ya mazao yanayoweza kutoa malighafi yanayohitajika sokoni hususa ni Tanzania Bara lá afrika ,ulaya na Ásia
Tutumie wataalamu wa kilimo kwa ushauri,tuache kilimo cha mazoeza na tujikite katika sayansi ya kilimo ili kuwa na kilimo chenye tija na kubadilisha maisha yetu
Tufanye utafiti juu ya masoko na taarifa sahihi kabla ya kuingia shambani,ili kuwa na kilimo chenye tija ni vizuri kujiridhisha juu ya masoko hususa ni kwa mazao tunayolima ili kukwepa hasara(risk)
N:B Suala la ajira kwa Sasa ni jambo ambalo litaongezeka kwa sababu kila mwaka wahitimu wanazidi kuwa wengi kwa takwimu za serikali.
Mwisho:
Vijana baada ya kulia na uhaba wa ajira tujikite katika shughuli zingine zinazoweza kutupa mafanikio katika maisha
KURA YAKO MUHIMU
Asante sana

Upvote
18