Mkuu
ONTARIO embu turudi katika uhalisia wa kipindi hiki cha magufuli...
Mtu ni graduate amemaliza chuo mwaka jana...hana kazi yupo kitaa amepigika! Je ni vipi atapata hiyo pesa ya kuanza buzines??
Na kwa ugumu wa biashara na maisha katika era hii ya huyu mjamaa ni vipi graduate anachomoka? Ukizingatia biashara zinafungwa kila siku...mzunguko wa pesa mdogo!! Tuanzie hapa mkuu!!
Kivipi graduate atapata pesa::
Kwanza niwe muwazi bila kepepesa maneno - mtu anatafuta mkopo kufungua biashara ni popoma (moron). ●Hakuna mtu atakayeweza kukupa pesa ufanye biashara ambayo haijaprove success, biashara inayokopesheka ni ile ambayo tyr ina run na daily/monthly financials zina make sense.
●Biashara yoyote ina uncertainties nyingi sana, 90% ya biashara zinazoanzishwa hufa mwaka wa kwanza, ukichukua mkopo maana unajimaliza mara 2, kwanza kuhakikisha biashara haifi na pili kuhakikisha unalipa mkopo wa watu bila kuuwa biashara.
Njia pekee ya kuwa na mtaji ni personal savings, kama ulikua unakunywa supu chapati 2 na maji kwa 3000 anza kugonga mihogo na kandoro kwa jero (mfn tu). Fanya chochote kikuingiziacho kipato - jiulize watu wanatoka kigoma, mtwara wanakuja kwa magari ya mkaa still wakikaa Dar kwa miezi mi2 wanaeza kuafford chumba, chakula nk. Kuna dogo nilikua naongea nae yeye anauza hizi kahawa na kashata, alinambia kwa siku analala na buk 7.
Ugumu wa biashara::
Sijui unaishi wapi!! Mimi hua nakuwa Dar weekends nyingi, mara kadha hua nazunguka jioni maeneo ya Tabata. Kule kuna Bars nyingi sana kama KP, The great nk. Amsha amsha ni hatari, watu wanagonga mivinyo mpaka asubui, watu wanachoma pesa, mtu wa kawaida kuacha laki 2 pale ni kawaida. Bado unasema hakuna pesa?? Pesa ni ngumu labda kwako. Wanaofunga biashara nahisi ni wale ambao walikua wanatumia njia za uchochoro. Niambie yale maduka ya hardware pale Mwenge mangapi yamefungwa?? Niambie wapi madaladala yamepaki kua hakuna abiria?? Niambie yale maduka ya mbao pale buguruni kama yamefungwa?? Niambie duka gani pale mcity limeacha space wazi!! Umeona juzi diamond kaitwa ufunguzi wa duka gani sijui pale mcity!!
Nisiwe theorist sana - juzi nimeuza mahindi kutoka heka kadhaa nilizolima. Niambie watu wataacha kula