Boss, hiyo article ya mwananchi ambayo walitranslate kutoka article ya gazeti la The citizen iliniletea usumbufu mkubwa sana sana. Yani hawa journalists wa Bongo niliwavua vyeo wote na kuwadharau.
Kabla gazeti halijatoka niliwaambia kuna vitu wasiviandike kabisa, lkn hivyo vitu ndio walivitumia kama headlines. Yani acha tu, ningekua najua sheria au ht kujuana na Tundu Lissu tungekimbizana mahakamani.
Nashukuru sana pia kwa complements zako, kuna kipindi nilikua natamani nitumie kipaji changu cha uandishi kupiga pesa, lkn nikaona huko pesa hakuna, but ipo siku nitaandika kitabu kuhusu maisha yangu, nasubiri tu nifike level fulani ambayo sitahitaji kujiintroduce ili watu wanitambue.
... Kuhusu Forex, kaka nina dreams kubwa, ngoja niseme KUBWAA sana in capital letters ili kutia msisitizo. Na nataka kuuleta huu mgodi Bongo, afe simba afe mmasaai nitapambana na mamlaka mpk kieleweke. Nchi nyingi sana za Afrika wananchi wake wamefichwa kuhusu siri nzito ya utajiri uliopo kwenye hii biashara. Hakuna serikali wala financial institutions itakayotaka mwananchi ajue kutrade maana watu wakipata uelewa kuhusu hii kitu hakuna mtu ataingiza pesa zake fixed account, hakuna mtu ataingiza pesa zake kwenye DSE nk nk.
But all in all tutafika tu. Kama wenzetu Afrika kusini waliweza kwanini na sisi tusiweze. Nikiweka kila kitu sawa kuhusu paper works na mikataba fulani fulani then nitarudi kuanzisha uzi kuhusu hiyo kitu. Inabidi huu 'umasikini' tupambane nao kwa akili sana, tuubane mpk kwenye kona ya nyumba, tuupe kichapo aina ya 'kifo cha mende'.