Jinsi nilivyokaa siku 100 bila kuangalia saa

Napata picha unajiamkia tu asubuhi hujui ni saa ngapi hujui kama umechelewa kuamka ili ujue utajiandaa kwa muda gani,kituo cha kazi reporting time ni 08:30 asubuhi wewe uingie pale saa 09:40.

Yaani huyu jamaa sijamuelewa kabisa huyu.
ni ngumu sana kuelewa unaishije bila kuangalia muda,wazungu wanakuambia time is money 😂
 
Napata picha unajiamkia tu asubuhi hujui ni saa ngapi hujui kama umechelewa kuamka ili ujue utajiandaa kwa muda gani,kituo cha kazi reporting time ni 08:30 asubuhi wewe uingie pale saa 09:40.

Yaani huyu jamaa sijamuelewa kabisa huyu.

Atakua jobless huyu kijana
 
Swala Hapo Si Saa,,Swala Hapo Ni Muda...
###MudaHauitajiSaa###
###SaaNdioInahitajiMuda###
​
 
Mkuu ulijitahidi sana kwa mazingira ya sasa. Ila nikuambie... miaka wala siyo mingi sana iliyopita, hayo ndiyo yalikuwa maisha ya vijiji vingi Tanzania. Kuna watu wengi walikuwa wanaenda shambani, shule nk kwa kutumia majogoo, ndege, vivuli vya nyumba na hisia nyingine. Siyo ngumu kivile kama mtoto wa sasa wa Gen Z. anavyodhani.
 
Ila wengi ndivyo mumemsema kwa kutaka iwe kivyenu basi ndivyo mlivyo..

Badalahata ya kuuliza ilikuwaje? Kuna vitu aliona anakosa au kukosea kwa kutokujua muda... Ila, mjisikitikie

Kuna, jambo moja
Je, hajawahi kuamka, muda, fulani kimazoea hata iweje mtashtuka tu haswa kuamkia asubuhi? Na, ukiangalia saa muda ule ule mfano ndani ya -/+10mins
 
kuna watu hawaamini, hawa wana "trust issues" jaribu oekeyako hata wiki moja na utagundua inawezekana. mwili wenyewe una saa, binadamu tumeishi miaka mingi bila saa saa imekuja juzi tu, kuku na dege wanaamka asubui muda uleule bila saa, jogoo anawika sa tisa sa 12 etc, hakosei na hatumii saa, hata ukichunga n'gombe muda wao wa kurudi nyumbani hawakosei.

na binadamu tupo hivyo ststem nzima ilishakwepo tayari na ina ji update, ndo maana kuna muda unasikia usingizi hata ujizuie unalala, kuna muda usingizi unakata, kunamuda unasikia njaa

na matendo mengine yote yanaweza kuingia kwenye mfumo wa mwili ndani ya siku chache tu
 
Kwa nn ulirudi Tena kuangalia saa?
nilirudi kwasababu naishi kwenye dunia ambayo huo ndo utaratibu uliopo

ngoja nikuulize pia.. kwanini unafunga kipindi cha mfungo alafu baadae unaendelea na mambo yako ya kawaida ? hatakama wewe ukisema haufanyi hivo mbona wengi wanafanya na unaona ni sawa ?
 
Mada yako ni nzuri na inafikirisha , kiukweli tunaishi kwenye ulimwengu wa matrix, ukiweza kujitoa hapo maisha yako yanakua na uhuru wa asili sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…