Jinsi nilivyokamata laptop yangu(31-Dec-2012) iliyoibiwa November

Jinsi nilivyokamata laptop yangu(31-Dec-2012) iliyoibiwa November

Ndo uzuri wa miji midogo......saridalama huwezi kuipata......kwanza adapter ataenda kuiulizia kwenye maduka ya wahindi...ambayo idadi yake ni kama laki hivi....
 
My story is simple, kama movies za van damme za kipindi kile..

Mwezi wa kumi na moja nikiwa chuoni laptop yangu iliibiwa tukiwa hostel. Kwa ujumla ziliibiwa laptop mbili, modem mbili na simu moja. Ilikuwa ngumu sana kupata hata mahali pa kuanzia kwa sababu room mates(4) wote hawakuwepo chumbani kwa muda kama masaa mawili wakati wa tukio. Mengi yalitokea hapo katikati hata kiasi cha kumpeleka moja kati ya tuliowahisi Polisi.

Toka laptop imeibiwa nilikaa kama wiki mbili nikaanza kujipanga kununua nyingine ila niliona nifanye juhudi ya mwisho kuipata, Nilianzia hapa: Laptop iliibiwa bila adapter kwa hiyo nilifikiri nikaona kuwa lazima huyu jamaa ataanza kutafuta adapter. Nilizunguka kwa mafundi wanaorekebisha computer mjini(ambao ninajuana nao) nikawapa maelekezo kuwa ukiona mtu anaulizia adapter ya laptop(model na specifications nikawaelekeza).

Zilipita kama wiki mbili nikaelekezwa kuwa kuna mtu anatafuta adapter ya laptop(inayofanania na yangu) maeneo ya karibu na stand Arusha. Nilifika hapo huyo mtu alipoipelika but damn!! i was late. Saa kumi jioni ya 31-Dec nikiwa Moshi nilipigiwa simu, nilifika Arusha kwa mwendo wa Fastjet!! Fundi tayari alikuwa na laptop yangu. Niliwashtua Mabaunsa kadhaa tukafika pale mimi nikiwa kama anayeuza adapter, Kwa kifupi dogo hakuwa na cha kubisha kwa sababu computer kuwasha tu ilidisplay picha yangu basi tukaichukua kwa dogo akatupeleka kwa aliyempa na aliyempa alipewa na mwizi mwenyewe. Kila kitu tumerudishiwa ila jamaa amekataa kututajia aliyeiba.

Ama kweli, NGARENARO NI KUBWA KULIKO ARUSHA

Nakusifu kwa kutumia akili mazee. Na inaelekea huyo mwizi ni kibaka mnayekuwa naye karibu.
Huyo jamaa aliyekataa kutoa jina la mwizi ni heri mgempiga pasi ya shavuni, jina lingetoka tu.
 
Hapo ndio ujue Arusha si Dar,Arusha ni kama kitongoji cha Sinza,kwa Dar sahau kula kona kuna mafundi wa computer na pia kuna maduka mengi yanayouza charger na laptops,kwa hiyo njia kaka ukiibiwa Dar usahau
 
Back
Top Bottom