We si ulimpendaga Salim aliyetaka kufanya mke wa pili, pia ulimpenda na muinjilist? Au nimechanhanya mafaili.Throwback
Zamani hizo nishawahi kutongoza wakaka wawili
Wa kwanza
Huyo kaka nilikuwa nampenda mpk namuogopa yaani naona aibu nilikuwa natetemeka hata akinisemesha nikikutana nae na mkwepa
Nikamtuma best angu akamwambie mimi nimekufa kwake nimeoza [emoji23][emoji23] Yule mbwa alienda kumtongoza yeye akawa ana date nae sasa nikawa najiuliza yule kaka ina maana kanikataa ama… baadae nikaja kugundua ilikuwa ni nyege maana ndio nilianza kukuakuaa kipindi hicho
Yule jamaa tulivyokuwa wakubwa ndio alikuja kuniambia kwamba ujumbe haikufikishwaa badala yake niliemtuma aliniibia
Wa Pili
Kaka mmoja wa kisabato yule kaka ni handsome halafu ni wale tall na dark halafu ndevu zipo nikiwa niko first year yeye yupo mwaka wa 4 kwa mara ya kwanza tulikutana cafeteria weeee nilimpenda palepale alikuwa na best ake uzuri ukaja best ake alikuwa anafahamiana na best yangu akaja kumsalimia
Kijana nilievutiwa nae tumwite P yeye alibaki kwa mbali hakutusogelea pale tulipo basi wakasalimiana na rafiki angu wakaondokaa..
Nipo hostel na best yangu nikamuuliza habari za wale vijana ila P hakuwa akimjua alisema tu huwa anamuonaona tu pamoja na huyo best ake..
Siku hiyo tumekaa nikamkumbuka P ikabidi nimtege shoga angu vipi leo twende tukatembetembee hostel za kina P uzuri na yeye alikuwa na mishe za kwenda huko akasema jioni tutaenda… Kweli bhn jioni yake tukaendaa mpk hostel za kina P
Tulipoingia room tukawakuta vijana wengine tu wanapiga story wakatukaribisha tukakaa pale rafiki angu alikuwa msemaji mimi kwa kuwa sikuwa nawajua nilikua kimya tu najisemea moyoni mbona P hatokei
Tulikaa kama dk 10 nikamuuliza best angu mbona yule kijana simuonii?? Yeye akaniuliza kijana gani nikamwambia yule wa siku ile cafeteria si akaCheka kwa nguvu wale vijana wakasikia[emoji3][emoji3]
Ikabidi wamuulize vipi akawaambia namuulizia P weee jamani mashemeji ni wanoko kama unavojua wanaume kwa unafki wakachukua simu wakampigia
Oyaa kaka njoo huku kuna Pisi kali anakuuliziaa [emoji1787]Nyie jmn niliona aibu
Aisee P hakuchukua hata dk 5 akaingia room[emoji15] kumbe chumba chake kilikuwa floor ya juu tu
Basi bhn alivoingia nikaanza kujifichaficha si unajua tena aibu za kike[emoji6][emoji6] Wenzie wakaanza Mamamzungu uliekuwa unamuulizia kaja wee nilitamani kukimbia
Yule kaka alinisogelea mpk nilipokaa akanisalimia vizuri akaiuliza jina langu tukabadilishana namba akawa ananipigisha story mimi sasa ndio mpolee
Baada ya kurudi hostel zetu .. nikachukua simu yangu maana niliicha hostel (Mimi huwa sitembei na simu kubwa mara chache sana unikute barabarani nimeshika smartphone)… Nikaingia WhatsApp nikakuta P kanicheki
Tukachart chart basi lile likaka lilacs hata halinitongozi [emoji38][emoji38][emoji38]
Ikabidi mimi ndio nianze kazi ya kumtongoza na nyimbo za maua Sama ile ya mwenzako nakuelewa [emoji16][emoji16]
Ni hivi tulikuwa na urafiki but hakuwa kunitongozaa mpk anamaliza chuo.. kilichokuja kunikera kwake ni yeye kumwambia rafiki angu kuwa nimemtongoza aisee nilijisikia vibaya sana… nikamtoa moyoni na nikamwambia kwamba sikupenda kama alikuwa hanitaki asingemueleza best angu
Tangu siku hiyo mazoea yakaisha nikafuta namba yake alikuwa akinitafuta sijibu… imepita miaka mingi sasa tunawasiliana vizuri halafu sasa ndio ananitongoza nimemwambia tu hapana kwasasa sina hisia nae kabisaa
NB: Yule Kijana alikuwaga na demu wake niliambiwaga na best ake ndio maana aka ananikwepaa [emoji38][emoji38][emoji38]