Jinsi nilivyonusurika kufa leo asubuhi

Jinsi nilivyonusurika kufa leo asubuhi

Kumbe umebarikiwa dactari wa familia mna pesa jf member
 
Madud
Vipi Dawa Imeongeza Perfomance?
Kuna Vitu Vingine Mtakuja Kujiua We Unakunywa Juice ya Pilipili Unategemea Nini??
Tena Pilipili Za Tsh 1000😅😅🙌🙌
Madude ya hivi ukipewa uyafanyie postmorterm unaomba wakuache pekee yako unayatia walau vibao vitatu alafu unawaita ndugu na mashaidi waendelee kutazama maana ni lijinga la karne
 
Usipende kujaribu jaribu utajaribu kuliwa 0713.
All the best
 
Tatizo mnapenda sana kufatisha mambo ya mitandaoni ,utasikia mara ukinywa panadol na energy drink mkongo unasubiri na wewe unaenda kufakamia bila kujiuliza kama unaenda kujiua.
 
Dah, K hizi zitamaliza watu.
K zenyewe hazitosheki, wanaume wanajifia tu!
 
Wakuu habari zenu.

Leo ilikua siku yangu ya mwisho hapa duniani ni vile tu Mungu hakupanga.Ipo hivi 👎

Jana katika pitapita zangu humu j.f nikakutana na uzi ukisema juisi ya vitunguu swaumu na pilipili kichaa huongeza nguvu hasa ya tendo la ndoa.

Kwakua mimi ni mtu wa kujaribu jaribu vitu vipya nikaiweka kwenye notebook yangu ili leo nifanyie kazi.

Sasa jana usiku nilipiga konyagi mzinga ule mkubwa nikajilalia zangu.

Leo asubuhi kabla sijatoka nikasema em ngoja niende sokoni nikanunue vile vifaa nije nitengeneze juice yangu ili nikirudi jioni mama watoto apate chakula yake.

Nikanunua vitunguu swaumu vya elfu moja na pilipili kichaa ya elfu moja. Nikasaga kwenye brenda nikachanganya na asali nikaacha kwenye friji kwa nusu saa nikachukua nikapiga fundo kadhaa afu nikatulia.

Aisee baada ya sekunde kadhaa tumbo likaanza kunyonga vibaya mno(sijawahi kuumwa tumbo kama hii leo).Nikaanza kutoka jasho jingi utasema nimemwagiwa maji, nikakimbilia msalani nikakuta wife anaoga nikapiga mlango ikabidi anipishe atoke nje.

Nikazama toilet naugulia maumivu tu sipati haja yoyote nikarudi tena chumbani huku nagalagala🥲.

Kulikua na maji pale chumbani nikawa nakunywa ili nipunguze ule ukali wa tumbo.

Nikamwambia wife achukue pesa ya matumizi akanunue flagile (metronidazole) ili nipoze maumivu ya tumbo.

Niliendelea kuumwa vibaya mno hadi wife alipofika na dawa akanipa ninywe ili nipoze maumivu.🙏

Nilikwisha sahau kama nilikunywa mzinga wa konyagi ile jana usiku na asubuhi sikula chochote zaidi ya Juice ya vitunguu swaumu na pilipili kichaa.

Bahati nzuri nilikua natapika vibaya mno kwahiyo ile dawa sikunywa na nilikua natoa jasho jingi sana mwilini huku mapigo ya moyo yakienda kasi nikajua hapa sitoboi nasubiri miujiza tu.

Baada ya kutapika kwa mda mrefu na jasho jingi kutoka ile khali ikaanza kupungua na ile dawa flagile sikuigusa kabisa.Sasa baada ya kutulia nikaongea na Daktari wa familia akasema kama ningechanganya ile flagile na ile konyagi ya jana huenda ingekua ndio kifo changu maana haichukui round kuharibu mfumo mzima wa upumuaji na mapigo ya moyo yaani disulfiram like effects.🙆‍♂️

Je, ushawahi nusurika kufa kisa pombe au namna yoyote ile, ilikuaje?

View attachment 3152333
Natumai Leo usiku utaperfom vizuri kitandani kwani nguvu zako za kiume zimeongezeka mara dufu kiasi cha kuwa hotspot wanaume ulio karibu nao.
 
Mkuu pole sana na hayo Maswaibu yalishawahi kunitokea miaka fulani. Nilidanganywa na Wajinga fulani. Eti. Konyagi na red bull changanya halafu baada ya nusu saa kunywa panadol.

Chamoto nilikiona aisee
 
Pole sana mdau. Ila na mimi na wish nifikie viwango vya kwako kiuchumi. Kuwa na dakitari wa familia.
 
kwahiyo unachotaka kutuambia hapa ni huna nguvu za kiume, ndio ulikuwa unafuata ushauri wa humu ndani ila Bahat mbaya ulikosea masharti sio?
Niko vizuri sana mkuu ila ni kutaka kujaribu vitu vipya ndio yakatokea hayo.
 
Sasa mkuu,
Kwanini utake kujiboost namna hiyo, kwani shemeji alikuambia humridhishi?

Binafsi naona wanaume tunajipa matatizo wenyewe, yaani unataka umkomoe mwanamke kwa kumuweka sana?
Mkuu hua napenda kua strong wakati wote ndio maana nilitaka kuongeza na busta ya pilipili yakanikuta.
 
Vipi lakini ulijaribu mitambo kwa mkeo utupe mrejesho wa dawa au bado hadi usiku
Nijaribu wapi mkuu,nilitapika vyote mda ule ule yani bado sipo fresh hata nikipewa mbususu hapa naikataa
 
Back
Top Bottom