Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
sasa ungekufa ukijaribu, ridhika na ulivyo, nina uhakika ukimwambia wife ataomba talakaNiko vizuri sana mkuu ila ni kutaka kujaribu vitu vipya ndio yakatokea hayo.
😂Ungekufa kizembe sana kisa kutaka kupambana na mbususu. Ungekufa tungekuzika kwa huzuni kisha tomorrow we shall be lowering your wife's panty as we giggle at how stupid you were.
😅😅😅😅😅😅Madud
Madude ya hivi ukipewa uyafanyie postmorterm unaomba wakuache pekee yako unayatia walau vibao vitatu alafu unawaita ndugu na mashaidi waendelee kutazama maana ni lijinga la karne
Mkuu nenda kacheki kama una vidonda vya tumbo...fanya hivo mapemaWakuu habari zenu.
Leo ilikua siku yangu ya mwisho hapa duniani ni vile tu Mungu hakupanga.Ipo hivi 👎
Jana katika pitapita zangu humu j.f nikakutana na uzi ukisema juisi ya vitunguu swaumu na pilipili kichaa huongeza nguvu hasa ya tendo la ndoa.
Kwakua mimi ni mtu wa kujaribu jaribu vitu vipya nikaiweka kwenye notebook yangu ili leo nifanyie kazi.
Sasa jana usiku nilipiga konyagi mzinga ule mkubwa nikajilalia zangu.
Leo asubuhi kabla sijatoka nikasema em ngoja niende sokoni nikanunue vile vifaa nije nitengeneze juice yangu ili nikirudi jioni mama watoto apate chakula yake.
Nikanunua vitunguu swaumu vya elfu moja na pilipili kichaa ya elfu moja. Nikasaga kwenye brenda nikachanganya na asali nikaacha kwenye friji kwa nusu saa nikachukua nikapiga fundo kadhaa afu nikatulia.
Aisee baada ya sekunde kadhaa tumbo likaanza kunyonga vibaya mno(sijawahi kuumwa tumbo kama hii leo).Nikaanza kutoka jasho jingi utasema nimemwagiwa maji, nikakimbilia msalani nikakuta wife anaoga nikapiga mlango ikabidi anipishe atoke nje.
Nikazama toilet naugulia maumivu tu sipati haja yoyote nikarudi tena chumbani huku nagalagala🥲.
Kulikua na maji pale chumbani nikawa nakunywa ili nipunguze ule ukali wa tumbo.
Nikamwambia wife achukue pesa ya matumizi akanunue flagile (metronidazole) ili nipoze maumivu ya tumbo.
Niliendelea kuumwa vibaya mno hadi wife alipofika na dawa akanipa ninywe ili nipoze maumivu.🙏
Nilikwisha sahau kama nilikunywa mzinga wa konyagi ile jana usiku na asubuhi sikula chochote zaidi ya Juice ya vitunguu swaumu na pilipili kichaa.
Bahati nzuri nilikua natapika vibaya mno kwahiyo ile dawa sikunywa na nilikua natoa jasho jingi sana mwilini huku mapigo ya moyo yakienda kasi nikajua hapa sitoboi nasubiri miujiza tu.
Baada ya kutapika kwa mda mrefu na jasho jingi kutoka ile khali ikaanza kupungua na ile dawa flagile sikuigusa kabisa.Sasa baada ya kutulia nikaongea na Daktari wa familia akasema kama ningechanganya ile flagile na ile konyagi ya jana huenda ingekua ndio kifo changu maana haichukui round kuharibu mfumo mzima wa upumuaji na mapigo ya moyo yaani disulfiram like effects.🙆♂️
Je, ushawahi nusurika kufa kisa pombe au namna yoyote ile, ilikuaje?
View attachment 3152333
Hayo ni masaa ya waoga, yenyewe ni 8..!!Mbona nasikia ni masaa 72 baada ya pombe ndio unywe dawa