MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 21,387
- 44,030
Miaka hiyo nikiwa nimepigika vibaya mno kiuchumi nilibahatika kukutana uso kwa uso na takrima toka kwa Lema wa CHADEMA. Enzi hizo ilikuwa kawaida sana kutembea kwa mguu toka Mianzini hadi Kerai kutokana na hali ya kiuchumi kutokuwa rafiki. Ilikuwa nikikata kona pale round about ya Florida kuitafuta Levolosi kisha Ngarenaro ndani ya muda mchache najikuta kona Mbauda, JR mwisho Kerai. Kiafya nilikuwa fit mno.
Siku moja nikiwa kwenye matembezi yangu nikaona nipite shortcut fulani inayoanzia stendi ya Mirongo.. nikiwa ndo nimekunja tu kona ndanindani nje ya kibaa fulani nikakuta Lema yuko na watu wengine wamemzunguka akiwaelezea mambo ya siasa. Nikasimama nisikilize. Enzi hizo alikuwa TLP.
Mara ghafla Lema akaagiza mhudumu wa kile kibaa atupe maji ya kunywa wote tuliokuwa pale. Ikumbukwe hiyo siku nilikuwa nimetembea kwa mguu kutoka Kona Ilboru na kulikuwa na jua kali. Kiukweli ile chupa ya maji baridi ilikuwa na maana kubwa sana kwangu. Ninamshukuru sana Lema kwa ile takrima.
Ninamshauri Lema arudi TLP kwa sababu ndo nyota yake iling'aa sana akiwa huko. Huku CHADEMA anachonganishwa mno na wapiga kura wake. Lema ni mwanasiasa mzuri akiwa TLP. Mimi kwenye ukuaji wangu nilikuwa sijui mwanasiasa mwingine wa upinzani zaidi ya Lema kwenye jimbo la Arusha. CHADEMA inaharibu mno wanasiasa.