Jinsi nilivyothibitisha Uchawi, hutoamini nakwambia!

Hakuna uchawi. Uchawi haupo.

Ni watu wapumbavu [blithering idiots] tu wanaoamini uchawi upo.

Sasa ukichanganya ujinga na upumbavu, unapata uzuzu.

Siku hizi kuna drones ambazo hazionekani kwa rada.

Mtu akirusha stealth drone yake yenye uwezo wa kufanya mashambulizi na kumlenga adui na kumuu bila kujua hizo risasi zimetoka wapi, mazuzu wanasema huo ni uchawi kumbe ni sayansi tu na teknolojia.

Ni rahisi sana kuwadanganya Watanzania.
 
Sikia mkuu unaongea kwa sababu hujawahi kutana na TUKIO ZITO wewe, na hujawa exposed to maisha
 
Mkuu elezeaa vizuri
 
Vipi kama huo uchawi ni jina la teknolojia ya kiafrika ambayo huwezi kuiona kwa macho kama ambavyo unajua una malaria ila huwezi kuviona vimelea kwa macho bila kupitia microscope..

Sasa kama wewe unaaminishwa unaumwa malaria kwa dalili tu pasipo kuthibitisha kwa microscope "mwenyewe" Kwa sababu huna utaalamu huo, kwa nini umuone mtu mwendawazimu kwa kuamini anarogwa na akaponywa na mtaalamu kwa sababu tu "hujauona huo uchawi kwa macho"..
 
Yeah. Ni kweli kwani watanzania ni wepesi kuamini badala ya kuchunguza, kudadisi au kutafakari kwa kina kwanza; wengi wakikosa jawabu, haraka wao hukimbilia jawabu rahisi i.e. ni Uchawi. Ukimwambia akuelezee huo uchawi ukoje anaishia kukwambia "we hayajakukuta".
 
Mkuu elezeaa vizuri
Ata musa naharuni walivoagizwa kwa farao ili awaachie wana wa israil[waliagizwa na MUNGU,]MUNGU aliwapa fimbo akamwambia musa,ukifika farao atatuma wachawi waje wawajaribu wakitupa fimbo zao na wewe tupa fimbo yako,basi walipofika kule walifanya ivo,wachawi walipotupa fimbo zao za kichawi zikageuka nyoka,musa nae akatupa fimbo alopewa na MUNGU,basi fimbo ya musa ikageuka nyoka,na nyoka wa musa akameza fimbo za wachawi
 
Kwa mantiki hiyo, ina maana kwamba Mungu ni mchawi zaidi sio?
 
Wewe unalala njaa ndio maana unaota ndoto za ajabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…