Jinsi nilivyothibitisha Uchawi, hutoamini nakwambia!

Hahahahahah

Ila uchawi upo Hilo hata usikatae
 
Utajuaje kama uchawi upo kama hu-, practice uchawi wenyewe?

Ili ujue uchawi upo anza kuufanya na kuusoma vizuri.
Ujue miti yote na kazi zake,
Ujue mimea yote na kazi zake,
Ujue baadhi ya michoro ya kichawi na kazi zake,

Na pia ikiwezekana nenda kwa Mganga ukafanye utafiti ili ujue kama uchawi upo na unafanya kazi ama laa.

Hapo nitakuona umefanya la maana na unastahili kuwa na hiyo BLUE TICK.

Ushuhuda wangu kuhusu uchawi.

Alikuwepo Bamdogo wangu hakuwa amezaliwa na kifafa ila cha kushangaza alipofikisha miaka 31 alianza kudondoka kifafa.
Tulimpeleka hospitali kwa ajili ya matibabu lakini hali yake iliendelea kuwa mbaya.

Hapo Mzee ilibidi ajiongeze kujaribu upande wa asili Ili kunusuru uhai wa Bamdogo, Nakuambia haikupita hata siku 3 mgonjwa wetu alipona kabisa na mpaka leo ana miaka 44 hajawahi kuanguka tena, Na kwa maneno ya Mganga alitupiwa kifafa ( Sijui hii teknolojia inavyofanya Kazi).

Naamini wewe ni Msomi na unaweza kutenga mda wako kujifunza kitu kipya. No research no right to speak.

Lakini ukiwa mtu wa keyboard tu. Mpaka unafariki unaweza usishuhudie hii teknolojia ya asili inavyofanya kazi.
 
Blah blah blah.
 
Nanukuu: "Naamini wewe ni Msomi na unaweza kutenga mda wako kujifunza kitu kipya. No research no right to speak".
Sawa kabisa. Sasa ww unayetusemesha hapa (comment) tuanzie kwako. Leta Research findings zako hapa ili tuweze kukusikiliza. Tofauti na hapo; U have no right to speak.
 
Huwa najiuliza hivi hizo tekinolojia kwanini zisitumike kutuletea maendeleo, au zikawa kama silaha dhidi ya mataifa makubwa hayo yenye dhuluma na ushenzi wa kila aina?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…