Hahahaaa!
Blah blah nyiiingi lakini uthibitisho hakuna.
Wengine walisema niende Gambosi nikajionee mwenyewe. Nikaenda na sikuona chochote zaidi ya ujinga na umaskini tu.
Tanga nimefika. Nimelala sana Mkonge hotel enzi hizo. Sikuona uchawi wala nini.
Uchawi haupo.
Utajuaje kama uchawi upo kama hu-, practice uchawi wenyewe?
Ili ujue uchawi upo anza kuufanya na kuusoma vizuri.
Ujue miti yote na kazi zake,
Ujue mimea yote na kazi zake,
Ujue baadhi ya michoro ya kichawi na kazi zake,
Na pia ikiwezekana nenda kwa Mganga ukafanye utafiti ili ujue kama uchawi upo na unafanya kazi ama laa.
Hapo nitakuona umefanya la maana na unastahili kuwa na hiyo BLUE TICK.
Ushuhuda wangu kuhusu uchawi.
Alikuwepo Bamdogo wangu hakuwa amezaliwa na kifafa ila cha kushangaza alipofikisha miaka 31 alianza kudondoka kifafa.
Tulimpeleka hospitali kwa ajili ya matibabu lakini hali yake iliendelea kuwa mbaya.
Hapo Mzee ilibidi ajiongeze kujaribu upande wa asili Ili kunusuru uhai wa Bamdogo, Nakuambia haikupita hata siku 3 mgonjwa wetu alipona kabisa na mpaka leo ana miaka 44 hajawahi kuanguka tena, Na kwa maneno ya Mganga alitupiwa kifafa ( Sijui hii teknolojia inavyofanya Kazi).
Naamini wewe ni Msomi na unaweza kutenga mda wako kujifunza kitu kipya. No research no right to speak.
Lakini ukiwa mtu wa keyboard tu. Mpaka unafariki unaweza usishuhudie hii teknolojia ya asili inavyofanya kazi.