Endelea ...
Baada ya kufika kijijini pale Ikuti tulikaribishwa vizuri kijiji kilikuwa kimezungukwa na migomba ya ndizi mingi ,wenyeji wa kijiji kile ni wakulima wa ndizi na kahawa sana sana,hivyo basi tukakaribishwa kwa kinywaji cha kahawa na ndizi za kuchemsha mara kwa mara.Kama nilivyosema ilitubidi tukae pale kama mwezi.
Nilianza kupatiwa matibabu taratibu taratibu na kuna kipindi mganga alilazimikabkusafiri kwenda Mbarali ,Dar na maeneo ya karibu kutafuta baadhi ya dawa alizokuwa anaoteshwa na mizimu baada ya mwezi atimaye taratibu nikaanza kuona nafuu na fahamu na kumbukumbu zikaanza kurudi taratibu sasa niawa naweza hata kuongea na kuuliza maswali na watu wakawa wananiadithia kilichotokea .
Ila kwa sasa sikuwa na uwezo wa kutembea au kusogeza kiungo changu maana bado vilikuwa vimekakamaa hivyo nikawa kama mlemavu.
Yule mganga alijitahidi sana kurejesha ukomavu wa viungo lakini haikuwa rahisi ,hivyo nikashukuru tu Mungu mpaka hapo aliponisaidia maana kutoka kuooteza fahamu na kumbukumbu mpaka kurudi kwenye hali ya kawaida sikuwa na budi kushukuru.
Ila baada ya kutibiwa na kupata unafuu ilibidi nipate dawa za kujikinga na watu wabaya maana hii ilikuwa kama ni vita mtu anayekuroga akikuona umepona anatamani akuue kabisa .
Hapa ilibidi sasa twende kwa mtu mmoja ambaye alikuwa na ukaribu sana na watu wa familia ya chifu wa kabila ili kupata hiyo kinga ,na inasemekana ni kinga hatari sana kama binadamu atakuwa nayo ndio inayotumika kukinga familia za ki chifu.
Sitopenda kutaja jina la hiyo kinga maana msomaji unaweza ogopa ,ila ni dawa fulani ambayo ukipewa unakuwa mtu hatari sana inasemekana hii dawa ilitumika hata kipindi cha manabii ukitumia wachawi wa kijiji kizima utakachoingia wanapata taarifa kwamba kuna mtu ambaye sio wa kawaida ameingia kwenye ardhi yao ,kiufupi inauwezo wa kuwazuia hata kufanya mambo yao ya kichawi kijijini na wakitembea unakuwa unawaona ,uwepo wako unawafanya wachawi washindwe kupaisha nyungo zao usiku yaanj ina mambo mengi sana kama ile fimbo ya Mussa matumizi ya hii dawa maana unaweza hata kusafiri kimazingara bila mtu kukuona.
Dawa hii ina mambo mengi sana ila haitolewi hivi hivi wala hakuna mtu au binadamu anaweza kupewa isipokua mtu wa karibu wa ukoo wa kichifu kama una ukaribu naye unaweza ukamuomba kama utakuwa na bahati mizimu ya kichifu ikakupenda na kuona kwamba hauna nia ya kuitumia vibaya anaweza kukupatia vumbi lake ambalo linachanganywa na sarafu ya kale yenye miaka zaidi ya mia na.
Hatimaye nilifanikiwa kupata dawa zote na kinga zote nikarudi Dar Es Salaam,nikiwa nimepona lakini sikuwa na uwezo wa kutembea maana viungo vilikuwa vyote vimekufa .
Itaendelea..