Fuatana na mimi sasa
Baada ya kuwa nimejirusha kwenye maji dada yangu anaendelea kunisimulia kuwa nilionyesha umahiri wa hali ya juu wa kuyakata maji huku nikizama na kuibuka, katika hali ya mshangao kuna wakati nilizama kwenye maji na nikaibuka na mamba nikiwa nimemkaba koo kisawasawa hali akawa anatoa machozi.Hali ilizidi kuwa ni ya taharuki baada ya yule mamba kunizidi nguvu na kuanza kunishambulia ,watu wote walianza kushika vichwa vyao na kuanza kuomboleza.Ghafla yule shemeji yangu mtu wa Dar es salaam aliamua kujitosa kichwa kichwa kwenye maji kitendo ambacho kiliwashangaza wengi kwa sababu alikuwa hajui kuogelea hasa ukichukulia yeye ni mzaliwa wa Dar es salaam maeneo ya Kazula mimba mkoani Dododoma.itaendelea