Jinsi nimwonavyo NILHAM RASHED . . . .

Jinsi nimwonavyo NILHAM RASHED . . . .

Nafikiri nilham amekamata nafasi ya malaria sugu katika upande wa pili wa shilingi.
 
ameen ya raab...:clap2:

Nimefurahi Nilham dua kuitikia
Dua uloitikia Rahman aijubu
Walimwengu waeleze we ndo wangu muhibu
Wajuze wafaham me ndo wako tabibu
Yale maradhiyo polepole hukutibu
Watamkie bayana usikae kama bubu
 
Nilham mnayemuona kwenye avatar sio yeye. Siva zake halisi hizi hapa chini:

Nilham ni mfupi, wa kimo sio mawazo,
Huvaa sketi fupi, ana ndevu si mchezo,
Hupenda kulamba pipi, nywele kichwani tatizo,
Avatar zinadanganya, Nilham namjua.
 
haya my dear nakusoma habiby wangu ila mi siwezi kujibu kimashairi ispokuwa yanisuuza na kuutoa uchafu niliopakwa na wasiojua kupenda wa kunyenyekea....inshallah tutadumu mimi na wewe na maisha tufurahie... mapenzi kupendana si kukerana inshallah kheyr..:first:
Nimefurahi Nilham dua kuitikia
Dua uloitikia Rahman aijubu
Walimwengu waeleze we ndo wangu muhibu
Wajuze wafaham me ndo wako tabibu
Yale maradhiyo polepole hukutibu
Watamkie bayana usikae kama bubu
 
heheheh haya waambie angalau wapunguze kasi... kwani kumbe sura ndio kosa hapa??
Nilham mnayemuona kwenye avatar sio yeye. Siva zake halisi hizi hapa chini:

Nilham ni mfupi, wa kimo sio mawazo,
Huvaa sketi fupi, ana ndevu si mchezo,
Hupenda kulamba pipi, nywele kichwani tatizo,
Avatar zinadanganya, Nilham namjua.
 
Nafikiri nilham amekamata nafasi ya malaria sugu katika upande wa pili wa shilingi.

Daaah . . . ina maana nafananishwa na MS upande wa pili au?? :twitch:
 
Nimefurahi Nilham dua kuitikia
Dua uloitikia Rahman aijubu
Walimwengu waeleze we ndo wangu muhibu
Wajuze wafaham me ndo wako tabibu
Yale maradhiyo polepole hukutibu
Watamkie bayana usikae kama bubu

Duuuh
Jamaa ana mashairi utafikiri alianza kuimba tumboni kwa mama ake
Ngoja nichote ujuzi . . . :coffee:
 
hehehehheehhe... ukishauchota upitie huu upande wangu unipunguzie na mie..
Duuuh
Jamaa ana mashairi utafikiri alianza kuimba tumboni kwa mama ake
Ngoja nichote ujuzi . . . :coffee:
 
waache waseme my dear we hujazoea tuu binaadam ndo tulivyo hivi.... ndio maana pia kukaumbwa na kitu subra...okay??? soo leave it ... and leave it to them what ever they say bora ukweli naujua mimi na wewe.... keep it up my boy...:clap2::clap2:

Nakupata vizuri mamiiii:yo:
Hata waone gere vipi mi nitaendelea kumwaga mistari :drum:
Nishawapotezea

:loco::loco::loco::loco:
 
Duuuh
Jamaa ana mashairi utafikiri alianza kuimba tumboni kwa mama ake
Ngoja nichote ujuzi . . . :coffee:

Ukikipenda moyoni hakika utakijua
Mola mwema atajaalia akili kuifungua
Mashairi kuminika yenye nahau kujawa
Usijali jitahidi mbona unacho kipawa???
 
hehehehheehhe... ukishauchota upitie huu upande wangu unipunguzie na mie..

Hana haja ya kupita mimi ntakufunza
Si mashairi pekee namizungu utaijua
Tena ila ya kishua penzi letu kulitunza
Utakua ukighani huku mimi nakutunza
 
mmmmmh inshallah....heheheh usinitie haya basi mwenzio nakwambia mi siwezi kuyatunga kama hivi...
Hana haja ya kupita mimi ntakufunza
Si mashairi pekee namizungu utaijua
Tena ila ya kishua penzi letu kulitunza
Utakua ukighani huku mimi nakutunza
 
hehehehheehhe... ukishauchota upitie huu upande wangu unipunguzie na mie..

Utapata tu mamiii
Maana jamaa anamwaga mi-line ka vile mdogo wake Amr Diab
Ngoja nii-copy then nai-analyse
 
Nilham mnayemuona kwenye avatar sio yeye. Siva zake halisi hizi hapa chini:

Nilham ni mfupi, wa kimo sio mawazo,
Huvaa sketi fupi, ana ndevu si mchezo,
Hupenda kulamba pipi, nywele kichwani tatizo,
Avatar zinadanganya, Nilham namjua.

Tafadhi kashaijabutege naomba uache mabezo
Nilham hawezi vaa nguo fupi hawezi huo mchezo
Acha sifa mbaya kumpatia ukajaleta mzozo
Nywele ndufu kajaaliwa zanipa mimi liwazo
Naomba uishie hapo uache yako mawazo
 
Check jibu hilo sasa . . . . kudadadadadadeki
Utafikiri ana madesa
 
Back
Top Bottom