fimboyaukwaju
JF-Expert Member
- Aug 3, 2020
- 2,977
- 3,798
Leo nawaletea changamoto nyingine ninayokumbana nayo baada ya kuzungumzia gharama za maji ya kunywa na umeme. Safari hii ni kuhusu gharama za usafi wa nyumba na mwili:
a) Usafi wa Nyumba (Eneo la Maliwato)
Eneo la maliwato, ambalo lina choo na bafu, kwa Waingereza huitwa self-contained. Kwenye sehemu hii, natumia vifaa na bidhaa mbalimbali kama:
1. Choo cha kukaa,
2. Choo cha kukojolea wanaume, na
3. Choo cha kukojolea wanawake.
Hii tumeweka ili kuzuia maambukizi kama UTI. Tunashirikiana na mke wangu kutumia choo cha kukaa pekee. Changamoto kubwa ni kwamba mimi nina passion ya usafi, hivyo kila siku nafanya usafi wa:
Hii hali inagharimu sana. Watoto wangu hufadhaika na kuhoji matumizi makubwa ya sabuni na vifaa. Wanapokuja na wake au waume zao, huniuliza jinsi ninavyohakikisha usafi wa kiwango hiki. Ninawaeleza hatua kwa hatua huku mke wangu akicheka.
Pesa nyingi hutumika kwa bajeti ya vifaa hivi. Sipendi kabisa harufu mbaya, ndiyo maana nawekeza sana kwenye usafi wa eneo hili.
b) Usafi wa Mwili
Hapa, matumizi yangu ni makubwa pia. Ninatumia pesa kununua:
Nina tabia ya kupiga mswaki mara tatu kwa siku na kusukutua pia mara tatu kwa siku. Kabla ya kutoka kwenda mjini, humuomba mke wangu aninuse mdomo ili kuhakikisha uko safi.
Huu ni ugonjwa wangu wa usafi ambao unanigharimu pesa nyingi sana. Watoto wangu huchukua jukumu la kununua vifaa hivyo kwa zamu huku wakicheka kuhusu tabia yangu ya usafi.
Ingawa usafi huu unanigharimu, najivunia kuwa na mazingira safi na mwili uliotunzwa. Ni changamoto inayohitaji bajeti kubwa, lakini inanipa utulivu wa akili na furaha ya maisha.

- Sabuni za unga na maji,
- Madawa ya kuua wadudu kama Jik na Dettol,
- Sabuni zenye harufu nzuri, na
- Pafyumu za hewa nzuri, za kupulizia na zile zisizohitaji kupulizwa.
1. Choo cha kukaa,
2. Choo cha kukojolea wanaume, na
3. Choo cha kukojolea wanawake.
Hii tumeweka ili kuzuia maambukizi kama UTI. Tunashirikiana na mke wangu kutumia choo cha kukaa pekee. Changamoto kubwa ni kwamba mimi nina passion ya usafi, hivyo kila siku nafanya usafi wa:
- Choo,
- Chumba cha kulala, na
- Kitanda.
Hii hali inagharimu sana. Watoto wangu hufadhaika na kuhoji matumizi makubwa ya sabuni na vifaa. Wanapokuja na wake au waume zao, huniuliza jinsi ninavyohakikisha usafi wa kiwango hiki. Ninawaeleza hatua kwa hatua huku mke wangu akicheka.
Pesa nyingi hutumika kwa bajeti ya vifaa hivi. Sipendi kabisa harufu mbaya, ndiyo maana nawekeza sana kwenye usafi wa eneo hili.
b) Usafi wa Mwili
Hapa, matumizi yangu ni makubwa pia. Ninatumia pesa kununua:
- Vifaa vya kunyolea, sabuni yake, na aftershave,
- Taulo za aina tatu (uso, mgongo na tumbo, na sehemu za siri),
- Dawa ya mswaki na dawa za kusukutua mdomo.