Jinsi panya wanavyofundishwa kugundua mabomu SUA Morogoro kitengo cha APOPO

Jinsi panya wanavyofundishwa kugundua mabomu SUA Morogoro kitengo cha APOPO

bf59f36d638f553961c3df2bfeee6b91.jpg
 
Nikagundua kuwa panya anaweza kutumika kwa mambo mabaya na mazuri Nimeanza kuwafundisha panya kuzijua noti na kuzibeba yaani kuhamisha kutoka sehemu moja kwenda nyingine, kuzitafuta zilipo ikiwa ni ndani na kuzileta nje.

Zoezi ni gumu lakini naendelea vizuri nitaleta mrejesho nikifikia mwisho hivyo naomba ushauri zaidi kwa wataalamu wa kufundisha wanyama.

Naona mpango wako ni mzuri sana ni mfano wa chuma ulete au mang'opo fulani hivi kila lakheli kwa hilo
 
Usije kumuadhibu tu
 

Attachments

  • 1450802412099.jpg
    1450802412099.jpg
    24 KB · Views: 222
Hawa viumbe wana akili sana hata mitego wanajua kuitegua. Paka siku hizi hawatishi hata kidogo
 
de798f03c8fa8f33ee40cfd49e9b769f5a8f1aa0_254x191.jpg

Bart weetjens​

APOPO(anti-persoonsimijnen otmijnende product ontwikkeling)

APOPO ni belgium non government organization ambayo hufundisha waafrika kuwafundisha panya kugundua mabomu ambayo yametegwa ardhini,hii organization ilianzishwa mwaka 1997,ambapo kwa Afrika makao makuu yao ni Tanzania morogoro chuo cha kilimo SUA.

Bart weetjens ndie mwanzilishi wa APOPO pia ndie mkufunzi au mgunduzi wa kwanza wa panya wanaotegua mabomu,amesomea chuo kikuu Antwerp huko ubelgiji.

Bart ktk ukuaji wake alizoea kukaa karibu na panya hivyo aliweza kuchambua upekee wa panya na wanyama wengine hasa ktk uwezo wa kunusa.

Nje ya panya kuwa mharibifu na kuwa adui wa mwanadamu lkn pia panya huyohuyo anaweza kuokoa maisha ya mwanadamu ni vile tu unavyoweza kumtumia!.

Panya aina ya rodent ndio hasa hupendwa kutumiwa ktk kazi hii ambao ktk nchi yetu hupatikana kwa wingi!

Nafikiri hiyo ni moja ya sababu APOPO kuja Tanzania.
 
Hivi ndivyo wafanyavyo SUA ktk kuwafundisha panya
hatua ya kwanza ni kumfanya panya kuwa rafiki na binadamu..zoezi hili huanza wiki nne baada ya panya kuzaliwa hapa mwalimu humkaririsha sauti panya(sauti ya mwalimu) na harufu ya mwalimu!.hivyo humsaidia panya kumng'amua mwalimu wake na pia humjengea mazingira huru ya kutomuogopa..

hatua ya pili ni kutambua sauti na kupewa chakula
hapa panya hupigiwa alarm fulani kisha anapewa chakula hivyo hukariri mlio huo na kuanza kutambua,kiufupi naweza sema huimarishiwa uwezo wake wa kukariri,zoezi hili huchukua wiki mbili.

hatua ya tatu hufaamika kama tundu moja
hapa panya hufundishwa kunusa na kukariri harufu ya unga wa baruti ktk tundu moja(huu ndio unga unaokuwa kwenye bomu) kisha hupewa chakula.

hatua ya nne hufaamika kama matundu mawili
moja huwekewa kitu chengine na tundu jengine huwekewa unga wa bomu(baruti) hapa panya anatakiwa atambue tundu lenye unga wa baruti ndio apewe chakula! hii humuundia uwezo wa kufanya kazi hiyo ya kung'amua unga kwani
 
tayari anakuwa anajua kuwa aking'amua unga huo hupewa chakula hivyo hufanya kwa bidii.

hatua nyengine huongezewa sampuli nyingi zaidi ili kuona kama amekariri na hivyo hutakiwa kunusa na kuonyesha ni tundu lipi au wapi kuna unga wa baruti ambapo akifuzu hupelekwa hatua nyengine na hapa panya hufuzu kutokana na uroho wake kwani anajua bila hivyo hapati msosi!

hatua nyengine panya hupelekwa porini na huchimbiwa vyombo vya bati vilivyo na aina mbalimbali ya vitu na hapo pia hutakiwa kung'amua wapi unga wa baruti ulipo.
mbali na kugundua mabomu pia panya anauwezo wa kufukua ambao hutumia uwezo huo kufukua mabomu..
pia hufundishwa kubaini mabomu ktk umbali tofauti kuanzia mita tatu hadi tano.
pia hatua ya mwisho kabisa panya hutakiwa kufukua eneo la ukubwa wa mita mraba 400! akifuzu hapa ndio amefuzu na hutumika kuwa panya wa kugundua mabomu.

nje na hapo panya hawa hutunzwa kwa kupewa tiba na msosi mzuri kbs,hupewa karoti,dagaa,karanga,ndizi,maji n.k pia hupimwa uzito na hupimwa afya zao kama wanaumwa wanatibiw
 
kwanini panya wanatumika kugundua mabomu...?
Huweza kung'amua mabomu mengi kwa muda mchache.
anauzito mdogo ambao hata akisimama juu yake ni ngumu kulipuka.
anauwezo mkubwa wa kunusa na kuchimba.
hana gharama kubwa ktk mahitaji.
mwepesi kufundishika.

Panya hutumika kung'amua mabomu ila wametumia neno kutegua kama kung'amua,akishang'amua eneo lenye bomu mkufunzi wake huweka alama na huja wataalumu wa mabomu kuja kutegua.

Panya wa SUA wanauwezo wa kung'amua TB kwenye makohozi ya mtu anaeumwa TB.
hebu wawafundishe na harufu ya mtu alietoka kuchepuka!
ha ha! nawajoke tu!.

Hii imenifunza kuwa binadamu tunauwezo mkubwa sana na tunaweza kuendesha dunia vile tutakavyo!
kwa manufaa yetu leo hii panya anaokoa maisha ya wanadamu ambao walitakiwa wafe kwa mitego walioekewa na adui zao! hebu fikiri mpo ktk purukushani ya vita familia yako inaangamia ktk harakati za kujiokoa kukimbia huku na kule wanakanyaga mabomu hlf kumbe panya aliekula file lako juzi na kumuua angeweza kuokoa familia.
thanks to BARK WEETJENS
 
hivi dunia ya sasa bado kuna mabomu ya kupanda ardhin?
kwanini yakose..?
vita si kitu cha hovyo ndugu na wengine wanayatumia ili kujilinda.. au kama alam! pale adui anapotimba anga husika
 
Back
Top Bottom