tayari anakuwa anajua kuwa aking'amua unga huo hupewa chakula hivyo hufanya kwa bidii.
hatua nyengine huongezewa sampuli nyingi zaidi ili kuona kama amekariri na hivyo hutakiwa kunusa na kuonyesha ni tundu lipi au wapi kuna unga wa baruti ambapo akifuzu hupelekwa hatua nyengine na hapa panya hufuzu kutokana na uroho wake kwani anajua bila hivyo hapati msosi!
hatua nyengine panya hupelekwa porini na huchimbiwa vyombo vya bati vilivyo na aina mbalimbali ya vitu na hapo pia hutakiwa kung'amua wapi unga wa baruti ulipo.
mbali na kugundua mabomu pia panya anauwezo wa kufukua ambao hutumia uwezo huo kufukua mabomu..
pia hufundishwa kubaini mabomu ktk umbali tofauti kuanzia mita tatu hadi tano.
pia hatua ya mwisho kabisa panya hutakiwa kufukua eneo la ukubwa wa mita mraba 400! akifuzu hapa ndio amefuzu na hutumika kuwa panya wa kugundua mabomu.
nje na hapo panya hawa hutunzwa kwa kupewa tiba na msosi mzuri kbs,hupewa karoti,dagaa,karanga,ndizi,maji n.k pia hupimwa uzito na hupimwa afya zao kama wanaumwa wanatibiw