Jinsi Pele alivyoipaisha PUMA...

Jinsi Pele alivyoipaisha PUMA...

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
15,460
Reaction score
24,233
Wengi hawajui kwamba Puma na Adidas ni ndugu yaani ni brainchild ya mtu na kaka yake ambao waligombana na mpaka wanafariki walikuwa na chuki kubwa baina yao hata hawakuzikana, hio ni story ndefu na ya siku nyingine ila kuweza kuipata unaweza ukatafuta kuhusu The Dassler brothers yaani Adolf ("Adi") and Rudolf ("Rudi") Dassler..

Sasa hawa walikuwa na Kampuni ya Viatu na walikuwa na business model ya kusign mastar (Mfano Jesse Owens kwenye Olympic ya Ujerumani); baada ya kugombana kila mmoja akaunda Kampuni yake Adidas (Adi) na Puma (Rudolf) sasa hawa jamaa mpaka wanazeeka walikuwa bado wanajaribu kuharibiana na kuhakikisha kila mmoja anamzidi mwenzake, ugomvi huu ulifikia hadi kwa watoto wao ambao walikuja kuwa ndio wasimamizi wa Kampuni husika..,

Kipindi cha WordCup ya 1970; hawa watoto wa hao makaka wasiopendana walifahamu kabisa kwamba hakuna Star zaidi ya Pele na kila mmoja akitaka kumpa mkataba avae kiatu chake wangepandishiana dau na mpaka wote kufirisika, Hivyo wakaingia Gentleman agreement (PELE PACT) kwamba hakuna wa kumsign Pele.., yaani yoyote ni sawa ila sio Pele...

Sasa ilikuwa ni jambo la kushangaza na kushitua baada ya World Cup kuanza wadau wa Adidas kuona Pele amevaa Puma..., na sio kuvaa tu bali alifanya trick ya kujifanya anafunga kamba ya Kiatu hivyo TV zote majumbani kwa wote wenye TV kwa kipindi hicho waliweza kuona PUMA.....

View: https://youtu.be/ZpYlGhsAXLE?si=4uxtBfLAtmLHmG8i
 
Ilikuwaje Pele akavaa kiatu cha kampuni ya PUMA wakati mkataba ulikuwa unataka asiwepo wa kuingia nae mkata wa kibiashara?.

Logikos
Ni kwamba Puma alimsaliti Adidas alimdanganya kwamba hatamsign pele ila akamfuata kwa siri na kumsign inasemekana alipewa 120,000 usd.

Kwahio Puma alimsaliti Addidas
 
  • Thanks
Reactions: K11
Puma saa hizi wanapumulia mipira, Adidas anamkimbiza.

Ila hii trick puma walicheza sana, ingekuwa ni miaka hii ya utandawazi, wangeuza mnoo
 
Puma saa hizi wanapumulia mipira, Adidas anamkimbiza.

Ila hii trick puma walicheza sana, ingekuwa ni miaka hii ya utandawazi, wangeuza mnoo
Ingawa huenda ugomvi wao uliwafanya wajitahidi ili kumpita mwenzako hivyo kuwa Kampuni kubwa ulimwenguni au walichofanya kilimpa mwanya NIKE kuweza kuwapita wote...
 
wezenu wanagombania biashara nyie mnagombania vidonda ndugu
Ni upuuzi hata kwa wao kugombana ila hii ilipelekea hadi miji miwili yote kugombana sababu ilikuwa inatengwa na mto kwahio hadi huko watu waliwaita a town of bent necks..., Yaani kila mtu akiwa anatembea anaangalia chini umevaa nini ili aone kama atakusalimia au hapana ? Ingawa mayor wao ili kujaribu kuunganisha watu alikuwa anavaa viatu vyote Puma na Adidas (ukizingatia pia hizi kampuni zilikuwa major employers)
 
Bora wao ipo siku watapatana na nyie kwenye vidonda ndugu mkipata ukimwi anawapatanisha nan
 
Bora wao ipo siku watapatana na nyie kwenye vidonda ndugu mkipata ukimwi anawapatanisha nan
Walikufa bila kupatana na wala hawakuzikana; walifikia hadi hatua ya kuchongeana ili mmoja wao aweze kufungwa in short vita vyao vilikuwa ni balaa na huenda wasingetengana Adidas ingekuwa bora zaidi kwani Adolf alikuwa mbunifu sana na Rudolf alikuwa ni Marketing Genius..., Na Ugomvi huu ulihamia hadi kwa watoto ambao mmoja wao alimsaliti mwenzake kwenye Pele Pact...
 
wabakie hivyo hivyo wakipatana kampuni zao zitakufa
 
wabakie hivyo hivyo wakipatana kampuni zao zitakufa
Kampuni sio zao tena zilishauzwa na wamiliki ni wengine ila arguably unaweza kusema kwamba vita vyao vilimpa upenyo NIKE, pia Puma bila Creativity ya Adidas ilikosa muelekeo na Adidas bila Charisma na Salesmanship ya Rudolf ilipoteza kitu fulani ila ndio hivyo Hadithi yako ya Maisha yao ni ya Kusisimua na Kushangaza na ni from rags to riches na creativity sababu kabla yao kulikuwa hakuna specialized sports shoes...; Na arguably Adolf ndio alifanya Ujerumani ikachukua kombe la dunia (sababu aliingia nao mkataba wavae Adidas) na mechi ya mwisho aliwapa viatu ambavyo unaweza ukaongeza (unscrew) meno hivyo kwa hali ya hewa ya mvua iliwasaidia wajerumani ingawa walikuwa inferior kwa timu ya Hungary (The Golden Team) 1954 (Hakuna mtu angeweza bashiri kwamba Ujerumani ingeshinda) ila hali ya uwanja na advantage ya viatu iliwasaidia.
 
Back
Top Bottom