Jinsi Rais Samia alivyouliza maswali magumu kwenye mkutano wa G20

17 Novemba 2024
Rio de Janeiro, Brazil

MKUTANO WA G20

Majadiliano baina ya rais Prabowo Bertemu wa Indonesia na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. Samia Hassan katika viunga vya mkutano wa G20 Rio de Janeiro

View: https://m.youtube.com/shorts/a7oVC-sVxzE
Yalijikita katika masuala ya nishati na mahusiano baina ya nchi hizo mbili ..

Indonesia, Tanzania zajadili ushirikiano wa nishati, gesi nchini Brazil​

Indonesia, Tanzania zajadili ushirikiano wa nishati, gesi nchini Brazil

Picha ya skrini ya Rais wa Indonesia Prabowo Subianto (kushoto) akikutana na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan huko Rio de Janeiro, Brazil, Jumapili (Novemba 17, 2024)

(Ofisi ya Mawasiliano ya Rais ya ANTARA/HO-Ofisi/ya kwanza)
Jakarta (ANTARA) - Rais wa Indonesia Prabowo Subianto na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan walijadili ushirikiano katika sekta mbalimbali za kimkakati, ikiwa ni pamoja na nishati, mafuta na gesi, Jumapili (Novemba 17), kwa mujibu wa ofisi ya rais wa Indonesia.

Ofisi hiyo pia ilituma picha kwenye Instagram ikiwa na nukuu inayosomeka: "Mkutano wa nchi mbili wa Rais Prabowo Subianto na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Tanzania, kabla ya shughuli za Mkutano wa G20," ilitumwa Jumatatu.

Mkutano huo ulifanyika Rio de Janeiro, Brazil, ofisi iliongeza.

Indonesia na Tanzania zimejitolea kuongeza uwezo wa rasilimali watu kupitia elimu na mafunzo, pamoja na kuharakisha juhudi za uwekaji digitali ili kuleta maendeleo katika nchi zote mbili.

Wakati wa ziara iliyopangwa ya Rais Hassan nchini Indonesia Januari 25, 2024, mataifa hayo mawili pia yalikubaliana kuimarisha ushirikiano katika sekta kadhaa za kimkakati, zikiwemo biashara, uwekezaji, maendeleo ya rasilimali watu, afya na miundombinu.

Hatua moja madhubuti iliyoainishwa katika mkataba huo ni kuanzishwa kwa mazungumzo ya makubaliano ya biashara ya upendeleo (PTA) mwaka wa 2024, yenye lengo la kukuza biashara baina ya nchi hizo mbili.

Zaidi ya hayo, nchi zote mbili zilithibitisha dhamira yao ya kuimarisha ushirikiano katika sekta ya nishati, hasa katika mafuta na gesi, kwa kuhusika na makampuni yanayomilikiwa na serikali ya Indonesia kama vile PT Pertamina na Medco Energi.

Katika sekta ya elimu na mafunzo, Indonesia itasaidia katika kuongeza uwezo wa rasilimali watu wa Tanzania, kwa kuzingatia kilimo na viwanda vya mafuta na gesi.

Kuhusu ushirikiano wa afya, mataifa yote mawili yalikubaliana kuimarisha uhusiano katika sekta ya dawa na kuharakisha mchakato wa usajili wa bidhaa za dawa.

Nchi hizo mbili pia zilisisitiza kuunga mkono hoja ya Palestina na kusisitiza ushiriki wa Tanzania katika Kongamano la Indonesia na Afrika ili kukuza ushirikiano wa Kusini-Kusini.
 
Baada ya maneno yote hayo kuzikoromea nchi tajiri Mheshimiwa Raisi akatoa kitita cha milioni 700 kwa timu ya mpira huku kuna maeneo nchini wanafunzi hawana madarasa.
Shida iko wapi,kwahiyo hatustahili furaha?
 
Indonesia, Tanzania discuss energy, gas cooperation in Brazil

A screenshot of Indonesian President Prabowo Subianto (left) meeting with Tanzanian President Samia Suluhu Hassan in Rio de Janeiro, Brazil, on Sunday (November 17, 2024). (ANTARA/HO-Presidential Communication Office/rst)
Jakarta (ANTARA) - Indonesian President Prabowo Subianto and Tanzanian President Samia Suluhu Hassan discussed cooperation in various strategic sectors, including energy, oil, and gas, on Sunday (November 17), according to the Indonesian president's office.

The office also shared a photo on Instagram with a caption that read: "Bilateral meeting of President Prabowo Subianto with Her Excellency Samia Suluhu Hassan, President of the Republic of Tanzania, ahead of the G20 Summit activities," posted on Monday.

The meeting took place in Rio de Janeiro, Brazil, the office added.

Both Indonesia and Tanzania have committed to enhancing human resource capacity through education and training, as well as accelerating digitalization efforts to drive progress in both countries.

During President Hassan's planned visit to Indonesia on January 25, 2024, the two nations also agreed to deepen cooperation in several strategic sectors, including trade, investment, human resource development, health, and infrastructure.

One concrete step outlined in the agreement is the initiation of negotiations for a preferential trade agreement (PTA) in 2024, aimed at boosting bilateral trade.

Additionally, both countries reaffirmed their commitment to strengthening cooperation in the energy sector, particularly in oil and gas, with involvement from Indonesian state-owned companies such as PT Pertamina and Medco Energi.

In the education and training sectors, Indonesia will assist in enhancing the capacity of Tanzanian human resources, focusing on agriculture and oil and gas industries.

On health cooperation, both nations agreed to strengthen ties in the pharmaceutical sector and expedite the registration process for drug products.

The two countries also reiterated their support for the Palestinian cause and highlighted Tanzania's participation in the Indonesia-Africa Forum to promote South-South cooperation
 
Rais Samia ni mpango wa Mungu Mwenyewe.Huyu Mama ni chaguo la Mungu aliyeinuliwa kwa mkono wa Mungu Mwenyewe
Ukiwa umeshikilia Sinia la Pilau ulilopewa ule lazima useme hivyo yaan pila nyama ya kuku mezani halafu unaambiwa muongelee Rais Dkt. hapo ni kumwaga point za kusifu na kuabudu tu
 
Matonya wa kike!
Wafutiwe madeni ili waishi kifalme?
Ngoja aje Trump ndo atajua hajui!🤣🤣
 
Baada ya maneno yote hayo kuzikoromea nchi tajiri Mheshimiwa Raisi akatoa kitita cha milioni 700 kwa timu ya mpira huku kuna maeneo nchini wanafunzi hawana madarasa.
Kwani hata walimsikiliza basi? Walikuwa wana mchora tu.
 
U
Hivi karibuni Rais Samia Suluhu Hassan ametoa hotuba ya kihistoria kwa kuuliza maswali magumu katika mkutano wa G20, ambapo akiwa anasikilizwa na Rais wa Marekani, Joe Biden, Rais wa China, Xi Jinping, Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer na viongozi wakuu wa nchi hizo 20 tajiri, ametaka dunia kukataa umaskini uliotopea, kumaliza janga la njaa, kuipa Afrika nafasi, kuweka usawa katika upatikanaji wa fedha za maendeleo na kubwa zaidi, amewasilisha ombi la nchi zinazoendelea kufutiwa madeni.

“Natoa shukrani zangu kwa Rais Lula da Silva [wa Brazil] kwa mwaliko na kwa ukarimu wa hali ya juu. Leo hii, tunajikuta katika dunia yenye utajiri mkubwa, lakini bado Afrika inakabiliwa na viwango visivyovumilika vya umasikini, njaa, magonjwa, utapiamlo, na uzalishaji hafifu. Dunia ambamo idadi kubwa ya vijana inakumbwa na changamoto zilizoambatana na migogoro na sera za kimataifa zinazoongeza uhaba wa chakula, kuzorotesha ushindani, na kupunguza fursa za kufikia masoko na teknolojia inayohitajika."

“Dunia ambayo wengi bado wanasubiri ahadi ya utandawazi ya ustawi itimie, huku wakiendelea kuwa na matumaini kwamba mageuzi ya utawala wa kimataifa yatawaletea uwakilishi wa haki na upatikanaji wa rasilimali zinazohitajika kutokomeza umasikini. Hata hivyo, tukiacha dunia kama ilivyo, swali tutakalouliza mwaka 2030 halitakuwa ‘tulikosa kufikia SDGs kwa kiasi gani,’ bali ‘ni watu wangapi zaidi dunia imewaacha nyuma.’

Baada ya kuwaeleza ukweli huo mchungu, Rais Samia akaongeza: “Waheshimiwa, tunaamini kuwa dunia yenye usawa, haki, na endelevu itapatikana pale nchi zinazoendelea kama yangu zitakapopata msaada, rasilimali, na uwakilishi unaohitajika ili kuendesha maendeleo endelevu.

“Licha ya vikwazo vilivyopo, Tanzania imefanikiwa kufanya mageuzi makubwa ya kisera na kitaasisi pamoja na uwekezaji mahsusi ili kubadilisha mifumo yetu ya kilimo na chakula. Kwa kuwa 61.5% ya nguvu kazi yetu ipo kwenye sekta ya kilimo, juhudi zetu zimeongeza kiwango cha ukuaji wa sekta hiyo hadi 4.2%, zimefikisha kiwango cha kujitosheleza kwa chakula hadi 128%, na zimepunguza viwango vya umasikini hadi 26.4% mnamo mwaka 2023.

“Pamoja na mafanikio haya, changamoto bado zipo, zikiwemo uhaba wa mashine, mbolea na utafiti na maendeleo (R&D). Tunaamini kuwa kwa msaada mahsusi, tunaweza kutumia uvumbuzi kwa ufanisi zaidi, kujenga ustahimilivu, na kuwezesha ukuaji wa maana na jumuishi.”

Sitanii, Rais Samia akagusa mfumo wa uchumi duniani: “Maombi yangu mahsusi kwa G20 ni kugawa upya Haki za Kuweka Akiba (SDRs) kwa Taasisi za Kifedha za Afrika kama vile Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB). Pamoja na haja ya mfumo wa usawa wa mgao katika muundo wa sasa wa kifedha wa kimataifa, Tanzania inatoa wito wa kuwepo kwa mifumo zaidi ya msamaha wa madeni, misaada, na mikopo yenye masharti nafuu inayoshughulikia mahitaji yetu na udhaifu wetu.”

Haki za Kuweka Akiba ni mfumo ulioanziswa na Shiria la Fedha Duniani (IMF) mwaka 1969 amba unatambua rasilimali au mali zenye thamani kubwa ambazo huwekwa kama dhamana na kupewa mikopo kwa bei nafuu. Nchi nyingi duniani zilikuwa zinaweka dhahabu kama dhamana na hivyo zinakopesheka kwa riba ndogo, lakini miaka ya karibuni nchi tajiri zimetambua sarafu tano duniani ambazo zinatambulika badala ya dhahabu. Sarafu hizo ni dola za Marekani, Yen ya Japan, Pauni ya Uingereza, Ero ya Ulaya na Renminbi ya China.

Sitanii, ingawa dhahabu si fedha inayoweza kununua kitu, ikitambuliwa kama rasilimali yenye thamani kubwa, Tanzania na nchi nyingine zenye madini ya aina hiyo, zinaweza kupewa mikopo yenye kiwango kidogo ca riba za asilimia 2. Hoja hii ikikubaliwa, ni wazi itazikomboa nchi zinazoendelea kwani zinatumia sehemu kubwa ya makusanyo ya kodi zao kwa ajili ya kulipa madeni, ambayo kiwango kikubwa cha madeni kinatokana na riba.

Rais Samia ameunga mkono ushirikiano ulioimarishwa kama vile Muungano wa Kimataifa wa G20 Dhidi ya Njaa na Umasikini ili kuchochea uvumbuzi na ukuaji jumuishi. “Mkutano huu unadhihirisha dhamira yetu ya pamoja ya kutoiacha dunia kama ilivyo. Tunapaswa kuongeza juhudi zetu na kufufua ahadi zetu za kujenga dunia yenye usawa, ustawi, na haki,” amesema.

Soma pia:
PICHA: Rais Dkt. Samia aelekea Brazil kushiriki mkutano wa G20

Sitanii, mkutano huu wa G20 umempa Rais Samia fursa ya kupiga hatua nyingine katika juhudi zake za kiufungua Tanzania kidiplomasia na kukuza uchumi wa taifa letu. Dunia imezidi kumpa heshima Rais Samia na sasa amekuwa Rais wa kwanza kutoka Tanzania kushiriki mkutano wa mataifa 20 yenye uchumi mkubwa duniani,hapa de Jenairo, Brazil.

Takwimu zinazotolewa na taasisi mbalimbali duniani zinaonyesha kwa sasa uchumi wa dunia una thamani ya dola trilioni 110. Kiuhalisia uchumi wa dunia unashikiliwa na nchi 10 ambazo zinachangia asilimia 76 ya pato la dunia na zinashikilia zaidi ya asilimia 50 ya biashara zinazofanyika duniani. Nchi maskini ikiwamo Tanzania zinashikilia asilimia 8 tu ya biashara ya dunia.

Wanachama wa G20 ni nchi 19 na Umoja wa Ulaya (EU) na Umoja wa Afrika (AU). Ukubwa wa uchumi wa nchi hizi (GDP) kwa mwaka 2024, kwa thamani ya dola za Marekani kwa trilioni (trn), ni kama ifuatavyo:
Marekani (26.7), China (19.37), Ujerumani (4.72), India (4.47), Japan (4.4), Uingereza (3.07), Ufaransa (2.78), Urusi (2.24), Canada (2.14), Italia (2.01), Brazil (1.92), Australia (1.68), Korea Kusini (1.67), Mexico (1.41), Indonesia (1.31), Saudi Arabia (1.1), Uturuki (0.91), Argentina (0.63), Afrika Kusini (0.4). Umoja wa Ulaya unakisiwa kwa ujumla wake kuwa na uchumi wenye thamani ya dola trilioni 16. Afrika takwimu hazitolewi.

Sitanii, mkutano wa G20 ni jukwaa linalojumuisha nchi zilizo na uchumi mkubwa duniani, una faida kubwa kwa Tanzania inaposhiriki kama mwalikwa. Tanzania inapata fursa ya kushiriki mijadala ya kimataifa inayohusu uchumi, maendeleo, biashara na changamoto za dunia kama mabadiliko ya tabianchi na usalama wa chakula.

Kwa ushiriki huu, Rais Samia anaimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na mataifa yenye ushawishi mkubwa duniani. Hii itavutia wawekezaji wakubwa na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi, kijamii na kiteknolojia. Wataalamu wanasema Tanzania itatumia fursa hii kuvutia uwekezaji kwenye miradi ya kimkakati kama kilimo, miundombinu na nishati mbadala.

Kupitia ushiriki huu Tanzania inapata nafasi ya kushawishi ajenda za kikanda na kimataifa zinazoendana na masilahi yake. Kwa mfano, moja ya ajenda inazolenga kupenyezwa ni umuhimu wa usaidizi wa kifedha kwa nchi zinazoendelea, kwa maana ya kupata mikopo yenye masharti nafuu kwa nchi zinazoathiriwa na mabadiliko ya tabianchi na inalenga kuhimiza biashara yenye usawa kwa bidhaa za kilimo na maliasili.

Ushiriki huu unaipa Tanzania nafasi ya kujifunza mbinu bora za kuwaletea wananchi maendeleo kwa kujifunza nchi wanachama wa G20 zilifanikiwaje, ikiwa ni pamoja na sera za kiuchumi na teknolojia za kisasa. Pia inatoa jukwaa la kuonyesha mafanikio yake na kuvutia washirika wa maendeleo.

Kwa kushiriki kama mwalikwa, Tanzania inaongeza nafasi yake ya kushiriki zaidi kwenye uamuzi wa kimataifa, hivyo kuboresha ushawishi wake katika masuala yanayoathiri dunia. Ushiriki huu ni hatua muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na kidiplomasia ya Tanzania.

Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Noel Kaganda, amewaambia wahariri waliopo hapa Rio de Jenairo kuwa mkutano huu unafanyika kwa siku mbili ambazo ni Novemba 18 na 19, mwaka huu.

Tanzania ni moja ya nchi zilizoalikwa na Mwenyekiti wa mhula unaokwisha, Rais wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva. Nchi nyingine 18 zikiwamo Misri, Nigeria, Angola na Msumbiji zimealikwa pia. Hii ni mara ya kwanza katika historia ya G20 kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kualikwa.

Kabla ya G20 kulikuwapo na G8 iliyoasisiwa mwaka 1999, ambayo hadi 2008 ilikuwa na wanachama wanane. Mwaka 2005 aliyekuwa Rais, kwa sasa hayati Benjamin William Mkapa, alishiriki mkutano wa G8 na mwaka 2008, aliyekuwa Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete naye alishiriki. Baada ya hapo zilipoongezeka kuwa G20, ushiriki wa Tanzania ulikoma.

Sitanii, pia Rais Samia anakuwa mwanamke wa kwanza kutoka Afrika kupata fursa ya kushiriki mkutano wa G20. Mkutano huu umetanguliwa na mikutano ya ngazi ya mawaziri, iliyoanza kufanyika tangu Desemba mwaka jana.

Kaulimbiu ya mkutano huu ni kujenga “Dunia yenye haki, usawa na maendeleo endelevu.” Mkutano wa G 20 una vipaumbele vitatu, ambavyo ni:

  1. Ushirikishwaji wa jamii katika mapambano dhidi ya njaa na umaskini (usalama wa chakula).
  2. Mabadiliko ya nishati sambamba na kukuza maendeleo endelevu katika nyanja za uchumi, jamii na mazingira.
  3. Mageuzi ya mifumo ya kiutawala katika taasisi za kimataifa.
Sitanii, vipaumbele hivi vinaakisi kaulimbiu ya mkutano huu, kuondoa umaskini uliokithiri katika Bara la Afrika, ambako zaidi ya watu miioi 600 hawana nishati ya umeme

Pia zaidi ya watu milioni 950 Afrika wanatumia nishati isiyo safi kupikia, kwa maana ya kuni, mkaa, kinyesi cha mifugo na nyingine zenye athari kwenye mazingira, “afya za binadamu,” uchumi na maendeleo, kwani wanatumia muda mwingi kutafuta kuni.

Sitanii, ikumbukwe Rais Samia ndiye kinara wa kuhamasisha Nishati Safi ya Kupikia barani Afrika. Lengo ni kuondoa umaskini na kupunguza madhira kwa kina mama wanaotumia muda mwingi kutafuta kuni na wengine kuishia kubakwa wanapokuwa maporini.

Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025 inalenga kuondoa umaskini na njaa kwa kujenga viwanda. Dira ya Taifa 2050 inaendelea kubeba ajenda nzima ya kumaliza njaa.

Mkutano huu una fursa za uwekezaji, mitaji, kuwapo sauti katika ngazi ya kimataifa kuhamasisha sera zinazosaidia nchi za ulimwengu wa tatu katika kufikia malengo ya kuendeleza watu wake.
Balozi Kaganda anasema ushiriki wa Rais Samia haujatokea kwa bahati mbaya, bali umetokana na kushamiri kwa diplomasia ya Tanzania.

“Kwa sasa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, imeendelea kupokea mialiko mingi sana, ambapo Rais ameshiriki michache, mingine amewatuma wasaidizi wake akiwamo Makamu wa Rais, Dk. Phillip Mpango, Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Naibu Waziri Mkuu, Dk. Doto Biteko. Hii inaashiria kuimarika na kupaa kwa diplomasia ya nchi,” anasema Balozi Kaganda na kuongeza:

“Amekuwa Rais mwenye mvuto, hivyo kuwezesha viongozi wenzake kushiriki. Tanzania inacho cha kuchangia. Tumejipambanua kwenye eneo la nishati, kuzuia njaa, kudai usawa na kuongeza sauti katika mifumo ya utawala – Sirika la Fedha la Kimataifa, Benki ya Dunia, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa… sauti ya Tanzania imekuwa ikisikika. Anachokifanya kinaendana na falsafa yake ya 4R, ambazo ni maridhiano, ustahimilivu, mageuzi na kujenga upya. Hilo ndilo analifanya Rais Samia kimataifa.”

Balozi Kaganda anaamini Rais Samia atatumia mkutano huu kuhamasisha ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia. Mwakani Januari kutakuwa na mkutano wa marais wa Afrika unaoandaliwa na Benki ya Dunia juu ya Nishati Safi ya Kupikia na Tanzania imepewa heshima ya kuandaa mkutano huu.

Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika zenye madini ya kimkakati ambayo yanatumika kutengeneza betri za simu na magari, betri ambazo zinaendesha mitambo na magari, hivyo kuwa mbadala wa mafuta yanayotokana na Kisukusi (fossils) yanayochafua mazingira. Ipo Nikel pale Kabanga, Ngara, na kwa sasa nchi inayo gesi ya kutosha inayoweza kuzalisha LNG.

Tanzania imefanya uwekezaji mkubwa kwenye kilimo, miundombinu na teknolojia zinazoongeza tija na thamani katika eneo hilo la kilimo. Tanzania imefikia asilimia 128 katika uwezo wa kulisha watu wake chakula, hivyo kwa sasa iwekeze katika lishe. Mkutano huu ni mwendelezo wa alama kubwa ambayo Tanzania inaendeleza sasa kwenye anga za diplomasia.

Katika ziara hii, pia Rais wa Tanzania anatarajiwa kukutana na mwenyeji wake Rais wa Brazil, Lula, ambapo watajadili maeneo ya ushirikiano na Brazil kwa maendeleo ya Watanzania.

Tanzania imekuwa mfano wa kuigwa kwa jinsi wananchi walivyofikiwa umeme vijijini na dunia nzima inataka kujifunza Wakala wa Umeme Vijijini (REA) umewezaje kufanya kazi hii kwa ufanisi mkubwa kiasi hiki.

Mwakani kiti cha G20 kinahamia nchini Afrika Kusini, hali inayoaminiwa kuwa Afrika itakuwa na sauti kubwa zaidi. Brazil inatarajiwa kuwasilisha Azimio la Usalama wa Chakula ambapo Tanzania imesema italiunga mkono azimio hili na Uingereza inataka kuanzisha ushirika wa nishati duniani (Global Power Alliance), suala ambalo Balozi Kaganda amesema Tanzania italiunga mkono pia.

Source: Jamhuri Media
Imeandikwa na: Deodatus Balile
Ungeweka hotuba Kama ilivyo bila kuongeza mbwembe zako za kichawa ingependeza

Pia naona Kama Risala vile
 
Picha ya skrini ya Rais wa Indonesia Prabowo Subianto (kushoto) akikutana na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan huko Rio de Janeiro, Brazil, Jumapili (Novemba 17, 2024)

(Ofisi ya Mawasiliano ya Rais ya ANTARA/HO-Ofisi/ya kwanza)
Jakarta (ANTARA) - Rais wa Indonesia Prabowo Subianto na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan walijadili ushirikiano katika sekta mbalimbali za kimkakati, ikiwa ni pamoja na nishati, mafuta

22 November 2024

MAFANIKIO YA SAFARI YA RIO DE JANEIRO BRAZIL MKUTANO WA G20

View: https://m.youtube.com/watch?v=VgoiEZegnz8
 
Rio de Janeiro, Brazil

Katika mkutano wa G20 Brazil waziri mkuu wa Vietnam Mh. Pham Minh Chinh na rais wa Tanzania Mh. Dr. Samia Hassan walipata wasaa wa kufanya mazungumzo kuhusu mahusiano ya kiuchumi na TEHAMA
1732308199333.jpeg

Prime Minister Pham Minh Chinh meeting with president of Tanzania H.E Samia Hassan. The prime minister also held separate meetings with other world leaders and leaders of organisations in Rio de Janeiro on November 18 afternoon (local time) on the occasion of his attendance at the G20 Summit and bilateral activities in Brazil. VNA Photo: Dương Giang
 
Siasa mbali , Huyu mama ni kichwa kweli na anaing'arisha Tanzania kwenye jumuia ya madola
 
G20 Social Jamii inazindua wito wa kimataifa wa dunia jumuishi, demokrasia na mageuzi ya utawala​

Azimio la Rio de Janeiro, linalotokana na G20 Social, linakuza matakwa ya harakati za kijamii kwa ajili ya haki ya kimataifa, mapambano dhidi ya njaa na mabadiliko ya hali ya hewa, na mageuzi ya haraka ya utawala wa kimataifa. Tukio hilo linakamilika Jumamosi hii, kabla ya mkutano wa viongozi hao wiki ijayo.

1732309106188.jpeg

Rais Samia Hassan asema masuala ya utawala bora, jumuishi pia yaligusiwa katika mkutano wa G20 Rio de Janeiro Brazil ingawa ni mataifa ya G20 ndiyo yalizungumza huku nchi waalikwa kama Tanzania n.k zilikuwa wasikikizaji. Hayo yamebainika katika mkutano wa Rais Hassan na wahariri waandishi wa habari
Na Leandro Molina/Tovuti G20
Kufungwa kwa G20 Social kuliwekwa alama kwa hotuba zenye msisitizo na uwasilishaji wa Azimio la Rio de Janeiro, hati iliyotayarishwa kwa ushirikiano na vuguvugu la kijamii kutoka kote ulimwenguni. Hafla hiyo, iliyofanyika pamoja na shughuli za G20, ilisisitiza udharura wa kufanya mageuzi ya utawala wa kimataifa ili kushughulikia changamoto za kisasa kama vile mabadiliko ya hali ya hewa, ukosefu wa usawa wa kijamii, na migogoro ya kijiografia. Oliver Röpke, rais wa Kamati ya Uchumi na Kijamii ya Ulaya, alielekeza fikira kwenye hitaji la kupigana na ukosefu wa usawa ili kuunda wakati ujao wenye haki zaidi. "Tuko katika njia panda. Jeshi la kimataifa linakabiliwa na mgogoro ambapo mifumo ya utawala haitumiki tena wakati wetu. Tunahitaji marekebisho ya kimuundo kujumuisha jumuiya za kiraia na kuimarisha jumuiya ya kimataifa kwa ukuaji jumuishi na kulinda haki za kijamii," alisema. Kwake, G20 Social inapaswa kuwa mfano wa kimataifa, kuonyesha kwamba inawezekana kuunda ulimwengu unaosikiliza matarajio ya idadi ya watu
 
Hivi karibuni Rais Samia Suluhu Hassan ametoa hotuba ya kihistoria kwa kuuliza maswali magumu katika mkutano wa G20, ambapo akiwa anasikilizwa na Rais wa Marekani, Joe Biden, Rais wa China, Xi Jinping, Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer na viongozi wakuu wa nchi hizo 20 tajiri, ametaka dunia kukataa umaskini uliotopea, kumaliza janga la njaa, kuipa Afrika nafasi, kuweka usawa katika upatikanaji wa fedha za maendeleo na kubwa zaidi, amewasilisha ombi la nchi zinazoendelea kufutiwa madeni.

“Natoa shukrani zangu kwa Rais Lula da Silva [wa Brazil] kwa mwaliko na kwa ukarimu wa hali ya juu. Leo hii, tunajikuta katika dunia yenye utajiri mkubwa, lakini bado Afrika inakabiliwa na viwango visivyovumilika vya umasikini, njaa, magonjwa, utapiamlo, na uzalishaji hafifu. Dunia ambamo idadi kubwa ya vijana inakumbwa na changamoto zilizoambatana na migogoro na sera za kimataifa zinazoongeza uhaba wa chakula, kuzorotesha ushindani, na kupunguza fursa za kufikia masoko na teknolojia inayohitajika."

“Dunia ambayo wengi bado wanasubiri ahadi ya utandawazi ya ustawi itimie, huku wakiendelea kuwa na matumaini kwamba mageuzi ya utawala wa kimataifa yatawaletea uwakilishi wa haki na upatikanaji wa rasilimali zinazohitajika kutokomeza umasikini. Hata hivyo, tukiacha dunia kama ilivyo, swali tutakalouliza mwaka 2030 halitakuwa ‘tulikosa kufikia SDGs kwa kiasi gani,’ bali ‘ni watu wangapi zaidi dunia imewaacha nyuma.’

Baada ya kuwaeleza ukweli huo mchungu, Rais Samia akaongeza: “Waheshimiwa, tunaamini kuwa dunia yenye usawa, haki, na endelevu itapatikana pale nchi zinazoendelea kama yangu zitakapopata msaada, rasilimali, na uwakilishi unaohitajika ili kuendesha maendeleo endelevu.

“Licha ya vikwazo vilivyopo, Tanzania imefanikiwa kufanya mageuzi makubwa ya kisera na kitaasisi pamoja na uwekezaji mahsusi ili kubadilisha mifumo yetu ya kilimo na chakula. Kwa kuwa 61.5% ya nguvu kazi yetu ipo kwenye sekta ya kilimo, juhudi zetu zimeongeza kiwango cha ukuaji wa sekta hiyo hadi 4.2%, zimefikisha kiwango cha kujitosheleza kwa chakula hadi 128%, na zimepunguza viwango vya umasikini hadi 26.4% mnamo mwaka 2023.

“Pamoja na mafanikio haya, changamoto bado zipo, zikiwemo uhaba wa mashine, mbolea na utafiti na maendeleo (R&D). Tunaamini kuwa kwa msaada mahsusi, tunaweza kutumia uvumbuzi kwa ufanisi zaidi, kujenga ustahimilivu, na kuwezesha ukuaji wa maana na jumuishi.”

Sitanii, Rais Samia akagusa mfumo wa uchumi duniani: “Maombi yangu mahsusi kwa G20 ni kugawa upya Haki za Kuweka Akiba (SDRs) kwa Taasisi za Kifedha za Afrika kama vile Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB). Pamoja na haja ya mfumo wa usawa wa mgao katika muundo wa sasa wa kifedha wa kimataifa, Tanzania inatoa wito wa kuwepo kwa mifumo zaidi ya msamaha wa madeni, misaada, na mikopo yenye masharti nafuu inayoshughulikia mahitaji yetu na udhaifu wetu.”

Haki za Kuweka Akiba ni mfumo ulioanziswa na Shiria la Fedha Duniani (IMF) mwaka 1969 amba unatambua rasilimali au mali zenye thamani kubwa ambazo huwekwa kama dhamana na kupewa mikopo kwa bei nafuu. Nchi nyingi duniani zilikuwa zinaweka dhahabu kama dhamana na hivyo zinakopesheka kwa riba ndogo, lakini miaka ya karibuni nchi tajiri zimetambua sarafu tano duniani ambazo zinatambulika badala ya dhahabu. Sarafu hizo ni dola za Marekani, Yen ya Japan, Pauni ya Uingereza, Ero ya Ulaya na Renminbi ya China.

Sitanii, ingawa dhahabu si fedha inayoweza kununua kitu, ikitambuliwa kama rasilimali yenye thamani kubwa, Tanzania na nchi nyingine zenye madini ya aina hiyo, zinaweza kupewa mikopo yenye kiwango kidogo ca riba za asilimia 2. Hoja hii ikikubaliwa, ni wazi itazikomboa nchi zinazoendelea kwani zinatumia sehemu kubwa ya makusanyo ya kodi zao kwa ajili ya kulipa madeni, ambayo kiwango kikubwa cha madeni kinatokana na riba.

Rais Samia ameunga mkono ushirikiano ulioimarishwa kama vile Muungano wa Kimataifa wa G20 Dhidi ya Njaa na Umasikini ili kuchochea uvumbuzi na ukuaji jumuishi. “Mkutano huu unadhihirisha dhamira yetu ya pamoja ya kutoiacha dunia kama ilivyo. Tunapaswa kuongeza juhudi zetu na kufufua ahadi zetu za kujenga dunia yenye usawa, ustawi, na haki,” amesema.

Soma pia:
PICHA: Rais Dkt. Samia aelekea Brazil kushiriki mkutano wa G20

Sitanii, mkutano huu wa G20 umempa Rais Samia fursa ya kupiga hatua nyingine katika juhudi zake za kiufungua Tanzania kidiplomasia na kukuza uchumi wa taifa letu. Dunia imezidi kumpa heshima Rais Samia na sasa amekuwa Rais wa kwanza kutoka Tanzania kushiriki mkutano wa mataifa 20 yenye uchumi mkubwa duniani,hapa de Jenairo, Brazil.

Takwimu zinazotolewa na taasisi mbalimbali duniani zinaonyesha kwa sasa uchumi wa dunia una thamani ya dola trilioni 110. Kiuhalisia uchumi wa dunia unashikiliwa na nchi 10 ambazo zinachangia asilimia 76 ya pato la dunia na zinashikilia zaidi ya asilimia 50 ya biashara zinazofanyika duniani. Nchi maskini ikiwamo Tanzania zinashikilia asilimia 8 tu ya biashara ya dunia.

Wanachama wa G20 ni nchi 19 na Umoja wa Ulaya (EU) na Umoja wa Afrika (AU). Ukubwa wa uchumi wa nchi hizi (GDP) kwa mwaka 2024, kwa thamani ya dola za Marekani kwa trilioni (trn), ni kama ifuatavyo:
Marekani (26.7), China (19.37), Ujerumani (4.72), India (4.47), Japan (4.4), Uingereza (3.07), Ufaransa (2.78), Urusi (2.24), Canada (2.14), Italia (2.01), Brazil (1.92), Australia (1.68), Korea Kusini (1.67), Mexico (1.41), Indonesia (1.31), Saudi Arabia (1.1), Uturuki (0.91), Argentina (0.63), Afrika Kusini (0.4). Umoja wa Ulaya unakisiwa kwa ujumla wake kuwa na uchumi wenye thamani ya dola trilioni 16. Afrika takwimu hazitolewi.

Sitanii, mkutano wa G20 ni jukwaa linalojumuisha nchi zilizo na uchumi mkubwa duniani, una faida kubwa kwa Tanzania inaposhiriki kama mwalikwa. Tanzania inapata fursa ya kushiriki mijadala ya kimataifa inayohusu uchumi, maendeleo, biashara na changamoto za dunia kama mabadiliko ya tabianchi na usalama wa chakula.

Kwa ushiriki huu, Rais Samia anaimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na mataifa yenye ushawishi mkubwa duniani. Hii itavutia wawekezaji wakubwa na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi, kijamii na kiteknolojia. Wataalamu wanasema Tanzania itatumia fursa hii kuvutia uwekezaji kwenye miradi ya kimkakati kama kilimo, miundombinu na nishati mbadala.

Kupitia ushiriki huu Tanzania inapata nafasi ya kushawishi ajenda za kikanda na kimataifa zinazoendana na masilahi yake. Kwa mfano, moja ya ajenda inazolenga kupenyezwa ni umuhimu wa usaidizi wa kifedha kwa nchi zinazoendelea, kwa maana ya kupata mikopo yenye masharti nafuu kwa nchi zinazoathiriwa na mabadiliko ya tabianchi na inalenga kuhimiza biashara yenye usawa kwa bidhaa za kilimo na maliasili.

Ushiriki huu unaipa Tanzania nafasi ya kujifunza mbinu bora za kuwaletea wananchi maendeleo kwa kujifunza nchi wanachama wa G20 zilifanikiwaje, ikiwa ni pamoja na sera za kiuchumi na teknolojia za kisasa. Pia inatoa jukwaa la kuonyesha mafanikio yake na kuvutia washirika wa maendeleo.

Kwa kushiriki kama mwalikwa, Tanzania inaongeza nafasi yake ya kushiriki zaidi kwenye uamuzi wa kimataifa, hivyo kuboresha ushawishi wake katika masuala yanayoathiri dunia. Ushiriki huu ni hatua muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na kidiplomasia ya Tanzania.

Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Noel Kaganda, amewaambia wahariri waliopo hapa Rio de Jenairo kuwa mkutano huu unafanyika kwa siku mbili ambazo ni Novemba 18 na 19, mwaka huu.

Tanzania ni moja ya nchi zilizoalikwa na Mwenyekiti wa mhula unaokwisha, Rais wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva. Nchi nyingine 18 zikiwamo Misri, Nigeria, Angola na Msumbiji zimealikwa pia. Hii ni mara ya kwanza katika historia ya G20 kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kualikwa.

Kabla ya G20 kulikuwapo na G8 iliyoasisiwa mwaka 1999, ambayo hadi 2008 ilikuwa na wanachama wanane. Mwaka 2005 aliyekuwa Rais, kwa sasa hayati Benjamin William Mkapa, alishiriki mkutano wa G8 na mwaka 2008, aliyekuwa Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete naye alishiriki. Baada ya hapo zilipoongezeka kuwa G20, ushiriki wa Tanzania ulikoma.

Sitanii, pia Rais Samia anakuwa mwanamke wa kwanza kutoka Afrika kupata fursa ya kushiriki mkutano wa G20. Mkutano huu umetanguliwa na mikutano ya ngazi ya mawaziri, iliyoanza kufanyika tangu Desemba mwaka jana.

Kaulimbiu ya mkutano huu ni kujenga “Dunia yenye haki, usawa na maendeleo endelevu.” Mkutano wa G 20 una vipaumbele vitatu, ambavyo ni:

  1. Ushirikishwaji wa jamii katika mapambano dhidi ya njaa na umaskini (usalama wa chakula).
  2. Mabadiliko ya nishati sambamba na kukuza maendeleo endelevu katika nyanja za uchumi, jamii na mazingira.
  3. Mageuzi ya mifumo ya kiutawala katika taasisi za kimataifa.
Sitanii, vipaumbele hivi vinaakisi kaulimbiu ya mkutano huu, kuondoa umaskini uliokithiri katika Bara la Afrika, ambako zaidi ya watu miioi 600 hawana nishati ya umeme

Pia zaidi ya watu milioni 950 Afrika wanatumia nishati isiyo safi kupikia, kwa maana ya kuni, mkaa, kinyesi cha mifugo na nyingine zenye athari kwenye mazingira, “afya za binadamu,” uchumi na maendeleo, kwani wanatumia muda mwingi kutafuta kuni.

Sitanii, ikumbukwe Rais Samia ndiye kinara wa kuhamasisha Nishati Safi ya Kupikia barani Afrika. Lengo ni kuondoa umaskini na kupunguza madhira kwa kina mama wanaotumia muda mwingi kutafuta kuni na wengine kuishia kubakwa wanapokuwa maporini.

Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025 inalenga kuondoa umaskini na njaa kwa kujenga viwanda. Dira ya Taifa 2050 inaendelea kubeba ajenda nzima ya kumaliza njaa.

Mkutano huu una fursa za uwekezaji, mitaji, kuwapo sauti katika ngazi ya kimataifa kuhamasisha sera zinazosaidia nchi za ulimwengu wa tatu katika kufikia malengo ya kuendeleza watu wake.
Balozi Kaganda anasema ushiriki wa Rais Samia haujatokea kwa bahati mbaya, bali umetokana na kushamiri kwa diplomasia ya Tanzania.

“Kwa sasa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, imeendelea kupokea mialiko mingi sana, ambapo Rais ameshiriki michache, mingine amewatuma wasaidizi wake akiwamo Makamu wa Rais, Dk. Phillip Mpango, Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Naibu Waziri Mkuu, Dk. Doto Biteko. Hii inaashiria kuimarika na kupaa kwa diplomasia ya nchi,” anasema Balozi Kaganda na kuongeza:

“Amekuwa Rais mwenye mvuto, hivyo kuwezesha viongozi wenzake kushiriki. Tanzania inacho cha kuchangia. Tumejipambanua kwenye eneo la nishati, kuzuia njaa, kudai usawa na kuongeza sauti katika mifumo ya utawala – Sirika la Fedha la Kimataifa, Benki ya Dunia, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa… sauti ya Tanzania imekuwa ikisikika. Anachokifanya kinaendana na falsafa yake ya 4R, ambazo ni maridhiano, ustahimilivu, mageuzi na kujenga upya. Hilo ndilo analifanya Rais Samia kimataifa.”

Balozi Kaganda anaamini Rais Samia atatumia mkutano huu kuhamasisha ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia. Mwakani Januari kutakuwa na mkutano wa marais wa Afrika unaoandaliwa na Benki ya Dunia juu ya Nishati Safi ya Kupikia na Tanzania imepewa heshima ya kuandaa mkutano huu.

Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika zenye madini ya kimkakati ambayo yanatumika kutengeneza betri za simu na magari, betri ambazo zinaendesha mitambo na magari, hivyo kuwa mbadala wa mafuta yanayotokana na Kisukusi (fossils) yanayochafua mazingira. Ipo Nikel pale Kabanga, Ngara, na kwa sasa nchi inayo gesi ya kutosha inayoweza kuzalisha LNG.

Tanzania imefanya uwekezaji mkubwa kwenye kilimo, miundombinu na teknolojia zinazoongeza tija na thamani katika eneo hilo la kilimo. Tanzania imefikia asilimia 128 katika uwezo wa kulisha watu wake chakula, hivyo kwa sasa iwekeze katika lishe. Mkutano huu ni mwendelezo wa alama kubwa ambayo Tanzania inaendeleza sasa kwenye anga za diplomasia.

Katika ziara hii, pia Rais wa Tanzania anatarajiwa kukutana na mwenyeji wake Rais wa Brazil, Lula, ambapo watajadili maeneo ya ushirikiano na Brazil kwa maendeleo ya Watanzania.

Tanzania imekuwa mfano wa kuigwa kwa jinsi wananchi walivyofikiwa umeme vijijini na dunia nzima inataka kujifunza Wakala wa Umeme Vijijini (REA) umewezaje kufanya kazi hii kwa ufanisi mkubwa kiasi hiki.

Mwakani kiti cha G20 kinahamia nchini Afrika Kusini, hali inayoaminiwa kuwa Afrika itakuwa na sauti kubwa zaidi. Brazil inatarajiwa kuwasilisha Azimio la Usalama wa Chakula ambapo Tanzania imesema italiunga mkono azimio hili na Uingereza inataka kuanzisha ushirika wa nishati duniani (Global Power Alliance), suala ambalo Balozi Kaganda amesema Tanzania italiunga mkono pia.

Source: Jamhuri Media
Imeandikwa na: Deodatus Balile
Wenda ikawa hotuba ya kihistoria ,ila elewa wenzetu wako mbali sana , hotuba kwao ni vitu minor sana mkuu, yaani mtu anaumiza kichwa na migogoro ya nchi washirika alafu , awe based na hotuba toka tz ,hujui dunia , wengine wanaenda kwenye vikao kama hivi wakifocus next,usichukulie poa
 
Kuomba kusamehewa madeni daaa yaaani wamejazana Kwenye dege alilonunua mwenzao
 
Usitudanganye hakuuliza maswali, alienda kutuombea wadanganyika misaada. Maswali aliyouliza yako wapi?
 
Back
Top Bottom