Jinsi Rais Samia alivyouliza maswali magumu kwenye mkutano wa G20

Acheni kumsanifu. Aulize maswali magumu kwa kichwa gani? Kama ingekuwa mipasho, huenda ningewaamini. Hakuna swali lolote alilojibu tukiwa wakweli na kuacha uchawa
 
Sitanii imekaa kichawa sana
 
Bila JPM wangepanda sijui ungo
Mkuu wange panda, na wengfika na kurudi tu. Usimkuze Magufuli kama vile bila yeye kila kitu kingesimama Tanzania .

Mbona maisha yanaendelea bila uwepo wake!!!
 
Baada ya maneno yote hayo kuzikoromea nchi tajiri Mheshimiwa Raisi akatoa kitita cha milioni 700 kwa timu ya mpira huku kuna maeneo nchini wanafunzi hawana madarasa.
Wakuu wa mikoa na wilaya wanafanya kazi gani?. Mabilioni ya pesa yanatolewa na hazina kwa ajili ya maendeleo kila siku, wa kuhojiwa juu ya hayo madarasa wanajulikana na wafuatwe hao hao.

Kati ya mataifa 54 ya afrika timu zinazofuzu ni 24, kwa Taifa Stars kuwepo miongoni mwa timu hizo 24 kuna kazi nzito imefanyika na naamini hiyo milioni 700 ni haki kabisa kuwafikia wachezaji.

Tatizo letu wabongo akili nyingi za kishamba zinatusumbua, Hollywood Marekani kina Tom Cruise kule Hollywood anaishi kwenye jumba lenye thamani ya dola milioni 50 wakati hapo hapo Los Angeles kuna maelfu ya watu wanaoishi kwenye nyumba za maboksi.

Kwanini Cruise asiuze jumba lake ili hiyo pesa iweze kusaidia katika kuondoa ombaomba mitaani?.
 
Nasikia walikuwa hata hawamsikilizi walikuwa bize na kupakua chakula!....utawauloza maswali magumu watu unaowaomba wakusaidie!?nonsense
 
Swali gani gumu hapo ? Mbona nadhani hapo angeweza kuwapa majibu na mbaya zaidi naona amejisifia tu alichofanya (which means ni kama anasema kwamba hata mambo yakiwa hivyo bado tunaweza kufanya kwamba the onus is on us)
Alichofanya hapo kinaitwa Blowing ones own Trumpet (by cooking data I might add)
“Licha ya vikwazo vilivyopo, Tanzania imefanikiwa kufanya mageuzi makubwa ya kisera na kitaasisi pamoja na uwekezaji mahsusi ili kubadilisha mifumo yetu ya kilimo na chakula. Kwa kuwa 61.5% ya nguvu kazi yetu ipo kwenye sekta ya kilimo, juhudi zetu zimeongeza kiwango cha ukuaji wa sekta hiyo hadi 4.2%, zimefikisha kiwango cha kujitosheleza kwa chakula hadi 128%, na zimepunguza viwango vya umasikini hadi 26.4% mnamo mwaka 2023.

Na baada ya hapo kama kawaida ni mwendo wa kuomba msaada

“Pamoja na mafanikio haya, changamoto bado zipo, zikiwemo uhaba wa mashine, mbolea na utafiti na maendeleo (R&D). Tunaamini kuwa kwa msaada mahsusi, tunaweza kutumia uvumbuzi kwa ufanisi zaidi, kujenga ustahimilivu, na kuwezesha ukuaji wa maana na jumuishi.”
Ingawa binafsi nasema shida ni viongozi wetu na hivi sasa wana mentality za kwamba hakuna tunachoweza


Kwahio kuliko kwenda kudai haki wewe Kondoo kwa Fisi..., no bora nyie Kondoo mgaungana na kufanya maendeleo yenu...

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…