King Jim
Member
- Aug 12, 2024
- 6
- 16
JINSI SHULE INAVYOHARIBU UBAADAE WA WATOTO WA KI-AFRIKA.
Tafadhari soma hii ukiwa umekwisha graduate 🎓,
Kabla hatujaendelea, naomba nikuweke sawa kwenye maneno Shule na Elimu,
Elimu (Knowledge/Wisdom) ndio muhimu kwenye maisha ya mwanadamu na sio Shule ambayo ipo ndio kama mfumo wa Elimu wa sasa japo wanakosea kuuita hivyo.
1. Shule ilianzishwa na matajiri wa Ulaya ambao walikuwa kwenye wakati ambao madili ya viwanda yalibamba na hivyo hitaji la wafanyakazi likawafanya wabuni njia ya kuwapa ujuzi hao wafanyakazi na namna ya wao kuwa bora, ndipo SHULE zikaanza,
Lakini Elimu iliumbwa na Mungu mwenyewe
Kwa wakati huo shule ilisaidia sana, kwani ukisoma unauwakika wa mkono kwenda kinywani lakini sio kwa sasa.
Nabepari wakawa wajanja haswa kwa kubuni mfumo utakao wafanya wafanyakazi wawe watiifu kwa mabosi wao na wahofie kufanya makosa, hivyo vyote vinafundishwa shule mpaka leo. Tena wakahakikisha kuwa hao masikini wasomi wasije kuwa Matajiri kama wao kwa kuwa-program wakiwa shuleni ili kulinda matabaka yaliyopo na ndio maana nimekuja kukuandikia uzi huu.
Kwani kabla ya Shule hazijaanza Elimu ilipatikanaje?
Yesu alikuwa na Elimu ndio maana aliitwa Rabi au mwalimu na hukuwahi kwenda shule.
Je wale Ma-Engineer walio design na kujenga mnara wa babeli walisoma wapi? Vipi hekalu la suleimani? Au vipi yale ma Pyramids ya Misri? Je nao walienda shuleni kama sisi?
Jim Rohn anasema "Elimu ni kile unachobakiwa nacho baada ya kusahau kile ulichofundishwa shuleni" maanake chote unachofundishwa shuleni si Elimu japo wanakuamisha kuwa ni Elimu
Mbona madaktari wetu wa tiba asili hawakuhitaji shule?
2. Shuleni tulifundishwa kuwa Nidhamu ni utii, lakini Mabepari wanajua wazi kuwa Nidhamu ni uwezo wa kuchagua kati ya kitu unachokitaka sana mbele ya kitu kilichopo sahizi (kama hujaelewa unaweza nifata inbox nikuweke sawa) na sio lazima uwe mtii ili ufanikiwe, bali Wanakufundisha utii ili uwe kibaraka mzuri ukiisha ajiriwa ndio maana unafundishwa kutii bila shuruti, eti hadi viranjai wa shuleni hahaha, kuna mahali tanachezewa.
Wote waliofanikiwa hawakuwa watii kwenye maisha yao kwani kuwa mtii ni kukubali kufanyiwa maamuzi bila kujiongeza.
Zamani shule ilikuhakikishia ajira na maisha mazuri, nisingeweza ipinga kwani mabenki yaliweza kuajiri watu hadi 30,000 kwa kuwa Technology haikuwa kubwa lakini si sahizi ambapo kuna ATM's na Uwezo wa kufanya miamala kwa simu, eti ni Benki gani itaajili wafanyakazi 200 tena?
Hivyo shule imeshindwa kutuhakikishia uwakika wa ajira kwanini tusihamie kwenye Enterprenuership? Bado Waafrika wengi hatujiajili kwasababu anayetufundisha shuleni tukajiajiri naye kaajiriwa 🤦‍♂️ na hajui chochote kuhusu ujasiriamali zaidi ya kusoma notes tu pasi na kuzifanyia kazi,
4. Shule inatupotezea sana muda vijana wa kiafrika, tunaenda shule tukiwa na miaka 3-5 ila tunatoka tukiwa na 23-26/7. Umri huo ukitoka inabidi utafute tu kazi ili uweze kuishi mana kuendelea kujitafuta ni kama kupoteza muda zaidi ndio maana tunashindwa kuwa ma MoDewji au J Bezos au kama Elon Musk?
5. Shuleni tunachapwa tukikosea na kuaminishwa kufeli ni kushindwa lakini uhalisia wa maisha haupo hivyo, makosa ndio yamezalisha majina yote makubwa dunia kwenye wakati huu na wakati uliopita maana maisha sio kupata vyote, ni lazima kukosa pia maishani.
Sipingani na Elimu ya kusoma, kuandika na kuhesabu, hivyo ni lazima kila mtu ajue na havijaanzishwa na shule maana toka kipindi cha mitume na manabii watu walikuwa wanahesabu, na kuandika tu kama sasa, hiyo ndio sehemu pekee shule imeweze kubadilisha maisha yangu pia.
7. Shule inaua vipaji na ujuzi mbalimbali kwa kutuaminisha kuwa njia pekee ya kufanikiwa maishani ni kwa kuwa na taaluma fulani tu lakini maisha yanatufundisha kuwa kuna aina nyingi sana za Intelligence ambazo hazihusiani na kufaulu mitihani. Zipo kwenye picha unaweza jisomea 👇
Kama bado unabisha, basi chagua daktari mmoja kati ya hawa👇
â—ŹDakari John (28), muhitimu wa chuo cha Afya maarufu nchini kwako.
â—ŹDaktari Gwaba(28) aliyefundishwa na babu yake toka akiwa na miaka 12 tiba za asili, haitaji mashine kujua mapigo yako ya moyo wala sumu inayokutesa
Lengo la kuandika nikukuaminisha wewe kijana uliyekosa nafasi ya kusoma kwamba hakuna ulichopoteza bali nyote mnanafasi sawa maishani na si ajabu wewe ukatoboa wa kwanza kuliko wasomi wengi.
Ndio maana bado ndoto za watoto wetu ni kuwa kama CR7, Messi au Chibu na sio kuwa Prof Assad au Dr Mwaka.