Jinsi siasa za Tanzania zinavyodidimiza ustawi wa vijana

Jinsi siasa za Tanzania zinavyodidimiza ustawi wa vijana

kaligopelelo

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2013
Posts
2,832
Reaction score
4,070
Ndugu zanguni,

Hawa wanasiasa hawana nia njema na watu wa kawaida hata siku moja. Siku zote mwanasiasa anaanza kuangalia masilahi yake binafsi then atawaangalia jamaa zake wa karibu,ndugu na marafiki.

Ndiyo,lazima niseme hivyo...hatuna kiongozi wa kisiasa aliyepita,aliyopo madarakani wala ajaye mwenye nia ya dhati ya kuwakomboa Watanzania kiuchumi na kijamii. Hawa wote siasa waneifanya kuwa ni kazi na ni sehemu pekee inayomfanya mtu akamate fursa za kutoboa kiuchumi.

Sasa hawa wanasiasa mtaji wao mkubwa ni watu,na wenyewe wanajua matatizo yanayowakabili hao watu na ndio maana wakati wa kuomba kura wao wenyewe wanayaorodhesha matatizo yetu bila kuambiwa. Wanayajua matatizo yetu na ndio maana wanaweka ahadi ya kuyatatua ila tukishawachagua matatizo yetu wanajifanya hawayajui tena.

Nikiwa kama kijana baada ya kumaliza masomo yangu niliamua kujiajiri baada ya kufahamu changamoto ya ajira mjini kuwa janga la kitaifa. Ukiacha elimu yangu ya kukariri,mimi ni mtoto wa mkulima na kilimo ni kitu pekee nimejifunza Kwa matendo kupitia mikono ya wazazi wangu.

Ule mwaka wa kwanza nikaingia kwenye kilimo Cha mahindi na mbaazi, nilikuwa na mtaji kidogo ambao nilijibana nikiwa ninasoma. Niliamua kuwekeza laki tano kati ya million moja niliyokuwa nayo kwenye kilimo hicho. Kuja msimu wa mavuno mazao yetu yakakosa masoko na zile mbaazi zikakosa mnunuzi kabisa. Siasa zetu za ndani zilichangia kupoteza mnunuzi wa mazao yetu ikiwemo pamoja na zao la mbaazi.

Mwaka Jana nikaingia kwenye kilimo Cha korosho. Nilipambana Kwa jasho Kwa kiasi kikubwa Kwa lengo la kutaka kujikomboa kiuchumi. Zao la korosho ni zao linalohitaji uwe na mtaji mkubwa sana kutokana na zile gharama zake za uendeshaji kuwa juu. Baada ya mavuno soko halikuwa zuri kutokana na usimamizi mbovu,njama na hila za baadhi ya watu waliopewa mamlaka ya kusimamia zao hili.

Nikagundua kuwa hizi bado zilizoundwa kusimamia mazao haya na vyama vya ushirika vimejaa udalali mkubwa wa mazao,rushwa na kuwahujumu wakulima kiuchumi. Lakini pia wanasiasa hawa Kama viongozi wameweka mirija mikubwa Sana hasa kwenye zao la korosho kiasi kwamba pato la mkulima linashushwa kutoka na hiyo mirija ya ushuru,Kodi na Tozo mbalimbali.

Nchi hii ukitaka kufa masikini jiajiri kwenye kilimo. Mimi kama kijana nilitamani siku moja sera za kilimo nchini zikibadirika Ili ziweze kumnufaisha Kila mtanzania. Ziko wapi zile kauli mbiu za kuwa KILIMO NI UTI WA MGONGO WA TAIFA.
Au hizi kauli zina tafsirika Kwa mlango wa nyuma? Kwamba Wajinga ndio waliwao?

Iko wapi thamani ya vijana Kwa taifa hili?

Nguvu zetu zinapotea bure kwanini?

Mkombozi wetu sisi ni nani?

Wanasiasa kwanini mnaangalia masilahi yenu peke yenu? Kwanini hamtuhamasishi tusio na ajira kufurahia maisha kupitia upande tuliouchagua?

eb2a959adb4548c5120675e8bb1ac70b.png
 
Kila mtu ana bosi wake, anaweza kuwepo mwenye maono mazuri ila akashindwa kutekeleza kutokana na mazingira, mwisho wa siku naye akawa mbinafsi
 
Kila mtu ana bosi wake, anaweza kuwepo mwenye maono mazuri ila akashindwa kutekeleza kutokana na mazingira, mwisho wa siku naye akawa mbinafsi
Kama ana maono mazuri akayaacha au kushindwa kumshauri vizuri bosi wake naye akafuata njia ile ile ya kidhalimu,pasi na shaka huyo naye ni mchumia tumbo tu kama ilivyo Kwa wengine. Wanasiasa wote ni dhulumati.
 
Kama ana maono mazuri akayaacha au kushindwa kumshauri vizuri bosi wake naye akafuata njia ile ile ya kidhalimu,pasi na shaka huyo naye ni mchumia tumbo tu kama ilivyo Kwa wengine. Wanasiasa wote ni dhulumati.
Wanaosimamia kile wanachokiamini ni wachache sana, na kwa Afrika ni ngumu kuwepo; kwa wenzetu huko nje, huwa wanajiuzuru kulinda kile wanachokiamini.
 
Mtaji wa wana siasa ni kundi la wajinga, mtaji wa wanasiasa wa Afrika [ Tanzania ] ni kundi kubwa la wajinga Watanzania.
 
Back
Top Bottom