Jinsi siku yangu ilivyoharibika

Jinsi siku yangu ilivyoharibika

Gol D Roger

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2023
Posts
2,316
Reaction score
6,082
Leo nimeamka vizur sana, sikutegemea siku yangu itaelekea kuwa chungu.

Nipo zangu posta natembea mdogomdogo kuelekea ofisini asubuhi ya leo, mara ghafla kuna jamaa akaanza kuniongelesha (umri wake kama miaka 40-50) ambaye nilikuwa natembea nae njia moja....

Mshkaji; Oyaa niaje mzee?
Mimi; Safi mzee niambie?
Mshkaji; Poa kaka unaelekea wapi?
Mimi; (nikasita kidogo kujibu kwasababu simjui) naelekea kazini broo
Mshkaji; Daah sawa

(Mimi nikakaa kimya,
Baada ya kama dakika moja akaendelea kuniongelesha)

Mshkaji; unajua nn broo nimehangaika sana kuomba kazi za kuhudumia bustani na kukata kata majani kweny hizi hotel na ofisi za viongozi kwa miaka kumi na bado sijafanikiwa

(Mimi nikaendelea kukaa kimya, jamaa akaendelea)

Mshkaji; we acha tuu kaka hadi nimekata tamaa na maisha kila ninalofanya sifanikiwi, kazi ngumu maisha magumu, hadi kazi za kufyeka bustani nakosa kweli!!

(Sikuwa na kitu cha kumjibu kwasababu kanishtukiza ila nilihisi inabidi niongee kitu kwasababu kukaa kimya sidhani kama ni jambo zuri na jamaa anafunguka mambo yake)

Mimi; Usijali mwanang utapata, endelea kupambana

Baada ya kumwambia hivo, jamaa akaniangalia kwa jicho bana sana kama vile nimekosea kumwambia vile, hadi nikaanza kuogopa, nikawaza au maybe nimemtukana au kanisikia vibaya, jamaa hakuongea chochote aligeuka pembeni akanisonya, then kila mtu akaendelea na safari zake.

Aisee mimi nipo very sensitive na matatizo ya watu, yaan tokea asubuhi namuwaza yule mshkaji na incident iliyotokea, jinsi mshkaji alivohangaika kutafuta hizo kazi za bustani kweny hotel za pale posta, na mbaya zaidi kinachoniumiza kwann aliniangalia vibaya nilipomwambia maneno ya kumfariji, yaan niishie kusema leo sina raha kabisa.
 
😂😂😂😂😂 sometimes inabidi uwe na majibu short and clear pia usiwe mdadisi sana ....

Hizo sehemu ukiona mtu mpaka kakusimamisha jua amekukadilia mkuu..

Sasa mimi hapo kwanza na hili buti langu ningemuwashia moto aiseee yaani ananiongeleshaje kizembe.....

Angeruka kichura mpaka mtaa wa likoma na agrey..
Alafu tungegeuza tena mpaka keko veta kule ...
 
Mbona namimi nilikua mitaa hiyo ya Posta, karibu na jengo la Kishimba mkabala na Tanganyika stendi ya zamani hapa Mwanza....
Ila aijakuona...🙄
 
Huwa siwapi muda strangers waniambie mambo yao hata kunizoea tu.

Alikuwa anakupanga tu
wewe pia ni stranger kwetu.
Jitafakari sana sio kila stranger ni mwizi, kibaka au mtu mbaya.

Hata Yesu pia ni Stranger kwako, ila bado unampa muda
 
Leo nimeamka vizur sana, sikutegemea siku yangu itaelekea kuwa chungu.

Nipo zangu posta natembea mdogomdogo kuelekea ofisini asubuhi ya leo, mara ghafla kuna jamaa akaanza kuniongelesha (umri wake kama miaka 40-50) ambaye nilikuwa natembea nae njia moja....

Mshkaji; Oyaa niaje mzee?
Mimi; Safi mzee niambie?
Mshkaji; Poa kaka unaelekea wapi?
Mimi; (nikasita kidogo kujibu kwasababu simjui) naelekea kazini broo
Mshkaji; Daah sawa

(Mimi nikakaa kimya,
Baada ya kama dakika moja akaendelea kuniongelesha)

Mshkaji; unajua nn broo nimehangaika sana kuomba kazi za kuhudumia bustani na kukata kata majani kweny hizi hotel na ofisi za viongozi kwa miaka kumi na bado sijafanikiwa

(Mimi nikaendelea kukaa kimya, jamaa akaendelea)

Mshkaji; we acha tuu kaka hadi nimekata tamaa na maisha kila ninalofanya sifanikiwi, kazi ngumu maisha magumu, hadi kazi za kufyeka bustani nakosa kweli!!

(Sikuwa na kitu cha kumjibu kwasababu kanishtukiza ila nilihisi inabidi niongee kitu kwasababu kukaa kimya sidhani kama ni jambo zuri na jamaa anafunguka mambo yake)

Mimi; Usijali mwanang utapata, endelea kupambana

Baada ya kumwambia hivo, jamaa akaniangalia kwa jicho bana sana kama vile nimekosea kumwambia vile, hadi nikaanza kuogopa, nikawaza au maybe nimemtukana au kanisikia vibaya, jamaa hakuongea chochote aligeuka pembeni akanisonya, then kila mtu akaendelea na safari zake.

Aisee mimi nipo very sensitive na matatizo ya watu, yaan tokea asubuhi namuwaza yule mshkaji na incident iliyotokea, jinsi mshkaji alivohangaika kutafuta hizo kazi za bustani kweny hotel za pale posta, na mbaya zaidi kinachoniumiza kwann aliniangalia vibaya nilipomwambia maneno ya kumfariji, yaan niishie kusema leo sina raha kabisa.

Grow up we mtoto
 
Yaani bado unaendelea kunisimanga Tu bro mbona mi nimekupotezea baada ya kuninyima buku ya fegi
 
Huwa inatokea kwenye kusoma tunasema "maana ya msemaji na maana ya mpokeaji"Kuna wakati zinatofautiana
Kuna siku boss wangu alikuwa anatafuta funguo akaniambia nikamwambia "don't worry you will find it"
Akajibu kwa msisitizo sana "I must worry" na hakuendelea kunisemesha ila aliipata mda mfupi
 
Nakumbuka kuna siku nilikuwa posta mida ya jioni, miaka hiyo hata chuo sijaingia lakini kuna jamaa mmoja kavaa kiofisi na bahasha ya kaki akanisimamisha njiani na kuanza kuniomba nauli ya kwenda tabata. Nakumbuka nilimpa buku mbili alishukuru sana sanaaa

Sikuwahi kujua kuwa ipo siku nitajikuta kwenye hali ileile kama graduate ambaye nauli tu ya kunitoa posta kurudi home nilikosa. Siku nilipopitia hiyo hali daahhh nilimuelewa jamaaa sana na kuna njia ya posta hadi leo sipendi kupita maana inanikumbusha hiyo moment ya kutaka kumuomba stranger nauli. Hiyo hali Inafadhaisha na kudhalilisha kupita kiasi

Simaanishi kwamba jamaa alikuwa sawa kukufuata sana lakini sometimes mambo tunayoyaona hayawezekani huwa yanawatokea watu
 
Kwani hoteli Zenye bustani zipo Posta Tu Dar Kwa Tz nzima??
 
Back
Top Bottom