Jinsi suala la bandari linavyoidhalilisha na kuichafua LHRC

Habari zenu wanaJF wenzangu,

Ki ukweli hili suala la bandari ilikuwa ni lazima litokee ili watanzania tuweze kuwajua maadui wetu wa taifa. Lakini pia ilikuwa ni lazima litokee ili tuweze kuwajua wale Chui na Simba, waliojivika ngozi ya Kondoo na Swala.

Watanzania wenye akili zetu timamu we can't imagine inakuaje mzazi ambae unajifanya una elimu, malezi bora ya wazazi wako, utu na uwezo wa kutetea haki za binadam uache wanasiasa uchwara wamtukane kiongozi wako ambae ndio raisi wako matusi ya laana. I mean wamdhihaki, wamkejeli na kumdhalilisha mbele ya watoto wake na wananchi wake halafu wewe ukae kimya tu unacheka, na kujifanya hujui wala huoni.

Je, kumdhalilisha mkuu wa nchi kwa kusema kuwa ana akili za matope sio kumvunjia haki zake, kumvunjia heshima yake na kumfanya hana maana mbele ya wananchi wake?

Ikiwa umeshindwa kuwakemea hawa wanasiasa waliomtukana Rais, je utaweza kuwakemea watoto wako wa kuwazaa pale wanapovunja haki za wengine?

Au haki huwa inatumika tu kwa wale waliopo upande wako peke yako?

Tukiachana na hilo la wanasiasa wako kumtukana Rais, pia tumeshangazwa na kauli yako ya uongo kwa watanzania kwamba kina Dkt. Slaa wamekamatwa kwa sababu ya kupinga mkataba. Huu ni uongo mkubwa ambao unatakiwa ujitokeze hadharani kutuomba radhi watanzania kwa kutudanganya, na kujaribu kutufanya mazuzu.

Nasema umetudanganya watanzania kwa sababu kama kukamatwa kwao kungehusiana na ukosoaji wa bandari, basi kina kardinal Pengo, Prof Anna Tibaijuka, mzee Warioba, Mbowe, mtukanaji Lissu na wengine wengi wangekuwa jela sasa hivi.

Watanzania tunajua kile kilichowasukuma wewe na genge lako muamue kupindisha ukweli. Lakini nakuhakikishia kuwa hakuna baya" linaloweza kushinda "jema". Mtashindwa na mtadhalilika.

Japo umejaribu kuficha unafiki wako kwa kuunga unga vijistori vya hovyo, lkn uso wako kupitia macho yako na midomo yako vilikuwa inaonesha chuki ya wazi iliyopo ndani ya moyo wako dhidi ya Serikali yetu na raisi wetu.

Inasikitisha sana kuona mtu ambae ungepigania haki na sheria unakimbilia kwenye vyombo vya habari kupindisha sheria kwamba kina Slaa wamekamatwa kwa kukosoa mkataba utafikiri wewe ndio mahakama.

Unachotakiwa kujua kwamba mwanasiasa hana rafiki wa kudumu. Hao unaowatetea kwa uovu wao wa leo, kesho utaporudi kwenye mstari na kusimamia ukweli watakutukana na kukudhalilisha kama wanavyodhalilisha wengine.

Hebu soma maelezo ya Dkt. Slaa hapo pichani, halafu uniambie ni nani aliekuwa anajua kama Dkt. Slaa angekuwa miongoni mwa wanaopanga kumpindua raisi Samia?

Sio siri mama Anna Aloys Henga umejivunjia heshima na umejidhalilisha. I mean umeichafua CV yako kwa sababu ya kuliendekeza tumbo lako.

Kuanzia leo watanzania hatutakuita tena mtetezi wa haki za binadam, bali tutakuita mtetezi wa maadui wa taifa, na wapigania matumbo yao.

Dkt. Slaa mwenyewe ashaonya enzi za Mbowe kwamba dunia nzima hakuna mwananchi anaeweza kusema kwamba fulani ni mhaini au sio mhaini. Sasa wewe Anna unapata wapi ujasiri wa kupinga kuwa Slaa sio mhaini kabla mahakama haijaamua vinginevyo?
Kwani wametukanaje? Wengine tumepitwa na hayo matusi.
 
Mkiambiwa mchelea mwana hula na wa kwao muwe mnaelewa. Taasisi nyingi za kisheria kwa hili suala la mkataba wa bandari zimeamua kuwa za kinafiki au kukaa kimya, kimya cha kinafiki pia. Ina maana hawaoni utata wa mkataba huo au wameamua mambo yaende hivyohivyo tu kuepukana na kusulubiwa kwa kusimamia rasilimali za taifa? Shangaa msomi yule anayedanganya mchana kweupe eti wanaokamatwa kamatwa hawakamatwi kwa kupinga mkataba wa bandari. Hizi ni siasa za matango pori
 
Toa uthibitisho hapa kama kweli Rais wako ana akili timamu na siyo matope!
 
Mkiambiwa mchelea mwana hula na wa kwao muwe mnaelewa. Taasisi nyingi za kisheria kwa hili suala la mkataba wa bandari zimeamua kuwa za kinafiki au kukaa kimya, kimya cha kinafiki pia. Ina maana hawaoni utata wa mkataba huo au wameamua mambo yaende hivyohivyo tu kuepukana na kusulubiwa kwa kusimamia rasilimali za taifa? Shangaa msomi yule anayedanganya mchana kweupe eti wanaokamatwa kamatwa hawakamatwi kwa kupinga mkataba wa bandari. Hizi ni siasa za matango pori
Wewe nae ndio wale wale mnaoshikiwa akili na wanasiasa uchwara wa Tanzania.

Nimeamini kuwa siasa za Tanzania sio lazima mtu usome, bali uwe na uwezo wa kushikilia au kumiliki akili za wale wanaoamini kila wanaloambiwa na wanasiasa husika.

Hivi kama kina Dr Slaa wamekamatwa kwa sababu ya kukosoa, mbona sasa wakosoaji wengine kina Pengo, Prof Tibaijuka, mzee Warioba wapo uraiani hawajakamatwa?

Mbona kina Mbowe na Lisu ambao ndio wapinzani wa kweli wa serilali, tena wanazunguka nchi nzima kupinga mkataba mbona hawajakamatwa?

Hata humu mitandaoni watu wanaandika thread na comments mbali mbali ukiwemo wewe mwenyewe mbona hamjakamatwa?

Mambo mengine hayahitaji akili kuyaelewa maana hata mtoto mdogo wa miaka mi5 anaweza kuyaelewa.
 
Unataka akili gani nje ya wanasiasa kwa mtazamo wako? wakitokea wanasiasa wa pande mbili wanapingana sisi wengine hupima mizania na kuja na maoni yetu bila kujali tuko upande gani
 
Sijakataa kwamba kila mtu yupo huru kuamini au kumsikiliza mwanasiasa anaemtaka bila kujali kama mwanasiasa huyo anasema uongo au ukweli.

Tatizo ni pale unapolazimisha na watu wengine waamini kile kinachosemwa na mwanasiasa unaempenda hata kama mwanasiasa huyo anaongea uongo wa wazi kabisa.
 
Back
Top Bottom