Jinsi suala la bandari linavyoidhalilisha na kuichafua LHRC

Kwani wametukanaje? Wengine tumepitwa na hayo matusi.
 
Mkiambiwa mchelea mwana hula na wa kwao muwe mnaelewa. Taasisi nyingi za kisheria kwa hili suala la mkataba wa bandari zimeamua kuwa za kinafiki au kukaa kimya, kimya cha kinafiki pia. Ina maana hawaoni utata wa mkataba huo au wameamua mambo yaende hivyohivyo tu kuepukana na kusulubiwa kwa kusimamia rasilimali za taifa? Shangaa msomi yule anayedanganya mchana kweupe eti wanaokamatwa kamatwa hawakamatwi kwa kupinga mkataba wa bandari. Hizi ni siasa za matango pori
 
Toa uthibitisho hapa kama kweli Rais wako ana akili timamu na siyo matope!
 
Wewe nae ndio wale wale mnaoshikiwa akili na wanasiasa uchwara wa Tanzania.

Nimeamini kuwa siasa za Tanzania sio lazima mtu usome, bali uwe na uwezo wa kushikilia au kumiliki akili za wale wanaoamini kila wanaloambiwa na wanasiasa husika.

Hivi kama kina Dr Slaa wamekamatwa kwa sababu ya kukosoa, mbona sasa wakosoaji wengine kina Pengo, Prof Tibaijuka, mzee Warioba wapo uraiani hawajakamatwa?

Mbona kina Mbowe na Lisu ambao ndio wapinzani wa kweli wa serilali, tena wanazunguka nchi nzima kupinga mkataba mbona hawajakamatwa?

Hata humu mitandaoni watu wanaandika thread na comments mbali mbali ukiwemo wewe mwenyewe mbona hamjakamatwa?

Mambo mengine hayahitaji akili kuyaelewa maana hata mtoto mdogo wa miaka mi5 anaweza kuyaelewa.
 
Unataka akili gani nje ya wanasiasa kwa mtazamo wako? wakitokea wanasiasa wa pande mbili wanapingana sisi wengine hupima mizania na kuja na maoni yetu bila kujali tuko upande gani
 
Unataka akili gani nje ya wanasiasa kwa mtazamo wako? wakitokea wanasiasa wa pande mbili wanapingana sisi wengine hupima mizania na kuja na maoni yetu bila kujali tuko upande gani
Sijakataa kwamba kila mtu yupo huru kuamini au kumsikiliza mwanasiasa anaemtaka bila kujali kama mwanasiasa huyo anasema uongo au ukweli.

Tatizo ni pale unapolazimisha na watu wengine waamini kile kinachosemwa na mwanasiasa unaempenda hata kama mwanasiasa huyo anaongea uongo wa wazi kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…