Jinsi Tajiri aitwaye saa tatu alivotumia nguvu ya pesa kubomoa nyumba huko Tunduma.

Jinsi Tajiri aitwaye saa tatu alivotumia nguvu ya pesa kubomoa nyumba huko Tunduma.

Joined
Dec 26, 2015
Posts
68
Reaction score
46

Tukio hilo la kubomolewa Kwa nyumba hiyo limetokea huko Tunduma na nyumba hiyo inasemekana ni mali ya marehemu pamoja na mke wake ambaye yuko hai. Inasemekana marehemu aliacha watoto kutoka kwa wake tofauti na kila mke alikuwa na nyumba yake.

Baadaye watoto wa marehemu Wakafungua shauri la mirathi wakateuliwa wasimamizi wa tatu, wawili kati yao wakaingiza nyumba hiyo kwenye mirathi wakaiuza kwa huyo mnunuzi abaitwa saa tatu na eneo ni potential kwelikweli mmoja kati yao akafungua kesi lakini na mke wa marehemu ambaye ndo mmiliki wa hiyo nyumba naye akafungua kesi.

Kesi zimeenda yule msimamizi wa mirathi mmoja ambae hakushiriki kuuza akashindwa kesi yake wakati huo mke kesi yake bado haijaisha na amewekewa zuio la mahakama la nyumba kutobomolewa.

Huyo mnunuzi akaamua kufosi kubomoa juzi Jumamosi baadhi ya ndugu wakamzuia asibomoe ndugu wakaripoti polisi hakuna alietoa ushirikiano ni kama jamaa alikuwa kamwaga mpunga kote leo pia kaja kubomoa ukazuka ugomvi mkubwa mno wenye nyumba wanatoa zuio la mahakama wabomoaji hawajali lakini pia wabomoaji hawana amri yoyote ya mahakama ya kubomoa ila mama anazuio.

Huyo mnunuzi leo kaamua kukodi njemba kibao na security wa kampuni fulani kwa ajili ya kubomoa na amefanikiwa kubomoa ila hakuna polisi hata mmoja alietokea licha ya tukio kulipotiwa polisi kwa OCS na mke mpaka sasa amebakia hana makazi. Ama kweli pesa inaweza kununua haki.

Na hizi ni baadhi ya video za ubomoaji kuna haja ya viongozi wa Serikali kuingilia hili suala kuona undani wake. Malalamiko ya wahusika wanadai kwamba walipeleka order yao ya zuio polisi lakini hakuna msaada wowote walioupata.

 
Hivi ndivyo vitu vya 'Mama' kujichukulia ujiko kwa kumsaidia huyo Mama kupata Haki yake na walioshiriki kuwajibishwa.

'Mwendazake' Show kama hizi alikua akizipenda sana.
 
Siku zote ukweli wajulikana kwa kuwasikiliza wote...
Mara nyingi wanaokimbilia huruma huwa si wakweli
 
Back
Top Bottom