Da'Vinci
JF-Expert Member
- Dec 1, 2016
- 35,812
- 107,628
Salute
Kipindi cha nyuma kabla sijawa na ufahamu wa masuala ya teknolojia nilikua nikiangalia muvi kama vile KingKong, Jurasic Park,Godzila,RoboCop, Cyborg , Terminator nk nilikua najua kwamba vile viumbe vya ajabu kwenye muvi hizi nilizotaja ni watu waliovaa vinyago/costume natumaini sio mimi pekee niliyokua nina fikra hizi bali ni watu wengi wanawaza hivi na mpaka leo hii wengi hujua hivi. Ukweli ni kwamba katika muvi hizi kuna teknolojia kubwa nyuma yake hadi muvi inapokamilika basi kazi kubwa imefanyika hapo ndio Application ya Physics hua inaonekana, wenzetu wazungu wameendelea sana huwa hawaendi tena location kurekodi matukio bali kila kitu kinamaliziwa ndani ya ukumbi.
Makampuni mengi ya utengenezaji wa muvi kama Disney,marvel,warner Bro, Sony nk muvi zao nyingi wanazitengenezea kwenye studio yaani ukumbi ambao unaweza kuset kila kitu kutokana na mazingira ya muvi unayotaka halafu wanamalizia kwa computer. Lakini wenzetu wanawezaje kutengeneza vitu vya kufikirika tunavyoona kwenye muvi mabalimbali?
Kwenye miaka 60 Bwana mmoja aitwae Lee Harrison III ambae alikua ni mtengenezaji wa katuni aligundua kwamba circuits, cathode ray tubes, na adjustable resistors zinaweza kurekodi na kuweza mjongeo wa mtu kupitia idea yake hii dunia iipata teknolojia mpya ambayo ilikuja kuboresha utengenezaji wa muvi.
Motion Capture
Ni mfumo wa kurekodi mjongeo wa kitu au mtu mara nyingi mfumo huu hutumiwa jeshini,michezo,afya na burudani. Katika utengenezaji wa filamu mfumo huu hutumiwa kurekodi matendo ya mwigizaji na kwa kutumia mjongeo huo unaweza kutengeneza kiumbe au kitu chochote unachokitaka katika mfumo wa 3D au 2D kwenye computer. Katika mfumo huu mwigizaji huvaa suti maalumu ambayo inakua imewekewa Dots (vinafahamika kitaalamu Marker) maalumu ambazo zinakua zina sensor..senesors hizi zinawezesha kamera kuona position ya hivyo vidot, dots hizi huwa kila sehemu ambapo kuna maunaganisho ya ya viungo (joints) hivyo basi kamera inakua inarekodi position na mjongeo wa hivyo vidot.
Kwa kutumia vidot hivyo basi unaweza kutengeneza kiumbe au mtu yoyote unayetaka, kupitia teknolojia hii inawezesha kurekodi mjongeo wa muigizaji na matendo ya muigizaji kwa wakati mmoja….Kwa ufupi ni kwamba hua hawarekodi mtu bali matendo na mjongeo wa viungo vyake.
[Muigizaji Akiwa na mavazi ya motion capture yenye marker/Dots kwenye Joints]
Sasa teknolojia hii inakua tofauti kidogo kama unataka kurekodi mjongeo wa sura ya mtu ili iwe halisi, mfumo huu wa kurekodi mjongeo wa sura ya mtu huitwa facial capture. Katika mfumo huu sura ya mtu huwekewa vidot hasa kwenye kope,nyusi,kidevu, lips,kisha huvishwa kamera /scanner za kidigitali ziitwazo lasser Scanner ambazo hurekodi /scan mjongeo wa sura kama vile kucheka,kutabasam,kukapua,kununa kushangaa nk.
[Picha zikionyesha Dots za Facial capture na Lasser scanner ambazo zinasaidia kurekodi movement za uso kama tabasam, kununa nk]
Baada ya kurekodi mjongeo/movement za mwigizaji , movements hizo huingizwa kwenye mfumo wa Visual effects (VFX) . VFX ni mfumo mtindo wa kutengeneza picha/viumbe au mazingira ya kufikirikana kuyafanya yaonekane halisi kwa kutumia movements zilizorekodiwa kwenye motion capture….kwa ufupi VFX ni mfumo ambao hutumika kutengeneza vitu vya kufikirika baada ya kurekodi vitu, nimesema hivi ili isikuchanganye na SFX.
[Picha zikionyesha kabla na baada ya kufanyika Visual Effects VFX]
Special Effects (SFX) ipo kama VFX ila yenyewe hutumika muda ule wa kurekodi tukio yenyewe hutumika kutengenea illusions kama vile milipuko, mlio wa risasi, mvua kunyesha,vidonda,upepo,mawingu,nk
[Mfano wa Special Effects]
Computer Generated Image (CGI), hii hutumika kutengeneza vitu ambavyo ningumu kuvipata au ni ghalama kuvipata hivyo hutumia kutengeneza picha ya kitu kitu ambacho hakipo kabisa. Mfano mtu anaweza kuwa kaonekana kashika bunduki lakini kiuhalisia hajashika kitu. Kwa ujumla ni kua CGI na SFX ni vipande vilivyomo ndani ya VFX.
[Mfano wa CGI, mtu huyu hajashika kitu hapo]
Chroma key compositing
Ni mtindo wa kuunganisha video au picha mbili kwa kuzingatia mfumo wa rangi, katika mfumo huu sehemu ya nyuma(background) ya video au picha huondolewa na kuwekwa kitu kingine kutegemea na mahitaji ya mtu.katika mfumo huu rangi maalumu huwekwa kama background kisha huondolewa kwa kutumia Visual effects (VFX) , rangi zinazotumika zaidi katika mfumo huu ni Kijani na Blue.Rangi ya blue ilikua inatumika kipindi cha nyuma ila kwasasa rangi ya kijani ndio hutumiwa zaidi kutokana na sababu kadhaa.
Rangi ya kijani ilitumika sana kama backgroung kwenye vituo vya TV kwenye kutangaza utabiri wa hali ya hewa kwa sababu watangazaji wengi hupenda kuvaa nguo/suti za rangi ya blue hivyo hii huleta changamoto wakati wa kufanya VFX maana nguo ya blue ikichanganyikana na background ya blue inafanya mtangazji aonekane hana mwili maana sehemu yenye rangi ya blue yote hufutika.
Hivyo suluhisho ilikua ni kutumia Background ya kijani. Kwakua nguo za rangi ya kijani hua hazivaliwi na watu sana basi waliona kwamba rangi ya kijani itafaa zaidi kuliko rangi ya blue, pia rangi ya kijani hua ipo sensitive zaidi katika rangi ya kijani hivyo ikaonekana rangi ya kijani inafaa zaidi na inatoa picha safi zaidi baada ya kufanya Edit kuliko blue.
Hivyo basi katika filamu background zote mbili blue na kijani hutumika kutokana na mtaumizi ya scene husika, japo kijani ndio inatumika zaidi maana kuna watu wengine wana macho ya blue hivyo huleta changamoto kidogo katika kufanya editing.
Cc Setsuko