Jinsi Tundu Lissu Alivyojikaanga Kwa "Mafuta ya Taaluma Yake!!"

Jinsi Tundu Lissu Alivyojikaanga Kwa "Mafuta ya Taaluma Yake!!"

Buchanan

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2009
Posts
13,192
Reaction score
1,972
Wakuu,
Haina shaka kwamba Hotuba ya Tundu Lissu imevuta hisia za washabiki wengi wa "Serikali 3/Nchi 3!" Pia nichukue nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa huyo kwa kuwasilisha maoni ya wachache na kuchambua Sheria akienda sambamba na historia ya Muungano wetu tangu kuundwa kwake mpaka leo.Mwanasheria huyo nguli, kama baadhi wanavyomwita ameenda mbali sana, bila kuuma maneno akidai kwamba Muungano wetu wa iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika na iliyokuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar hauna uhalali wowote wa kisheria kwa kuwa haukuridhiwa na Baraza la Wawakilishi, hata kama uliridhiwa na Bunge la Tanganyika tu!

Amedai pia kwamba kwa sasa tufute Sikukuu ya Muungano wetu na kuanzisha "Siku ya Shirikisho!"Kwa hoja hizo za Lissu mimi sina ubavu wa kuzipinga kwa kuwa ametaja na vifungu vya kisheria vya wakati huo, tukubali tu kwamba Muungano HAUNA UHALALI WOWOTE WA KISHERIA!

Hata hivyo, Tundu Lissu alifikiri kwamba hoja hiyo inamu-implicate tu Nyerere ambaye amemtaja mara nyingi kwamba mambo mengi ameyafanya kwa AMRI YA RAIS. Mambo hayo ni kamba vile:
1. Jina la Nchi,
2. Kuiua Tanganyika,
3. Nembo ya Taifa, nk.

Kama Muungano hauna uhalali wowote maana yake nini?

1. Ni kwamba Tundu Lissu alifanya makosa kugombea ubunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano "BATILI," kwa hiyo Ubunge wa Lissu mpaka sasa ni "BATILI!"
2. Kwamba, hata mchakato huu wa kuandika Katiba Mpya ni "BATILI" kwa kuwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba imetungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano" BATILI,"
3. Kwamba, Tundu Lissu amechangia kutunga Sheria "BATILI" za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa Bunge nalo ni "BATILI,"
4. Kwamba CHADEMA nacho ni chama "BATILI" kwa kuwa kimeundwa kwa Mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa ambayo imetungwa na Bunge "BATILI" la Muungano,
5. Kwamba, shughuli zote za kisiasa za Tundu Lissu hazina uhalali wowote wa Kisheria kwa kuwa zimefanywa kwa kufuata Sheria za Muungano "BATILI,"
6. Kama Lissu ana vyeti vya Shule za Tanzania navyo ni "BATILI" kwa kuwa vimetolewa na Serikali "BATILI,"
7. Kama Tundu Lissu amezaliwa baada ya Muungano na kupewa Cheti cha Kuzaliwa ahesabu kuwa ni "BATILI" mpaka sasa,
8. Kesi zote alizoshinda Tundu Lissu mahakamani ajue kwamba ni "UBATILI" mtupu maana" MUUNGANO HUU NI BATILI," kwa hiyo hata mahakama za Muungano ni "BATILI,"
9. Kama Tundu Lissu ameoa baada ya Muungano ajue kuwa ameumia, ni ndoa "BATILI" hiyo!!!
10..................

Hongera sana Tundu Lissu kwa Hotuba Murua...............Ila usiendelee kuwepo kwenye BUNGE hilo "BATILI" kwa kuwa limeundwa na Sheria "BATILI!!!" Tafadhali sana, I am not joking, this time around!
 
Akili yake mbaya huyo. Eti kama uwepo wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania sio halali kila kitu na kila sheria ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa nini isiwe halali? Jibu hilo swali Tundu Lissu (Toto Tundu)
 
Labda una IQ ndogo ya kuelewa
mbna ametumia lugha rahisi tu

Mkuu na wewe kwa maoni ya Tundu Lissu inawezekana umesoma na kupata vyeti visivyo halali, ndio maoni ya "Mwanasheria nguli" sio mimi!!
 
Mkuu sielewei unataka kutuambia nini hapa..., Kwahio kama hayo yote ni Batili na hapa imepatikana nafasi ya kurekebisha vya kurekebisha visirekebishwe sababu ya huo so called ubatili uliosema ?

Utarekebishaje kwa utaratibu BATILI mkuu, maana mpaka sasa Bunge Maalum la Katiba ni BATILI, labda tumuulize "Mwanasheria Nguli" Tundu Lissu atuelimishe pa kuanzia!
 
Kwa kweli mfa maji haishi kutapatapa. Hebu kajipangeni tena labda mtapata hoja
 
Unaonekana una uwezo mdogo sana wa kuelewa mambo na kujenga hoja. Unaacha hoja za msingi na kurukia za kijinga.
Jenga hoja kutokana na zilizopo. kwa hali hii wajinga ni wengi sana nchi hii.Mnafaidika nini na kuunga mkono hoja za kijinga kama zinavyotolewa na wajumbe walio wengi bungeni?
 
Akili yake mbaya huyo. Eti kama uwepo wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania sio halali kila kitu na kila sheria ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa nini isiwe halali? Jibu hilo swali Tundu Lissu (Toto Tundu)
Mbunge Lissu atoke Bungeni maana Ubunge wake ni "BATILI!!"
 
Kwa kweli mfa maji haishi kutapatapa. Hebu kajipangeni tena labda mtapata hoja

Hivi Muungano BATILI unaweza ukaunda Taasisi yoyote HALALI? Kama kuua Tanganyika hakukuwa HALALI hata kuunda Taasisi yoyote ndani ya Muungano hakutakuwa HALALI, labda kama unatofautiana na "Mwanasheria Nguli!"
 
CCM tulieni sindano iingie, "It looks like you don't know how advanced presentations are done. What Lissu was doing was to present the facts with evidence based facts before the CA, Unfortunately you being a shallow scientist you know nothing about what Lissu was talking about. It needs more than 50 years to realize the truth at hand."

Ninachoshangaa kwako mpaka hapo hujaelewa lolote? Du kama watu wa namna yako ndo wawe watawala wetu miaka mingine hamsini bado hata hizo raslimali za gesi na mafuta itakuwa ndoto kufaidika nazo kama ilivyo kwenye dhahabu na Almasi pamoja na Tanzanite sasa wametuachia mashimo na bado watu wanashangilia kama mazuzu...
 
Unaonekana una uwezo mdogo sana wa kuelewa mambo na kujenga hoja. Unaacha hoja za msingi na kurukia za kijinga.
Jenga hoja kutokana na zilizopo. kwa hali hii wajinga ni wengi sana nchi hii.Mnafaidika nini na kuunga mkono hoja za kijinga kama zinavyotolewa na wajumbe walio wengi bungeni?

Mkuu wewe unaonesha kuwa hujasikiliza "maoni ya wachache" yaliyowasilishwa na "mwanasheria nguli!"
 
CCM tulieni sindano iingie, "It looks like you don't know how advanced presentations are done. What Lissu was doing was to present the facts with evidence based facts before the CA, Unfortunately you being a shallow scientist you know nothing about what Lissu was talking about. It needs more than 50 years to realize the truth at hand."

Ninachoshangaa kwako mpaka hapo hujaelewa lolote? Du kama watu wa namna yako ndo wawe watawala wetu miaka mingine hamsini bado hata hizo raslimali za gesi na mafuta itakuwa ndoto kufaidika nazo kama ilivyo kwenye dhahabu na Almasi pamoja na Tanzanite sasa wametuachia mashimo na bado watu wanashangilia kama mazuzu...
Mkuu wewe umesikiliza kweli Hotuba ya "Mwanasheria Nguli?" Acha kuleta mambo ya rasilimali hapa, si mahali pake, hapa tunazungumzia juu ya Muungano wetu ambao ni BATILI, as simple as that!
 
Huna tofauti kimawazo na wale Wenyeviti wa Bunge Maalum la Katiba wanao wakilisha waliowengi , hasa kwa mawazo yako 1. hadi 10..... Poor Points with a lot of words.
 
Kuendelea kumsakama Tundu Lissu ni kujidhalilisha, Kama unakumbuka vema wakati wa Kampeni za Uchaguzi wa 2010 Mkulu wa Kaya alisikika akiwaamboa wana Iramba Mashariki kwamba Kumpa Tundu Lissu kura kuingia Bungeni ni kuwaletea wana CCM shida kubwa Bungeni. Ni afadhali kura zake za Urais apewe Dr. Slaa kuliko kumpa Ubunge Tundu LISSU.

Kwa wenye akilim wote wanaendelea kushangazwa na tabia ya wana CCM kuendelea kumsema Vibaya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mh. Jaji Joseph Sinde Waryoba, sasa naona sindano imeingia sawasawa mmeamua kuhamishia vita yenu kwa Mh. TUNDU LISSU.

Kama hujapata fursa ya kusoma both sides of the reports wall usimlaumu Tundu Lissu. Wambieni Prof. Shivji na Dr. Mwakyembe wakanushe taarifa ya Tundu Lissu
 
Huna tofauti kimawazo na wale Wenyeviti wa Bunge Maalum la Katiba wanao wakilisha waliowengi , hasa kwa mawazo yako 1. hadi 10..... Poor Points with a lot of words.

Mimi nimetoa pointi tupu, ndio maana hujakanusha hata moja, yaani umeshindwa pa kuanzia! Mimi nimekubali kuwa Muungano wetu ni BATILI, ila Lissu naye amechangia katika kuendeleza mambo BATILI. Au tuseme amegundua juzi tu wakati anaandaa Ripoti ya Wachache kuwa MUUNGANO WETU NI BATILI?
 
Back
Top Bottom