Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 1,194
- 911
Malengo ya waasisi wa CHADEMA yalikuwa ni kukijenga chama kwenye misingi imara ya kisiasa nchini kikisimama kama taasisi kuu ya upinzani iliyokusudiwa kutoa ushindani wa kisera na kuwa mbadala wa fikra baada ya CCM.
Hata hivyo mwelekeo huo wa kimaono ulianza kupotea na kuyumba pale chama kilipoachiwa mikononi mwa watu wasio na uwezo wa kuenzi malengo yake ya asili.
Hivi karibuni chama hicho kimeonyesha kuporomoka kwa ushawishi wake na kupotea kabisa kwa ajenda zenye tija kwa Taifa.
Badala ya kuimarika kama taasisi CHADEMA imeingia kwenye mkwamo mzito wa kimkakati unaochangiwa na mienendo ya viongozi wake wawili Tundu Lissu na John Heche.
Viongozi hawa wamefanikiwa kuua siasa za hoja na badala yake wamepandikiza siasa za uhasama, chuki na harakati za mihemko ambazo hazina tija kwa maendeleo ya Mtanzania wa kawaida.
Tundu Lissu amekigeuza chama kuwa jukwaa la "ushahidi wa kisheria," akija na sera za ajabu na malalamiko ya kudumu mbele ya jumuia za kimataifa.
Anaamini kimakosa kuwa siasa ni kutoa hotuba kali za lugha ya Kiingereza badala ya kugusa maisha na kero za Watanzania wa vijijini.
Soma Pia: Mwanza: Baadhi ya viongozi wamshauri Heche asisitize kesi ya Lissu ipelekwe haraka na si kuitisha maandamano
Kiburi chake na tabia ya kutaka kuonekana yeye ndiye "mjuaji" wa kila kitu kimefukuza wanachama wenye busara na kukiacha chama kikiwa na kundi la watu wanaofuata upepo wa mihemko badala ya mikakati ya kishindani.
Lazima ijulikane kama Lissu hajengi chama anajijenga yeye kama "shujaa wa kufikirika" huku taasisi ikisambaratika.
John Heche kwa upande wake amekuwa mstari wa mbele katika kukuza siasa za chuki na uchochezi wa barabarani.
Heche anaamini kuwa vurugu na mapambano dhidi ya vyombo vya dola ndiyo njia pekee ya kufanya upinzani akishindwa kuelewa kuwa wananchi wa leo wanahitaji kuona hoja za bajeti, sera za kilimo na suluhu za kiuchumi.
Siasa zake za "kugombanisha" wananchi na serikali zimekifanya chama kionekane kama genge la wahuni badala ya taasisi iliyojengwa kwa ajili ya Malengo ya kujenga.
Muunganiko huu wa Lissu na Heche umezalisha ombwe la uongozi ambalo limekimbiza watu makini na wenye maono ndani ya CHADEMA.
Matokeo yake ni chama kilichobaki na kundi linalopinga kila kitu bila kutoa mbadala wowote wa kimaendeleo.
Wamepoteza mwelekeo kwa kuchagua kuwa "wanaharakati wa mitandaoni" wanaotafuta "kiki" badala ya kuwa viongozi wanaopigania maisha ya watu.
Ikiwa CHADEMA haitawavua viongozi hawa wawili na kurejea kwenye misingi ya busara basi historia itawataja Lissu na Heche kama watu walioizika rasmi CHADEMA.