Habari JF members
Nimeona leo nielezee tabia ya kukurupuka ilivyonipa hasara mara kadhaa. Nimejifanyia tathmini nkagundua huwa nikitaka kufanya jambo lolote huwa napenda nilifanikishe kwa haraka sana ili niruhusu akili iweze ku focus na vitu vingine. Lakini tabia hii imenigharimu sana nakuepelekea kupata hasara ambazo ningeweza kuzizuia.
Mwaka 2022 na 2023 hii miaka nlinunua plots kadhaa za viwanja kutoka kwenye haya makampuni ambayo yanafanya promotion sana siku hizi mitandaoni, kununua haikua shida ila kwavile sikutuliza akili nkajikuta nimenunua viwanja haraka haraka bila kufanya hata research kidogo ila niweze kufanya comparison ya bei, hapa kwa haraka haraka 10m nkawa nimeipoteza ambayo ningetuliza akili nsingepigwa.
Kwenye kufatilia hati miliki hapa napo nimepoteza hela nyingi sana lakini sikuwa na namna.
Mwaka 2023 kipindi nafatilia passport ya kusafiria, hapa nlijikuta nimetumia karibu 750k sababu ya tabia hii hii ya kufanya vitu haraka haraka, kilichotokea hapa ni kwamba cheti changu cha kuzaliwa kilikua na makosa tarehe ya kuzaliwa, sasa kule uhamiaji wakaniuliza kama naweza kutumia tarehe ile ile ya makosa nkakubali bila hata kufikiria athari zake passport ikatoka, baadaye kufatilia nkashauriwa nitengeze cheti kingine cha kuzaliwa nirekebishe information zangu ziwe sahihi ntengeneze passport nyingine.
Manunuzi yangu ya vitu vingi, hasa vifaa vya electronics nimepoteza sana hela kwa tabia hii hii ya kufanya mambo haraka haraka.
Kuanzia sasa kwenda mbele nimeshaji-commit ntatuliza akili kwa kila kitu nnachotaka kufanya kuepusha hasara zinazoweza kuzuilika.
Karibuni na nyie mtoe uzoefu wenu
Wewe ni mkweli,umejua tatizo,na jinsi ya kulitatua una 95% za kua among 3% ya watanzania waliofanikiwa kivyovyote vile
Wataalaamu wanasema:-
Kabla hujafanya jambo Fanya simple research,weka Tathmini,yaani hata ukienda kununua shati la elfu 1
Ipi bidhaa Bora?,wapi kuna bei nafuu?,bei halisi ipoje na ya dukani ipoje?
Imagine unanunua kiwanja milioni 4,wakati kiwanja hiko hiko ungenunua milioni 2,kabla ya kununua bidhaa yeyote hakikisha siku uliyonunua sio siku ulioiona kwa mara ya kwanza.
Yaaani assume na ndio uhalisia,usiwe na haraka kabisa yaaani,
Kitu pekee cha kua na haraka ni konachoweza kutoka uhai wako ukiwa mgonjwa kwa wakati huo
Imagine ni wangapi wameoa,kuoelewa,na watu kwa kukurupuka,........unatoa mahali 5M plus kwa Malaya,wakati kuna Bikira amejituliza anahitaji tu laki 4πππ
Kiuhalisia kukurupuka ni chanzo cha 80% ya stress duniani
Una one Kali unaenda kusoma bachelor of education eti kosa mkopo,wenzako wanaifanya research wanaenda kupiga macourse yale ya SUA,after 3-5 yrs wapo kwenye mashamba makubwa huko Colorado,California,Israel etc,.....sio rahisi lakini,mwalimu wa chemistry chance za kutoboa kwenye hii nchi hata uingize at least 2M.per month ni almost 0.5%,
Kukurupuka ni sumu Kali sana,Bora usifanye jambo,kuliko ulifanye kwa kukurupuka