Jinsi unavyoweza kumvutia mwanaume wa maana/Bora

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
JINSI UNAVYOWEZA KUMVUTIA MWANAUME WA MAANA/BORA.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Mwanaume wa maana ni ndoto ya wanawake wengi waliopevuka, wanawake wanaohitaji kuwa na familia Bora, familia yenye furaha, Familia yenye Dira, Familia yenye Maadili ikiongozwa na Baba bora anayejua majukumu na wajibu wake. Baba na mume anayejua kumuongoza na kumtawala Mke na watoto.

Mwanaume wa maana ni Yule anayejua thamani ya kuitwa Mume, ajuaye thamani ya kuitwa Baba. Mwenye uwezo wa kubeba majukumu na wajibu kama kichwa cha nyumba kwa AKILI, UPENDO, HAKI na KWELI.

Mwanaume anayejua thamani ya Familia.

Mwanaume anayejua mke ni zawadi ya thamani inayohitaji kutunzwa, kuongozwa na kupew Furaha.
Lakini Mwanaume atakakuwa na Hekima za Haki na upendo wa kumuadhibu Mkewe na watoto kwa mustakabali wa Dira na hatma ya familia waliyoianzisha.

TaikonMaster leo nikasema niwakumbuke Dada zangu. Niwaonjeshe mbinu ambazo mtatumia kuvutuvia Sisi wanaume wa maana, Bora ili tuwaoe na muishi maisha ya Furaha yaliyokusudiwa na mwenye huu mradi wa Dunia.

Nisikuchoshe!

Jinsi unavyoweza kumvutia mwanaume wa maana/Bora;

1. Kujiamini bila Kiburi
Mwanaume bora huvutiwa na mwanamke anayejiamini, anayejua thamani yake bila kujikweza. Kujiamini huonyesha kuwa unajitambua, unajilinda na kujua thamani yako.
Kujiamini kunahusisha uwezo wa akili, uzoefu wa maisha, ujuzi na kujitambua kwako.
Sio unajiamini kisa unamatako makubwa. Huna tofauti na mbuzi kama unafikiri hivyo. Kujiamini kunahusisha akili.

2. Kujiheshimu na Kujiwekea Mipaka
Wanaume wa maana huwaheshimu wanawake wanaojiheshimu na wanaojua kusema “hapana” kwa mambo yanayovunja maadili au hadhi yao. Hii huonyesha msimamo na uzito wa mwanamke huyo. Usikubali kuvunjiwa heshima yako. Usikubali mtu akufanyie mambo ya kipumbavu pumbavu.

Hii utaifanya kama unajitegemea maana kujitegemea na uwezo wa kujilisha na kujitunza ni sehemu kuu ya mwanamke anayejiheshimu. Huwezi ukasema unajiheshimu wakati unategemea pesa za wanaume. Huo ni umbuzi! Na wewe ni mbuzi tuu!

3. Kuwa na Maono na Dira Maisha yako.
Mwanaume mwenye maono huvutiwa na mwanamke mwenye ndoto, malengo na anayejiendeleza. Mwanamke mwenye dira huwa mshirika anayevutia kwenye safari ya mafanikio.
Sasa huna ndoto yoyote unataka mwanaume mwenye ndoto wewe umelogwa wewe.
Ndoto ya kuwa msusi bora jijini, kuwa mpishi wa taifa, kuwa Mwanasheria, kuwa Mwalimu, kuwa Daktari, sio umekaakaa kama mfugo unaosubiri kuchinjwa kwenye Idi au Christmas.

4. Kuonyesha Huruma na Ukarimu wa Moyo kama Mwanamke.

Wanaume wa maana huvutiwa na wanawake wenye moyo wa upendo kwa watu wengine, wanaojali familia, jamii na mazingira yao. Hii huonyesha uwezo wa kuwa mama mzuri wa baadaye.
Mama Bora lazima uwe na huruma na ukarimu. Sio jitu wageni wanakuja unanuna nuna kama lijinga.

Au mume anatuma pesa kwao inakuuma. Inakuuma nini kenge wewe! Hela sio yako. Ndio maana ninawaambia mfanye KAZI ili nanyi mtumie pesa zenu kwa Uhuru. Shenzi kabisa!

5. Kuwepo Kimwili na Kihisia, Kampani.

Mwanaume bora hupenda mwanamke anayeweza kusikiliza kwa makini na kuhusika kihisia katika mazungumzo au changamoto. Hii hujenga uhusiano wa ndani zaidi kuliko sura au umbo tu. Sasa wewe hata chakuchangia huna.
Unawaza kuombaomba kama lijitu lisilo na upeo.
Mapenzi yanahitaji chemistry, sasa unahitaji kuwa na Mtu kama TaikonMaster, Stori zako za kitoto toto kama mtoto. Hujui hata Mambo ya NRNE. Hujui mambo ya uchumi walau basic tuu. Sasa tukiwa pamoja tutazungumza nini?
Haya tuseme tuzungumzie unachikifanya, huna hata biashara. Aah! Hapana!

Ukikaa na watoto utawaambia nini? Jishughulishe, jifunze, ongeza maarifa usiwe mvivu mvivu KAZI kukaa na kuangalia filamu na kuperuzi muda wote vitu visivyo na kichwa wala miguu.

Yaani mwanaume wa maana akuoe ili ashindwe kuwahi kurudi nyumbani kisa hamna mtakachoongea. Hamna urafiki. Really?

My sister, unaenda kuharibu maisha ya kijana wa watu.
Familia ni zaidi ya mapenzi. Sio uwaze ngono tuu hiyo no dalili huna akili.

6. Kutunza Muonekano bila Kujirahisiha

Kujipenda na kujitunza (mwili, mavazi, usafi) ni sifa inayomvutia mwanaume wa maana. Lakini kujirahisi kwa kila mwanaume huondoa mvuto na thamani.
Sio ukae uchi sasa. Vaa mavazi standard kwa uwezo wako. Yanayolinda Heshima, utu na thamani yako kama mwanamke.

Jitunze, sio binti mdogo kama lizee. Umeolewa kidogo unaanza kujisahau.
Jukumu la kutunza mwili wako ni lako mwenyewe. Usimuachie yeyote.

7. Kuwa Mwepesi wa Kuelewa na Kutojifanya Mjuaji

Wanaume bora hawapendi drama au unafiki mwingi. Mwanamke mwenye roho nzuri, anayeishi maisha ya kweli sio ulete maigizo ya kipumbavu.

Mimi nimemaliza, kama mmemaindi mtajua wenyewe.

Mkikataa kununua kitabu shauri yenu.
ZERO TO LEGACY; SAFARI YA KIJANA WA KIAFRIKA.
Tsh 15,000/=
0758216209
Mpesa
Robert Heriel

Ukituma pesa, ntumie ujumbe kisha mchakato wa kitabu ni siku Saba mpaka kumi

Acha nipumzike.

Robert Heriel
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
1753030340886.jpeg
 
Today's perspective
 
Back
Top Bottom