Jinsi vijana wasivyojua thamani ya muda

Jinsi vijana wasivyojua thamani ya muda

Tajiri wa matajiri

Senior Member
Joined
Apr 17, 2024
Posts
166
Reaction score
649
JINSI VIJANA WASIVYOJUA THAMANI YA MUDA

LIFE BEGINS AT 40.... HOW OLD ARE YOU?

Life Begins at 40....

Huo ni msemo wanao Waingereza wakimaanisha maisha yako ijapokuwa yanaanza toka milele iliyopita na toka umeumbwa au toka umefika duniani na toka umeanza kukua nk nk lakini bana maisha #halisi yataanza rasmi siku ukitimiza miaka 40. Ndii!!

Hapo kama bado nauli tena ya daladala ni ishu, ada, chakula, kodi ya nyumba, nk basi ndo utaanza kuelewa maana ya muda uliokuwa unatumia Facebook kulike picha za ajabu na story zisizokupeleka popote.
Nadhani unanielewa sasa hasa wewe ambaye unahisi umri wako bado ni mdogo kwa hiyo bado bado kidogo muda wa kuwa serious na maisha haujafika.

Sikia kijana... TODAY is your future kwa taarifa yako.. Ulipokuwa mdogo ulisema nikiwa mkubwa nitakuwa na gari na nyumba nzuri wazazi wangu wataishi hivi na vile. Je unayo? Je imetokea? Maybe yes. But maybe no.

Kama haijatokea je bado hujawa mkubwa? Bado mdogo ee? Basi kama ni mkubwa ujue kuna kitu hujafanya.

Huenda uko in your 20s or 30s... Unajisemea kwamba nikifika miaka 40 nataka niwe na hiki na kile watoto wangu wasome international school nk. Subiri uone miaka inavyoenda. Usishangae kufika 40 bado umeajiriwa kwa mtu na anakugombeza kwa nini mwanao anaumwa kila siku unachelewa kazini. Kazi nyingi. No bright future. No enjoyable present. Just existing and not living!

Hapo ndo unawaza kufungua kibanda cha M-PESA mtaani kwenu. Wenzako wa umri wako hapo unasikia wameanzisha business in Western Europe. Wamenunua kiwanja Mbezi Beach kwa 800M! Anamiliki Apartment Masaki, Nairobi, Jo'burg, Dubai. Na amezipangisha anapara rental income. Tena in dollars. Wewe kazi yako kutafuta tu wapi waliiba au kama ni mdada wapi alihongwa?

By that time wenzako wakienda Dubai wanafikia The Atlantis, wakienda UK wanaenda kula The Ritz (Google that). Wakitua Las Vegas wanaenda Caesar's Palace. Wanasomesha watoto zao the finest schools available wewe wa kwako wakati huo wamekosa nafasi hata Makongo tu hapo unaambiwa eti pamejaa wameenda ndani ndani huko wanapanda daladala kama tatu mara mwendokasi mara washuke warudi nyuma kidogo ndo wapuyange kwa miguu kwenda shule. Na kurudi hivyo hivyo. Hiyo shule au safari ya kwenda utumwani?

Wenzako in their 40s wanasaidia wasio na uwezo katika jamii wewe ndo kwanza ukipokea simu kutoka kijijini mzazi anahitaji support kidogo una-mute! Wenzako in their 40s wakisikia kuna ujenzi wa nyumba ya ibada wanachangia 10M kimyakimya.. Wewe ukitoa laki moja basi mpaka mtaa wa saba watajua! Halafu unashangaa wenzako wanazidi kuinuliwa. Unaanza kuwaita Freemason. Mwenye nacho ataongezewa au hujui? Na asiye nacho......

Wakati wenzako walikuwa wanajenga maisha na kujifunza vitu vya maana wewe ulikuwa unashinda Facebook kuongelea visivyokusaidia.

Vijana wa kitanzania yani wanajua kiiiila kitu. Uchaguzi hata uwe RWANDA wao wana cha kushauri. Maandamano yawe Kenya wanajua cha kushauri. Ishu hata iwe Ethiopia wanajua cha kushauri. Ikitoka clip hata Malema anaongea issue za Africa Kusini utasikia MWANAUME HUYU.
Muda unaenda hivyo...

Wanajua msanii anapaswa aongee nini kwenye interview ya maisha yake mwenyewe. Khaa! Wana maoni anatakiwa adate na nani na aachane na nani. Wanajua mahusiano ya zamani na ya sasa na yajayo ya msanii.
Muda unaenda hivyo...

Wanajua LIGI YA TANZANIA. LIGI YA ULAYA. Wanajua nani anapaswa kuwa kocha wa timu iko hata Ufaransa huko.
Muda unaenda....

Sasa my friend utaweza wewe kufanya vitu ambavyo wazazi wako wote wawili walishindwa? Utaweza kutengeneza GENERTIONAL WEALTH wewe?


Umeshajadili Zitto Kabwe ukaja Lissu, ukadakia Makonda mara una Msigwa...

Hivi vitu kila napoona vijana wanatumia muda kujadili watu.ambao wameshaju estdblish na wanajua wanachofanya huwa najisikia huruma sana... mtu anamtukana mwanasiasa ambaye hajui hata robo ya kinachojiri kwenye ulimwengu hadaa wa siasa!

Hebu fikiria kidogo. Yoote hayo yamekufikisha wapi? Mara Nape Nauye. Haji Manara. Mara unajadili Mwijaku eti. Khaaa.. Are you serious? Unafatilia habari zake mpaka kichwa kinajaa habari zinazokuvuruga tu. Haya mara Harmonize na Harmorapa je? Vitu hivi vinawezaje kuwa sehemu ya muda wa mtu ambaye yuko serious na maisha yake?

Mbowe uliyemjadili amekufikisha wapi. Makonda umefika nae wapi? Mara ujadili sijui Zari ana umri gani. Can you imagine? Yaani hicho ndo kichwa cha kijana wa kitanzania. Ukimwambia vitu vya maana anasema hana muda. Lol!! Mwingine anatukana!

Wenzako mkifika miaka 40 watu wa rika lako wana exposure ya uhakika. Wewe at 40 bado umeajiriwa na mchana unakula kwa mama lishe chakula hata virutubisho hakina. Wenzako at 40 washaacha ajira siku nyingi washatembea dunia na kujifunza maisha kutoka kila mahali. Walishafika kuanzia Sauzi, Botswana, Mozambique, Kenya, Ethiopia, Ghana, mpaka Egypt, The UK, Australia, Hawaii, Mexico, Croatia, The Netherlands, Switzerland, US, Panama mpaka Puerto Rico, Brazil na jirani zake, Hong Kong, Australia, Japan, China, (Incredible) India, Thailand, Singapore, New Zealand, Comorros, you name it..!!

Wewe hata Kampala hujawahi fika. Kila siku Tegeta Posta ndo ruti yako miaka 15 mfululizo eti unatafutia watoto maisha!

Unaishi au unaisha? Na watoto wenyewe nda wale safari ya shule kama safari ya kwenda utumwani!

Unasubiri kiinua mgongo? Utaenda kukiinvest wapi na kwa nguvu ipi. Na utaenjoy retirement kweli kama at 60 yrs ndo unafungua duka la vifaa vya ujenzi eti vinalipa. Kwa nini hukufungua ukiwa 30yrs ili uone vinalipa au la. At 60? With due respect. Kisa ulikuwa unafatilia ratiba zote za mechi za mpira na matamasha na mikutano yote ya kisiasa ukasahau muda unaenda.

Listen...
Hao unaowafatilia wako ndani ya kazi zao kwa hiyo muda wao unatumikia shughuli zao wakati wewe utatumia muda wako na pesa yako kwenda kuangalia nk. Jenga nidhamu mpya ya kulinda muda wako sasa.

Suffer the pain of discipline now. Or else you will suffer the pain of REGRET. Halafu ukianza kuregret ndo pressure zinakuja, stress, nk mwisho unawacha hata hao watoto (wale wa kwenye safari ya utumwa) in a far worse situation than your own lifetime. Kisa? Ulikuwa unatumia muda wote kuangalia vitu vya kuchekesha chekesha unaita MEMEs. Kuna Account Instagram kabisa eti za MEMES. Mwenzio anafanya biashara kwa kukulisha ujinga...

Seriously Mungu atakupa mafanikio kws kichwa hicho kilichojaa vitu cheap cheap hivyo?

Hivi vitu vinaiba muda wako sana ndugu zangu. Mtu akikutumia MEME ya vitu vya kijinga ujue kakuona wewe mjinga tu na huna direction kwenye maisha. Kuna watu anawaheshimu hawezi kudiriki kuwatumia huo upuuzi.

Hapa sijaongelea PORN*GRAPHY. Kichwa kilichojaa picha za ngono simu imejaa upuuzi kichwa hicho hicho kije kimiliki uchumi usaidie taifa na Jamii wewe huyo? Kama umeshindwa KUDELETE tu picha za ngono utunze usahihi wa fikra zako utaweza kutunza MILIONI HATA 100 wewe?

Utashangaa umri unaenda bila kupiga hatua. Umri wako ni kila sekunde na kila dakika na kila saa. Ndo umri huo. Umri siyo mwaka kwa mwaka. Ni sekunde na dakika. Ndo maana matajiri wanalinda muda wao kwa wivu mkali. Coz TIME IS MONEY.

Utashangaa unapoteza muda afu unafika 40 years ndo unawaza uanzie wapi. Wewe huko uliko angalia watu wenye miaka 40 plus ujifunze mapema. Wachunguze tu. Wengine bado kaajiriwa stress nyingi hata kusomesha ni issue. Kwani watoto walimshtukiza tu wakazaliwa ghafla wakafika umri wa shule? No. Time management my friend.

Mungu siyo mjinga kukupa umri huu wa ujana. Hajakupa uuchezee chezee tu.. Be careful my friend. Time flies.

Life Begins at 40 my friend.. How Old Are You?

So kama wewe unasema "Mimi bado mdogo.." endelea tu kupoteza muda wako utakumbuka tu siku moja but it might be too late.

Ni muhimu kujifunza haya mambo. Siasa hazitaisha. Angalia your life. Ukifika 40 years uwe very established. Bila hivyo utashangaa kweli. Wakati wenzako wachache wa rika lako mtakapofika miaka 40 wakati wenzako unasikia amenunua kiwanja Kurasini kwa sh Bilioni mbili kwa ajili ya kupaki tu Masemitrela zake kama 20 hivi wewe wakati huo unashangaa Kama Kurasini kumbe kuna viwanja? Wakati huo wewe unamiliki kigari cha mkopo unakipaki uwanja wa CCM unalipia sh 1000/- tu, mnaita buku na yenyewe sometimes unadaiwa. Fikiria vitu kama hivi. Utajua vizuri umuhimu wa kutumia muda wako vizuri.

Sasa ni November hiyo mwaka umeshaanza kuyoyoma.

And life, REAL LIFE, Begins at 40 my friend.

ENDELEA KUCHEZA
 
Mkuu umeeleweka sana but naona umelaumu zaidi badala ya kutoa ushauri kuwa watu wafanye nini na nini wasifanye
 
Mkuu umeeleweka sana but naona umelaumu zaidi badala ya kutoa ushauri kuwa watu wafanye nini na nini wasifanye
Yeye mwenyewe kacopy sehemu kaja kupaste jf anajifanya andiko ni lake. Nilishawahi kulisoma sehemu mwaka 2017 huko.
Screenshot_20241103_113902_Firefox.jpg
 
Back
Top Bottom