Jinsi viongozi wanavyotupiana katiba mpya kama kaa la moto

Mwendazake alibutuwa kwa β€œtik-tak” kabisa, na mama Samia ameipiga mwiko wa ukweli.πŸ˜ƒπŸ€¦πŸΎβ€β™‚οΈ
 
Yaani hapo ni kuchagua tu kusuka au kunyoa! Ccm ife kifo cha mende kupitia katiba mpya, au iendelee kuitawala nchi kimabavu kupitia katiba ya mwaka 1977!
 
Viongozi wanajua kitakachotokea baadae baada ya katiba mpya, hakuna mtu aliye tayari kwa hilo....
Tuendelee tu kujifukiza.
 
Wa tikitaka hakutaka kumung'unya maneno, alituweka wazi tokea dei wani
 
Katiba mpya ndiyo tosha yanguπŸ€—πŸ€—πŸ€—
 
Kila mtu anaogopa lawama. Kwasababu atayekubali kuunda katiba mpya ndiye atakuwa amefanya mauwaji na mazishi ya CCM.
Tunakumbushana kuwa katiba itaandikwa na wanasheria wabobevu wa sisiem unadhan wataandika kinyume na maslah yao???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…