Jinsi Waarabu wanavyoendelea kutawala soka la Afrika

Jinsi Waarabu wanavyoendelea kutawala soka la Afrika

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Waarabu wameshaonja utamu wa asali ya pesa za CAF kwa hiyo wamejijengea mtandao mkubwa wa kuhakikisha hakuna boya yoyote anakuja kuwanyang'anya asali na himaya yao.

Miaka ya hivi karibuni Simba na Yanga zimejitahidi kufanyafanya usajili na kujifunza mikakati michache ya ndani na nje ya uwanja na tumeanza kushuhudia kumbe Waarabu wanafungika vizuri tu tofauti na zamani, tena wakati mwingine hata nyumbani kwao.

Sasa mimi nadhani hiki ni moja ya kitu wanachofanya. Hawa jamaa wakisikia na wakiona kuna mtu anawasumbua wanakaa kwenye vijiwe vyao vya kahawa na halua halafu wanapanga njama za kumnyofoa pale mbaya wao ili asiendelee kusumbua.

Wanafanya hivyo kwa wachezaji, makocha na hata viongozi.

Wakiangalia katika vyungu vyao wakaisoma nyota ya Kibu wakaona haishikiki na anaenda kuwasumbua, wanawekeana pesa katika kibubu kwa kushirikiana (kumbuka hili ni muhimu) ili kufanikisha jambo lao. Ukiwa boya na vitamaa tamaa vyako unakimbia kufanya nao biashara kumbe ndo wamekumaliza.

Nimalizie kwa kuwauliza nyie waswahili, ukigundua chimbo lenye fursa, huwa unakimbia kuwaambia wengine au unatengeneza mazingira ya kulilinda ili ule mwenyewe na watu wako? Lishikeni hili litawasaidia.
 
Kwa kibu hapana mtoa mada acha uongo hamna timu ya kiarabu inunue garasa siku 400 halijafunga Gori kwenye ligi
Gori ndio nini?

Kwa siku unakunywa kuka ngapi? Na kuvuta bangi ngapi?

Ndugu zako wanajua lakini kama unakunywa kuka na kuvuta bangi?

Waambie ili wakusaidie usiwafiche.
 
Gori ndio nini?

Kwa siku unakunywa kuka ngapi? Na kuvuta bangi ngapi?

Ndugu zako wanajua lakini kama unakunywa kuka na kuvuta bangi?

Waambie ili wakusaidie usiwafiche.
Kuka ndio nini? Bangi ndio nini? Kunywa ndio nini?
 
Ni dhahiri kuwa hatuwezi kushindana na Waarabu kwenye manunuzi.Hata kama Wana nia fiche vipi kuhusu Mchezaji/kocha husika? Kwamba yeye akatae pesa ilu kuwalinda nyie msibomolewe?
 
Back
Top Bottom