ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 83,659
- 90,151
Uanaharakati mavi zaidi ya kuwa uchawi ni hasara kwao na Nchi.Saaaaaafi we waache na uwanaharakati WAO badala wategeshe
Full stop ,kwishaaaa
Uanaharakati mavi zaidi ya kuwa uchawi ni hasara kwao na Nchi.Saaaaaafi we waache na uwanaharakati WAO badala wategeshe
Full stop ,kwishaaaa
Kuumia NAFSI KILA wakisikia neno tajiri masikioni mwao MPAKA najisemea TU Hawa WATU ukiwaiga unaangamia Hawa washa zoea SHIDAUanaharakati mavi zaidi ya kuwa uchawi ni hasara kwao na Nchi.
Yaani yalivyo mapunguani yamefikia mahala Hadi wanataka wawapangie watu nani wa ku associates nae na nani sio.Kuumia NAFSI KILA wakisikia neno tajiri masikioni mwao MPAKA najisemea TU Hawa WATU ukiwaiga unaangamia Hawa washa zoea SHIDA
Full stop, kwishaaaa
Hakika kila nchi ina "untouchable". Muhimu sana kupambana kuingia kwenye circleKawaida tu kila nchi haikosi big fish 🐠, untouchables .kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake.
Kilichofanyika sio uchangiaji bali ni rushwa na hongo zenye kusudi maalumu...Wakuu naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha. Ukweli ni kwamba There is no free kunch in Africa. Kwa kuzingatia hili, hebu tujiulize hawa wafanyabiashara walioichangia CCM mabilioni ya pesa kwa mbwembwe na na hadharani watarejeshaje fedha zao walizochanga? Tukumbuke kwamba hawa wachangiaji ni wafanyabiashara na fedha walizochangua wamezinyofoa kwenye mitaji ya biashara, tena kwa ghafla kwa kushtukizwa kwani uchangiaji huu haukuwa kwenye malengo yao ya kibiashara. Na pia tukumbuke kule CCM hakuna biashara yoyote itakayofanikisha marejesho ya haya mabilioni ya fedha za mtaji wa biashara ambazo wamezimwaga ndani ya CCM.
Sujafuatilia sana jambo hili lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida, wakati nikipita social media, nimeshangazwa kusikia kampuni moja kubwa ya biashara hapa nchini ikitangaza kuchangia Tsh bilioni 10, ambazo ni sawa na 10% ya fedha zilizokadiriwa kuchangwa.
Kabla tujiulize wafanyabiashara hawa watarejeshaje hizi fedha zao, tunapaswa kujiuliza kuhusu matumizi ya michango hii. Hivi karibuni tumeshuhudia CHAUMMA wakinunua maelfu ya magari na kuyasambaza nchii nzima wakati kinafahamika ni chama masikini na hakijawahi kuitisha mchango wowote. Isije ikawa CCM wanajenga kwa jirani huku kwao kukizidi kuporomolewa na akina Polepole na genge lake. Je, CHAUMMA wamepata wapi ghafla fedha za kununua magari haya? Baada ya michango hii huenda watanunua magari mengi zaidi au watapata fedha za kutosha kukodi chopa za kuzunguka kwenye kampeni nchi nzima. Tusubiri tuone itakavyokuwa.
Tukirejea kwenye jinsi fedha za wafanybiashara zitakavyorudi nimeangalia katika nyanja tofauti. Uwanja wa kwanza ni kupitia ukwepaji kodi wa makusudi. Hawa wachangiaji kuanzia sasa watakuwa wakwepaji wakubwa wa kodi kwani wanajua fika kuwa wameishajipenyeza kwenye mfumo wa chama na serikali kama ambavyo Rostam Aziz amefanya. Sasa hivi Rostam hagusiki kabisa. Anaogopeka zaidi ya Rais. Rostam na Kikwete sasa hivi utadhani ndio wanaongoza nchi kwa remote.
Namna ya pili ya kurejesha hizo fedha ni maelekezo kutoka juu. Kwa kuwa sasa hawa wachangiaji wameingia sebuleni mwa CCM watakuwa wanafanya biashara bila kulipa kodi kwa maelekezo kutoka juu.
Namna nyingine ni kwa kuogopwa na maofisa wa TRA na kuachiwa wapite blila kulipa kodi kwa nidhamu ya uwoga. Wakaguzi wa TRA watakapogundua kuwa mizigo inayopita bandarini ni ya mchangiaji wa CCM, hawatamgusa....watamuachia apite bila kulipa kodi.
Mwisho, njia nyingine maarufu itakayotumiwa na mafisadi hawa walioichangia CCM ni kwa kupandisha bei za bidhaa au kupunguza kipimo kwani sasa wanajua fika kuwa wanaogopwa na TRA na wakala wa vipimo na uzito. Hii nchi ukitaka kuila vizuri kaa karibu na CCM.
Je, wewe mdau wa JF, ukitafakari vizuri na kwaa utulivu unadhani ni jinsi gani hawa wafanyabiashara watarejesha mabilioni yao waliyochomoa kutoka kwenye mitaji ya biashara na kuichangia CCM, ukizingatia kuwa CCM hawafanyi biashara itakayozalisha fedha ili wazirejeshe.
Inaumiza sanaFedha zote zipo mikononi mwa mafisadi na zimetejeshwa kwa Chama Cha Mafisadi (CCM).
Wafanyakazi wa Umma je ambao hawajaonhezwaa mishahara Kwa miaka 10? Zaidi ya kudanganywa na bi increment vidogo? Yooote hii kwasababu Kuna watu wanakwepa kodi ama wanapewa mikataba ambayo ni zaidi ya dhuluma Kwa umma. Nchi ngumu sana hii, but there is hope!Hilo nimeliwaza sana nyingine ni kampuni changa wafanya kazi wao wanalia njaa lkn huku kachangia million 200 hii nchi vituko haviishi aloo
Huhitaji nguvu sana Bali a genuine leader ambaye atafuata utawala Bora na yeye mwenyewe akizingatia Hilo. Siyo awe kama Pharaoh akitunga Sheria kwaajili ya commoners huku yeye na kundi lake wakila Kwa urefu wa kamaba zao. Hatuna genuine leaders na wengi Wana moral decayInaumiza sana
Tunahitaji mabadiliko ya kuweza kuwa na mfumo mzuri zaidi ya huu.
Yule PM aliesababisha tukatupa mpaka Radio ya Panasonic chooni, wa hivyo hapana
Huyu alidhani njia hiyo ni nzuri kwa kupata marndeleo.
Wa pili nae aliewashweka ndani matajiri na ili watoke lazima walipe, nalo lilikuwa wazo baya na lillileta chuki baina yetu.
Ukisema kuanzia Rais mpaka mawaziri wawe Wajeda nalo ni baya zaidi, maana watatulaza saa moja
Kila kitu inataka nidhamu lakini sio kama walizotumia baadhi ya mawaziri kwa kufunga Geti eti aliechelewa arudi nyumbani
Hiyo ilikuwa sio kazi ya Waziri
Naona hatujui governance maana yake la sivyo tungefika mahali
Kila anaekuja anataka aongoze anavyotaka.
Wizi umejichimbia mizizi na kuikata inataka maamuzi ya hali ya juu.Huhitaji nguvu sana Bali a genuine leader ambaye atafuata utawala Bora na yeye mwenyewe akizingatia Hilo. Siyo awe kama Pharaoh akitunga Sheria kwaajili ya commoners huku yeye na kundi lake wakila Kwa urefu wa kamaba zao. Hatuna genuine leaders na wengi Wana moral decay
Wajuu akisha onyesha uadilifu na kusimamia mifumo Kila kitu kina fall into lines
CCM ni ukoo wa panya......babu mwizi, baba mwizi, mtoto mwizi, mjukuu mwizi, kitukuu mwizi, kilembwe mwizi na kining'ina mwizi.Wizi umejichimbia mizizi na kuikata inataka maamuzi ya hali ya juu.
Hata ikiwa ku sacrifice kwa mambo kadhaa.
Kama leader akitokea sina maana hawa maana hakuna muadilifu kwa sasa.
Nchi nyingi zimeendelea kwa maamuzi magumu waliofikia
Wengine walinyonga kabisa
MiCCM ndivyo ilivyo.....inahalalisha wizi mchana kweupe!Kilichofanyika sio uchangiaji bali ni rushwa na hongo zenye kusudi maalumu...
Kwanza ieleweke wanachama na wapenzi wa chama cha siasa kukichangia chama kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli zake ikiwemo kugharamia kampeni ni jambo la kawaida na ndivyo ilivyo na ndio maana halisi ya chama cha siasa.....
Kwamba, chama cha siasa siku zote ni mali ya wanachama na wanachama ndio wanaopaswa kukiendesha kwa njia ya kukichangia kupitia mifumo iliyopo kisheria iliyo wazi mfano kulupia ada za uanachama, michango ya hiari nk...
Lakini lililo muhimu kuzingatiwa siku zote ktk ukusanyaji wa michango hii ni sheria na uwazi wa vyanzo vya fedha za wanaochangia ili kuepusha chama kuwa chanzo cha kupitishia pesa haramu (money laundering)....
Aidha ktk nchi zingine zinazotambua hatari ya chama cha siasa kuomba kuchangiwa fedha toka kwa watu, sheria imeweka ukomo wa kiwango ambacho mtu mmoja anaweza kukichangia. Kwa hapa kwetu Tanzania, sijui sheria inasemaje kuhusu ukomo wa mchango kwa mtu mmoja...
Aidha ktk nchi zingine, kampuni au mashirika makubwa ya kibiashara hayaruhusiwi kuchangia chama cha siasa kabisa na lengo ni kuepuka conflict of interests hususani ktk masuala ya kodi....
Mfano, kampuni ya GSM yenyewe peke yake kukipa chama siasa kilicho madarakani zaidi ya Tshs bilioni 11 inaleta maswali makubwa kuluko majibu. Hapa kuna conflict of interest kubwa. Hii kampuni itajenga jeuri na itataka malipo kwa njia moja au nyingine. Wanaweza kukwepa kulipa kodi na serikali isifanye lolote...
Kwa hiyo nakubaliana na wewe kabisa ndugu tpaul kuwa, there is no free lunch not just in Africa but it's in the whole world...
CCM wamelikoroga...
Siyo CCM ila wanaolitumia CCM kama kichaka chakupigaCCM ni ukoo wa panya......babu mwizi, baba mwizi, mtoto mwizi, mjukuu mwizi, kitukuu mwizi, kilembwe mwizi na kining'ina mwizi.
WANAWEZAJE KUPATA USINGIZI? Umenifikirisha sanaa...Inaumiza sana unapoona watu wanakosa maji masafi huku vichanga wakifa kwa kukosa uangalizi.
Unadhani wanashindwa kuifanya nchi iwe na maendeleo ?
Leo sijui tuko wa ngapi kwa umasikini duniani.
Na wanaona ni ufahari kutembea na mabasi zaidi ya 40
Huwa nashindwa kuelewa wanawezaje kupata usingizi?
Walahi inauma sana.WANAWEZAJE KUPATA USINGIZI? Umenifikirisha sanaa...
Ubarikiwe kwa hizi hekima.Walahi inauma sana.
Hii dunia tunapita na tutaenda na sanda tu, halafu kuna mtu anakuambia hivyo vijisenti ?
Mungu awape moyo wa ubinadamu
Sina la kuongeza
AmiinUbarikiwe kwa hizi hekima.
State capture in the makingWakuu naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha. Ukweli ni kwamba There is no free kunch in Africa. Kwa kuzingatia hili, hebu tujiulize hawa wafanyabiashara walioichangia CCM mabilioni ya pesa kwa mbwembwe na na hadharani watarejeshaje fedha zao walizochanga? Tukumbuke kwamba hawa wachangiaji ni wafanyabiashara na fedha walizochangua wamezinyofoa kwenye mitaji ya biashara, tena kwa ghafla kwa kushtukizwa kwani uchangiaji huu haukuwa kwenye malengo yao ya kibiashara. Na pia tukumbuke kule CCM hakuna biashara yoyote itakayofanikisha marejesho ya haya mabilioni ya fedha za mtaji wa biashara ambazo wamezimwaga ndani ya CCM.